Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

......Vijana wa Omar Mahita (Andengenye na Mangu) nyota zao zinawaka waka.........



...pamoja na hilo......Uteuzi wa IGP Mangu ni Compromise ya mambo mengi!.....bila ubishi wowote hii nafasi ilikuwa apewe Andengenye......jambo ambalo limemkosesha Thobias U-IGP ni malalamiko ndani ya Jeshi la Polisi......angeteuliwa.....sehemu kubwa ya Jeshi ingekuwa demoralised.....kwani kijana amepanda vyeo kwa kasi ya ajabu.....kiasi kwamba imeleta manung'uniko kutoka kwa maafisa wengi waandamizi.......suala la ukabila na upendeleo alilonalo Mangu ni rahisi kulidhibiti...... lakini morale ya wafanyakazi sio rahisi kuidhibiti.......kuthbiti morale ni very expensive........

Mangu kabila gani?
 
Tutajie tofauti kubwa hiyo.
How you perform investigation without involving intelligence ?
Kama kuna anayejua role Director of Criminal Investigation na Director of Criminal Intelligence atusaidie tafadhali
Of course mara nyingi tulikuwa tunamsikia Director of Criminal Investigation kidogo tunajua role yake sasa huyo mwingine.....?

Huyo wa Intelligence ni wa kudhibiti MAANDAMANO ya CDM na huyo wa Criminal Incestigation ni wa kukamata wauza gongo, mirungi na Bangi
 
Huyo wa Intelligence ni wa kudhibiti MAANDAMANO ya CDM na huyo wa Criminal Incestigation ni wa kukamata wauza gongo, mirungi na Bangi

Hakika Kamanda Mangu anastahili nafasi hiyo 100%,ni mmoja wa wachapakazi hodari saaana waliowahi tokea,tumuunge mkono jamani huu ni wakati wa wachapaka kazi kama abdulrahman kaniki,athuman diwani,thobiasi andengenye,david misime na faustine shilogile.,ahsante saana mwema kwa uongozi uliotukuka pamoja na changamoto mbalimbali ndani ya jeshi la police,pia hukuwa na tamaa ya madaraka ya kutaka kuendelea na kazi,Hongera saana kea Hili..,Ni wakati wa kupimzika kwa hiari sasa makamishima hawa mtweve,chagonja,kova na mngulu mpishe wachapakazi walio na hari na kutekeleza majukumu yao kwa haki,hekima,busara,bila kupendeleana na kutimiza wajibu wao kipolice......
 
Chonde chonde huyu naibu IGP ajipange vzr asije kukosa mafao yake kama mzee wetu Mrema ambae cheo chake kilikuwa hakipo kikatiba mpaka leo anadai mafao na hajayapata
 
Tumuunge mkono tumsaidie akiboronga ndio tumfundishe na kumpinga tumpe nafasi kwanza.

ni kamanda bora,mpeni muda mtaona matunda yake ndani ya jeshi la police...pamoja na majembe kama kaniki,andengenye,diwani na hawa ambao hawajapandishwa charls mkumbo,shilogile wa moro,na misime wa dodoma wapewe nafasi ni wachapakazi saaanaaa kwa vitendo na sio bla bla bla kama wengine...makamishina wa zamani pumzikeni msaidiwe kazi kwa hiari...
 
......Vijana wa Omar Mahita (Andengenye na Mangu) nyota zao zinawaka waka.........



...pamoja na hilo......Uteuzi wa IGP Mangu ni Compromise ya mambo mengi!.....bila ubishi wowote hii nafasi ilikuwa apewe Andengenye......jambo ambalo limemkosesha Thobias U-IGP ni malalamiko ndani ya Jeshi la Polisi......angeteuliwa.....sehemu kubwa ya Jeshi ingekuwa demoralised.....kwani kijana amepanda vyeo kwa kasi ya ajabu.....kiasi kwamba imeleta manung'uniko kutoka kwa maafisa wengi waandamizi.......suala la ukabila na upendeleo alilonalo Mangu ni rahisi kulidhibiti...... lakini morale ya wafanyakazi sio rahisi kuidhibiti.......kuthbiti morale ni very expensive........

