Kwa kuwa VODACOM wamekiri kuwa wanashirikiana na watu wasiojulikana ambao wameshindwa kuwataja kwa majina yao walio toa Amri kumzimia mawasiliano Kabendera.
Na kwa kuwa Voda wameamua kuacha Biashara yao halisi na sasa wamekuwa Genge la ujasusi.
Na kwa kuwa wamevimbiwa faida tunayo wapa kwa kutumia mtandao wao.
Na kwa kuwa VODA sasa wanashiriki kumwaga DAMU za wa TZ na kuzitumia kama Minara ya simu.
Ndugu zangu Kila mpenda Amani, Umoja na Haki shiriki kikamilifu kuondoa kampuni ya Voda hewani.
Usidanganyike na Mawakala wao wapuuzi wanao kuja hapa na hoja dhaifu eti hata huko mitandao mingine wanafanya kama VODA kwahiyo hakuna kwa kukimbilia.
Voda tunao uhakika na hata wao wamekiri kushiriki kutenda uovu na unyama kwa raia wema. Ni lazima tuwachukulie hatua stahiki kwa kuwakataa.
Jambazi Akikili kuwa ameua mtu ila alifanya hivyo kwa kuwa aliamliwa na mkuu wa majambazi haina maana kuwa jambazi huyo ni mzuri kwa kuwa kaongea ukweli. Tunawapinga Makaburu Vodacom pamoja na genge lenu lote la uharifu.
Tanzanzania ni kubwa na ya thamani kuliko VODA na genge lake la uhaini. Uhai wa Mtanzania una thamani kuliko Mtandao wa VOda na genge lao la utekaji watu nyara.
Vodacom Sio MAMA yetu, mlitukuta watanzania tukiishi vizuri kwa Amani na Utulivu mkaomba tuwape ruhusa na ninyi mkae na sisi lakini sasa mmegeuka kuwa Janga.
Voda mlitukuta na Mtaondoka na Kutuacha. Sio lazima kutumia mitandao ya kampuni ambayo ni hatari kwa usalama wetu.
Tukiona mitandao yote haina usalama, tutatumia email, watsap call au tutapanda mabasi mpaka eneo husika kupeleka taarifa kama tulivyo kuwa tukiishi kabla ya mitandao ya simu. Uhai unathamani kuliko Simu.
BAI BAI VODA.