Kampeni ya kuikataa Vodacom

moja kati ya makampuni yaliokuwa na jeuri sana na masoko yao ni HUAWEI, ona sasa kilichotokea, Consumers ni consumers chembe moja tu ya mchanga inaweza kuleta madhara makubwa katika uhalisia wa biashara, Makampuni yanahitaji sana wateja kuliko wateja wananavyohitaji makampuni. Mgomo huu ni mzuri kwa upande mmoja maana yatayafanya makampuni yasibweteke na sasa wataamua kufanya biashara na wananchi ama kujikita kwenye kuvujisha taarifa zao. Tunataka kampuni za simu zilizo strong zenye kulinda faragha ya wateja wake. Ni sawa na gesti ama hoteli, fumanizi zikizidi wateja wanakimbia, Law of motion. Nasema wananchi wamechelewa sana kuanzisha mgomo huu. Marekani ukihitaji kudukua kwanza unaenda mahakamani kutafuta kibali na si jambo la rahisi hata kidogo. Na sisi tufike huko maana tunawatengenezea hawa jamaa faida kubwa sana kwa nini wasitulinde
 
Kuna umuhimu wa kutoa elimu juu ya somo la udukuzi hapa JF..
Siyo Kila Mtu Anadukuliwa, Jambo Hilo Hufanyika Maalum Pia Watu Hawajui Nini Maana Ya Kuyaweka Makampuni Sambamba.
Yaani Airtel, Vodacom, Halotel, Tigo
 
Bakini na milaini yenu ya voda ila wenye akili timamu kama sisi hatuwezi kuendelea kuvumilia upuuzi wa wapuuzi.. Kwanza wamewahi kunizima 30000 kwenye mpesa mpaka leo kimya.
 
Watu wakubwa huwa wanaona mbali sana
 
halafu mpaka wasomi kabisa na akili zao, eti....wanaacha kutumia VODA!!! wakati ni mitambo ya TCRA na makampuni yote wanafanya hivyo
 
Kama una mambo ya hovyo lazima utadukuliwa hata tutumie mtandao gani!Sihami Voda ng'o...
 


unawaonea voda

wamepewa amrri na TCRA, na mkataba wao na leseni yao ilisema kabisa serikali ikihitaji chochote kutoka kwao watatoa

HII SIO KWA VODA TU NI MAKAMPUNI YOTE YA SIMU, kuna wakati tumieni akili zenu ngau kidogo tu
 
Siku wakitoa siri zangu nitaacha kuitumia ila kwa sasa sina sababu ya kuacha.
 
tunahama kama huwezi hama wewe baki ili kuonyesha nguvu ya uma tunahama voda
 
hashtag boycottvodacom
 

umefanya hayo kwa sababu ya ujinga

kampuni gani hawatoi mawasiliano wakiamriwa na TCRA, wakiamriwa na serikali??

umejipa hasara na umefuata mkumbo

makampuni yote wanafanya hivyo na sio kosa lao Voda

hivi wasomi mnawaza nini siku hizi??
 
Siyo siri kua serikali karibia zote zinamonitor mawasiliano ya watu wake.

Wakati mwingine hata serikali ya nchi C humonitor mawasiliano ya nchi A.

AU ilikua ikiibwa taarifa zake na serikali ya China. Sijawahi kusikia nchi yeyote imeishtaki China. Na China wamefuatilia hizo taarifa illegally.

Vifaa vya Huawei inasemekana vinakusanya data mbalimbali bila wewe kujua na kuzipeleka kwa serikali ya China. USA imezuia maofisa wake wa serikali kutotumia bidhaa za Huawei. Hapa Tz sijaona katazo.

Vitu serious kama hivyo ambavyo vimefanywa illegally siyo Halima wala mtu yeyote Tz ambaye amevisemea. Voda imetenda kwa kufuata matakwa ya serikali, JF ilipishana na serikali na tunajua ilikua off air kwa muda gani.

Same shit happening to Voda ingekua na hasara kuliko watu wachache kuhimizana kuiacha Voda.

Mtu mwingine atanipa mfano wa Apple kugoma kutoa password ya Iphone 5 ya yule gaidi. Lakini naomba ajiulize Apple wanaoperate nchi ya namna gani na Voda wako nchi ya namna gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…