Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Si tulisikia kuwa IGP - Msataafu Said Mwema kaongezewa miaka 2?? Ilikuwa zuga??

Ina maana hujajua kuwa operation Tokomeza inamgus pia Mwema? ni bora amekimbia kuliko kungoja kutimuliwa.
 
Naona watu wengi wanahusisha uteuzi na Operation tokomeza ujangiri,pamoja na kuwa JF kila siku ndo chanzo kikuu cha habari na elimu lakini inaonyesha jinsi watanzania wengi tusivyo makini na current issues.Mwema anastaafu kwa mujibu wa sheria kulingana na umri wake kutimia,alitakiwa kustaafu June 2013 akaongezewa miezi 6 ndo inaisha leo.Kwa hiyo hajastaafishwa bali ni kwa mujibu wa sheria.
 
Jamani mnakera sana kila wakati mnaongelea DINI DINI1 Ujinga mkubwa!
 
Lakini tukirudi Nyuma...Mwinyi (Rais wa awamu ya pili) alimteuaA. Mrema( Mb) kuwa Naibu waziri mkuu...!Na inasemekana Mrema analipwa masurufu ya nafasi hiyo ya Unaibu waziri mkuu. Swali, Je.Mwinyi Alikiuka Katiba?

Hicho ulichokiandika unatakiwa kukipigia mstari, nafasi ya waziri mkuu na makamu wa rais zimetajwa katika katiba ya nchi hivyo kama kungehitajika kuwa na makamu wao zingewekwa kwenye katiba hivyo unapotenda tofauti ni kinyume na katiba na hivyo umesigina katiba uliyoapa kuilinda kwa sababu zako binafsi, maana sidhani kama hao huwa hawajui ama washauri wao huwa hawalijui hilo. Anyway labda tuseme kama aliyepata kuwa mkuu wa mkoa wa DSM na katibu mkuu wa CCM kuwa "Mkubwa hakosei" lakini viongozi wa namna hii hawaitakii nchi yetu mema.
 
How comes mkuu? Yaani kaingiaje hapa huyo marehemu?
...hata mimi kanichanganya lakini huenda labda alimaanisha ndie kamfanya Kamanda Mangu apelekwe Mwanza na kisha kuonekana kwenye ramani ya uteuzi..... ni mawazo yangu tu haya, mwenyewe atudadavulie
 
Mwema aliongezewa mud a ila kwa sakata la 'TOKOMEZA' ilipaswa aachie ngazi akaamua astaafu ghafla kuepuka kuwajibishwa,kwa ufupi meli imezama ikikaribia ukingoni....pole sana Mwema kwa kushiriki dhambi ya kuwaumiza watanzania
 
Atakayechukua nafasi ya Saidi Mwema kama IGP Ni Kamishna Ernest Mangu.

Ataapishwa kesho.

8850079_orig.png

Ernest Mangu

​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua
​

nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

============
Wasifu wake:

​
hongera sana baba,mungu akuongoze,walitegemea watapewa wale maarufu wanaolichafua jeshi makao makuu dsm,pangua pangua wote na makundi yote hapo makao,ukitaka kufanikiwa baba waondoshe wote waliokuwa na mzee mwema na pendekeza wengine kutoka mikoani ambao hawana umaarufu,kuna watu hapo makao makuu wanajifanya km kwamba jeshi ni la kwao ni hao wanaoharibu utendaji hd kufikia Nchimbi kufukuzwa kazi.
 
Atawaondoa awapeleke wapi?..hilo ni jeshi,huwezi kumtoa CCP aende akawe mkuu wa kituo..na huwezi kumwachisha kazi bila kosa lenye kuwa na ushahidi.
 
J.K Amemteua Ernest Mangu kuwa IGP akichukua nafasi ya Said Mwema. Hiyo kwangu siyo habari. Nnachojiuliza ni kwa nini Mwema ame step- out wakati juzi juzi kuna taarifa zilitoka kwamba yeye Mwamunyange, na mwenzie wa usalama wa Taifa wanatakiwa kuendelea. Au anaogopa safari za Uholanzi
 
Afande Said Ali Mwema amestaafu rasmi tangu tarehe 26/12/2013, kila heri kwake..
Afande Mangu ni mtu mwenye upeo mkubwa, msomi na anasimamia sana taratibu za kijeshi.
Hivyo tutegemee kuendelea kuboreshwa kwa nidhamu ya askari, hongera kwake.
Afande Abrahaman Kaniki ni msomi pia, anapenda sana kufundisha na kujifunza hivyo ni sahihi kwake kuwa mshauri wa IGP, nampa hongera pia.

Asante kwa ufafanuzi mzuri ila ninachoamini mpaka sasa ni kuwa kuna vitengo hata umchukue msomi gani atachemsha tu kwakuwa wengi atakaoenda kufanya nao kazi hawajasoma kwahiyo automatically msomi ata disolve na kuanza kutekeleza maamuzi ya hisia zaidi na zaidi kufanya hata yaliyo nje ya sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom