Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kuna thread humu siku zilizopita zilimtuhumu huyu Kamishna kwa tabia ya Ukabila kwamba polisi wanaotoka kwenye makabila ya Mkoa wa Singida alikuwa anawabeba sana vipi tuhuma hizo zimeishia wapi?

Sijui lakini mimi ninadhani Thobias Andengenye angefaa zaidi.
Hiyo tabia ya ukabila haishi mpaka mtu anakufa,just wait and see.
 
ule upanga wa dhahabu anaenda nao Moshi?

Tumeshukuru kwa kiasi fulani JK kuliona hili kwani madudu ya Polisi Ex-IGP alikuwa anakula kobisi na kuacha jamii ikitesa kwa matukio ya kiuarifu.
 
Enzi ya Nyerere uongozi ulikuwa ni Utumishi lkn kwa sasa ni KUULA,,,! ndomana mtu akiteuliwa anaangusha PART cyakitoto kujipongeza!

sababu ni kuwaza juu ya kupiga deals za kutosha, ndiyo maana watu wanajipongeza!!
Mwisho wa siku wanakuja kuachia madaraka yako kwa aibu.
Haswa pale baadhi ya deals zinapokwama.
 
Je katiba inaruhusu cheo cha Naibu IGP?? au ni kubalance dini???? kwa kuwaumiza waTZ ambao serikali yao haina dini??? Naibu wa NINI???<br><br type="_moz">

Hii inatokana na mabadiliko kwenye muundo wa majeshi ili ufanane na nchi zingine hasa zile za SADC. Hili lipo hata Zimamoto
 
Tumeshukuru kwa kiasi fulani JK kuliona hili kwani madudu ya Polisi Ex-IGP alikuwa anakula kobisi na kuacha jamii ikitesa kwa matukio ya kiuarifu.

kwani alikuwa ana kula bila kumshirikisha mkubwa wake?
 
Atakayechukua nafasi ya Saidi Mwema kama IGP Ni Kamishna Ernest Mangu.

Ataapishwa kesho.

8850079_orig.png

Ernest Mangu

​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua
​

nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
​

naamini hii ni matokeo ya operesheni tokomeza...
 
Sasa naanza kuamini kwamba jamaa ni mdini, yani miaka yote IGP ni muislam. Safari hii kateua mkristo, eti katengeneza na cheo cha naibu IGP ambaye ni muislamu

Yeah! Hata mimi naamini kuwa jamaa (JK) kweli mdini. Maana hata IGP OMAR MAHITA alimteua JK. Ha ha ahaaaaaa. akili hizi nyingine zimejaa pumba...
 
Kwa hali ya mambo ilivyo sasa Kamisna Mangu ni mtu sahihi kwa nafasi aliyoteuliwa kuisimamia sasa...ni mweledi na ni mtu anayejua ni nini cha kufanya na ni kwa wakati gani afanye!

Hongera bwana Mwema kwa kustaafu kwa mujibu wa sheria japo habari za chini ya Zulia zinadai ni kwamba ulipewa ofa na bwana mkubwa ili umsaidie kipindi chake ila kufail kwako kupima athari za hako ka OTU kumemlazimu mkuu kukuondoa tu kulinda heshima yako kwa kigezo cha umri ila ulistahili kupitia mlango wa bwana Nchimbi and company!
 
Hongera sana mkuu,
Naamini utazidi kuimarisha jeshi letu la polisi.

Hongera pia JK walau umekonga nyoyo za wale wa mfumo Kristo.[/QUOTE]

Sikujua kama na wewe pia ni mnafiki wa masuala ya kidini!
 
Jakaya kwa usanii tu, sisi tunamzungumzia Pinda yeye anaibuka na Wema.
 
Tumpongeze mangu kwa uteuzi,na tumtakie utekelezaji mwema wa majukumu yake,nyie mnaosema cheocha naibu iGP hakifai,mkulu jaona kinafaa ya nini malalamiko? Subirini na nyie muwe maraisi mkiondoe,halafu bado mnahoji kwanini naibu iGP ni mwislamu na mnahitimisha jk mdini,kwa nini watanzania ambao mko tofauti na dini ya jk mnamuita jk mdini? Angeteua IGP muislamu mngesema mdini,kateua sio muislamu ila naibu muislamu jk mdini,kwa hiyo kwenu nyie ambao mko tofauti na dini ya jk ni kwamba akiteuliwa kiongozi yeyote lazimz awe tofauti na dini ya jk hapo jk hana udini,ila akiwa ini sawa na yeye basi jk mdini. Mimi nadhani mngeanza kuwaambia maaskofu kwanza waache udini,kama ule wa 2010 kutaka watanzania wamchague mwanakondoo kwenye uchaguzi mkuu,ndipo mrejee kwa mkulu.
 
IGP Mteule E.Mangu ni jembe la ukweli cool contented na msomi mwenye uzoefu wa kutosha katika ofisi ya IGP.
Tunategemea mabadiliko ya ukweli jeshi la polisi.
Hongera sana Mkuu.
 
Atakayechukua nafasi ya Saidi Mwema kama IGP Ni Kamishna Ernest Mangu.

Ataapishwa kesho.

8850079_orig.png

Ernest Mangu

​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua
​

nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
​

Ilishatabiriwa hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/558287-mrithi-wa-igp-watatu-wapitishwa.html na Ezekiel Kamwaga wa Raia Mwema.

"Faida Katika majina haya matatu (Thobias Andengenye, Ernest Mangu na Diwani), ni Mangu pekee ambaye amepitia CCP kulinganisha na wenzake. Kama atateuliwa kuwa IGP, itakuwa ni kuendeleza utaratibu wa kuwapa nafasi waliopitia katika chuo hicho"
 
IGP Mteule E.Mangu ni jembe la ukweli cool contented na msomi mwenye uzoefu wa kutosha katika ofisi ya IGP.
Tunategemea mabadiliko ya ukweli jeshi la polisi.
Hongera sana Mkuu.

uzoefu wa ofisi ni moja ya sababu inadumaza huduma nyingi sana hapa tanzania.
 
Back
Top Bottom