Andengenye muda wake bado haujafika pia
 
Hivi kweli jf members wameshindwa kujadili swala la uwepo au kutokuwepo kwa nafasi ya Naibu IGP kwa hoja zaidi udini? Nani aliyesema nafasi za utumishi zinajazwa kwa uwiano wa kidini? Wasio na dini sasa hawana nafasi tena?!

Kama udini ndio hoja na sifa ya kujadili nani katwambia dini zao? Majina yanatosha kuonyesha dini ya mtu, swala la imani! Wekeni ushahidi wa dini zao basi, maana hata hizo dini mnazowagawia hao watu yamkini sio zao.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya intelligence na investigation. Intelligence kwa maneno machache ni utaratibu wa kukusanya taarifa mara nyingi kwa njia ya siri na kuzifanyia analysis ili kupata usahihi wa taarifa hizo. Katika muktadha huo, Directorate ya Criminal Intelligence ina wajibu wa kukusanya na kutafuta taarifa kuhusu uhalifu wa kijinai hata kabla ya kutokea kwa uhalifu huo. Mathalani, kama kuna mtu au kikundi cha watu kinakusudia kufanya aina fulani ya uhalifu ni jukumu la Directorate hii kupata taarifa za mtu au kikundi hicho kabla hakijafanya uhalifu husika na kuchukua hatua stahiki za kuzuia uhalifu huo. Hiki si kitu kipya kwa Jeshi la Polisi bali sasa kitengo cha intelligence kilichokuwa chini ya DCI kimeimarishwa kuwa Idara kamili. Hii ni kama ilivyo kwa Military Intelligence kwa jeshi lolote ikiwemo TPDF. Kwa upande wa investigation, huu ni uchunguzi wa makosa ya jinai ambayo tayari yameshatendeka. Kusudi hapa ni kupata ushahidi wa kuthibitisha uhalifu wa kijinai uliotendeka mahakamani. Kuteuliwa kwa Naibu IJP kunafuatia muundo mpya wa Jeshi la Polisi ambao pamoja na mambo mengine umeongeza Idara na vitengo ambavyo awali havikuwepo katika Jeshi la Polisi. Ongezeko la Idara hizo linahitaji uwepo wa Naibu IJP wa kusaidia usimamizi na uendeshaji wa shughuli za jeshi. Hii ni kama ilivyo kwa TPDF ambapo kuna Chief of Staff ambaye hushughulikia masuala ya kila siku ya utawala ndani ya jeshi.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Huu mfumo utakuwepo hadi katika ngazi za Mikoa hadi Wilaya?
 
kwa katiba gani, na unaanzaje tu ghafla?

Nadhani Katiba haitoi muundo mzima, inaongelea uwepo wa Jeshi na mfumo wa kuliongoza, kwani unayo Katiba inayotaja cheo cha RPC? au RCO au hata DCI?

Katiba ni Sheria mama, zipo Sheria elekezi, regulations, standing orders nk Kama Katiba haitaji hata wizara Rais anafuta kuongeza na kupunguza kulingana na matakwa yake iweje unahoji hili dogo.
 
Kwa vigezo gani au kuongea itakuwa ulisaidiwa ndio maana unaongea

Nilisaidiwa kuongea vipi? Huyu afande ukifuatilia kesi za ugaidi za ubalozi wa Marekani ndio utajua ni nani,, ana vigezo, upeo na kujiamini. Amekuwa mwalimu wa masuala ya upelelezi wa kimataifa, uliza Marekani, Ujerumani,, Uingereza, Kenya,, Uganda, Rwanda n.k they know him.
 
Wote wanaolalamika kuhusu udini hawana hoja na malalamiko yao yameegemea zaidi kwa kuangalia majina ya watu na wala hamna hata mmoja aliesema anasali kanisa moja na “Ernest” kwa hiyo anamjua kuwa ni mkristo safi au anaswali msikiti mmoja na “Abdurahman” kwa hiyo ni mwislamu safi. Wote wanaangalia majina tu na kuanza kulalamika udini inabidi sasa Serikali ianze kuteua watu na kutangaza kwa majina yetu ya kibantu kama vile IGP wangesema ni “mangu” na msaidizi wa IGP ni “Kaniki” sidhani kama hizi comment za udini zingekuwepo. Tuachane na haya masuala ya udini jamani...tutakosa wachapakazi na waadilifu kisa dini....
 
Back
Top Bottom