Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

J.K Amemteua Ernest Mangu kuwa IGP akichukua nafasi ya Said Mwema. Hiyo kwangu siyo habari. Nnachojiuliza ni kwa nini Mwema ame step- out wakati juzi juzi kuna taarifa zilitoka kwamba yeye Mwamunyange, na mwenzie wa usalama wa Taifa wanatakiwa kuendelea. Au anaogopa safari za Uholanzi

Swali lako la msingi sana... Haiingii akilini kabisa
 
Kaniki ana LL. B na LL. M ...UDSM afu ni wakili msomi wakujitegemea! PhD student too!
 
Nafukiri amepima upepo na kuona unavuma ndivyo sivyo.
 
Itabidi Polisi waangalie namna wanavyogawa vyeo vyao kwani vinachanganya. Uko sahihi ingawa iko hivi:

CP Mango aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Intelijensia ya Jinai, kwa Kiingereza wao Polisi wanaita Director of Criminal Intelligence. CP Mngulu akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa UChunguzi wa makosa ya Jinai na kwa Kiingereza wanaita Director of Criminal Investigation.
Asante mkuu kwa somo sikujua kama kuna DCI wawili
 
sijui tunatumia katiba gani kuweka vyeo, utasikia mara waziri na waziri msaidizi, naibu na naibumsaidizi kesho wameondolewa tumerudi na waziri mmoja tu, mara tunaweka division 5 na zero, kesho wanaiondoa,oh michezo inafutwa mashuleni kesho inarudishwa, mawaziri wameteuliwa kesho wanaondolewa.na sasa cheo kipya kinaundwa kesho kitaondolewa, sijajua tunatumia dira ama katiba gani kuendesha hii nchi. kikubwa nachoona tunafanya majaribio katika kila jambo.
 
Huyu ndie alikuwa mshauri wa Mwema kwenye mambo ya intelijensia, viongozi wa ccm wanabaka na kutishia kuua wako uraiani wanakula bata, polisi wanapikea rushwa utadhani ni stahiki yao, raia wema wamekufa kwa mashinikizo ya kiutawala, i.e Arusha, Moro, Iringa, etc intelijensia uko kimya, leo mnampa kuwa IGP!!!!!! Mvinyo ni ule ule wa zamani kwenye chupa mpya. Huenda udhaifu wote tunaiuona kwa Mwema huyu ndie source, hata rais kaona hilo ndio maana kampa msaidizi.
Nakubaliana na Mh Warioba hawa watu wapitishwe na bunge iki vyeo vya fadhila viishe.

Unajua ukamishna wa intelijensia amepata lini, hata mshahara wake hajala, sasa unajifanya unamfahamu!
Mwezi uliopita ndio kateuliwa kuwa kamishna akitokea RPC Mwanza. Ila amewahi kuwa ADC wa IGP Omary Idd Mahita.
Kuweni makini na wanaozusha uongo kuhusu viongozi wenye sifa zilizotukuka.
 
Hii inatokana na mabadiliko kwenye muundo wa majeshi ili ufanane na nchi zingine hasa zile za SADC. Hili lipo hata Zimamoto

Sasa SADC ndo nchi yetu, katiba lazima iheshimiwe na watu wote, si angepeleka kwanza mabdiliko ya katiba, au asubiri hii mpya.
 
Kwenye position zenye majina kama haya ,hautasikia watu wakipigia kelele udini. Leo nimeprove wadini ni watu gan nchi hii!
 
Atawaondoa awapeleke wapi?..hilo ni jeshi,huwezi kumtoa CCP aende akawe mkuu wa kituo..na huwezi kumwachisha kazi bila kosa lenye kuwa na ushahidi.

Easy..na yeye Mangu aunde kitengo kipya awapeleke huko kwani hawezi fanya kazi zake vizuri na watu waliokwisha chafuka kwa makashifa lukuki ndani ya jeshi
 
Ni tukio la kustukiz sana ... lakini kikubwa kamanda Mangu ameanzia chini... Koplo ... mpaka IGP kweli inawezekana ikawa ni chaguo sahihi... HONGERA SANA MUNYAMPAA
 
Wakati wowote kunapotokea uteuzi unaohusu mtu ambaye hakutarajiwa, lazima tuupongeze. Yalishasemwa mengi na majina kutajwa, lakini Boss hakuona hivyo. welldone Boss. Tunatarajia hata katika kujaza nafasi za mawaziri Rais atafanya surprise. Walokwenda Bagamoyo kwa babu shauri zao.
 
Tatizo la kikwete ni kuvunja katiba kiholela, yeye kupachika watu hovyohovyo ni kawaida yake!
 
Tumuunge mkono tumsaidie akiboronga ndio tumfundishe na kumpinga tumpe nafasi kwanza.
 
Tatizo la kikwete ni kuvunja katiba kiholela, yeye kupachika watu hovyohovyo ni kawaida yake!

Mkuu, sasa raisi amevunja vipi tena katiba?

Raisi amemteua IGP mpya na kuongeza nafasi ya msaidizi wa IGP nafasi ambayo haijawahi kutokea tangia uhuru.Hii ni kutokana na madaraka alopewa raisi na katiba hiyohiyo.

Sasa katiba inasemaje kuhusu uteuzi wa IGP?

Tafadhali, kwa heshima na taadhima naomba ufafanue mkuu.
 
Unajua ukamishna wa intelijensia amepata lini, hata mshahara wake hajala, sasa unajifanya unamfahamu!
Mwezi uliopita ndio kateuliwa kuwa kamishna akitokea RPC Mwanza. Ila amewahi kuwa ADC wa IGP Omary Idd Mahita.
Kuweni makini na wanaozusha uongo kuhusu viongozi wenye sifa zilizotukuka.

......Vijana wa Omar Mahita (Andengenye na Mangu) nyota zao zinawaka waka.........

Ni tukio la kustukiz sana ... lakini kikubwa kamanda Mangu ameanzia chini... Koplo ... mpaka IGP kweli inawezekana ikawa ni chaguo sahihi... HONGERA SANA MUNYAMPAA

...pamoja na hilo......Uteuzi wa IGP Mangu ni Compromise ya mambo mengi!.....bila ubishi wowote hii nafasi ilikuwa apewe Andengenye......jambo ambalo limemkosesha Thobias U-IGP ni malalamiko ndani ya Jeshi la Polisi......angeteuliwa.....sehemu kubwa ya Jeshi ingekuwa demoralised.....kwani kijana amepanda vyeo kwa kasi ya ajabu.....kiasi kwamba imeleta manung'uniko kutoka kwa maafisa wengi waandamizi.......suala la ukabila na upendeleo alilonalo Mangu ni rahisi kulidhibiti...... lakini morale ya wafanyakazi sio rahisi kuidhibiti.......kuthbiti morale ni very expensive........
 
Back
Top Bottom