Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

Hakika
Kuna mwanafalsafa aliwahi sema

"free things are never served with respect, learn to hustle"

Leo hii Sirro anakua balozi same as Polepole tena Zimbabwe huku akina Hoyce Temu wakipewa balozi nchi nzito nzito huko Ulaya.
 
Pongezi nyingi. Sasa ni muda wa kuchapa kazi kwa weledi na maarifa na kwa kutanguliza masilahi ya Nchi yetu
 
Hongera Wambura
Kuchapa kazi kinalipa.

Ninamkubali alipokuwa kinondoni kabla kuhamishwa majambazi yalinyooka na kushika adabu

Hata mama Samia aliwahi.muongelea kama akilalamika uhamisho wake.akihutubia .Ali sent message sijui kama wasikilizaji wahusika walielewa ile meseji.

Kifupi majambazi nchi nzima yajiandae
Wambura ndio.eneo lake analolipenda yatakiona cha mtema kuni.
Mtaelewa lini kwamba nchi hii itakuwa bora zaidi kama itakuwa na taasisi imara badala ya kusifia sifia tu??
 
Majungu na fitina havina nafasi katika awamu hii ya 6.

Kamwe viongozi wetu wasikubali kuyumbishwa na kelele za wahuni wachache wenye wivu na chuki binafsi.
 
CCM watu wabaya sana... Wanakutumia halafu wanakutupa jalalani bila hata ya kugeuza sura zao kuangalia umeangukiaje huko jalalani.
 
Rais yoyote mwenye Akili Timamu ni lazima tu atateua Watu wa kutoka Kanda Maalum ( Kwetu Mkoani Mara ) kushika hizi Nafasi za Taasisi Nyeti na za Kimedani.

Kiulinzi na Kiusalama nchi ikiwa chini ya wana Medani wa Mkoani Mara ( Musoma ) itakuwa salama muda wote na Wananchi watafurahi.

Hongera yako sana Poti wangu wa Kikurya na Kizanaki IGP Wambura ila usiache tu mara moja moja kuja Kijiweni Mbezi Beach kwa Mzee Juma ( Mpwae Mzee Nimrod Mkono) kula Nyama na kupiga nasi Stori Nduguzo Wazanaki.

Pia usiache kwenda kuwatembelea Wazee wako unaowaheshimu na Kuwapenda kutokana na Utendaji wao mkubwa na Uliotukuka wenye Uzalendo kwa Taifa hili Wazanaki Wawili akina Mzee Butiku pale Kwake Mabwepande na yule Mwingine ( namhifadhi ) aishiye Jirani na Coco Beach ambao ndiyo walikuwa Mwalimu Nyerere's Think Tanks na bado wanaendelea kutumika Kiushauri mpaka sasa.

Wana Mara ( Musoma ) tunakuombea Majukumu mapya mema, Usiogope, Usitishwe, Jiamini, usimuangushe Rais Samia na mtangulize mno Mwenyezi Mungu kwani najua kuanzia sasa idadi ya Maadui zako itaongezeka.

Mengine nitaongea nawe Inbox Oky?
Kumbe ni Member wa JF?!
 
Kuna mwanafalsafa aliwahi sema

"free things are never served with respect, learn to hustle"

Leo hii Sirro anakua balozi same as Polepole tena Zimbabwe huku akina Hoyce Temu wakipewa balozi nchi nzito nzito huko Ulaya.
Polepole Yuko Malawi hapo mzee wangu
 
Hili la kumuondoa Siro limechelewa sana. Huyu bwana hakustahili kuwepo ofisini muda mrefu sana.
Tatizo la Tanzania ni kulindana bado anaendelea kutumia pesa za walala hoi.
Kuna mahali Mh. Rais kapotoshwa, Kingai hakustahili kuwa Dci. File lake halistahili hicho cheo. Kingai sio msafi.
 
Kingai kapandishwa cheo,anakuwa DCI!this is like tap on shoulder!mama anatumia the same script aliyotumia mwendazake,anayechukiwa,ndio unampa cheo zaidi,kama alivyokuwa makonda kwa JPM,sasa huyu mwamba aliyekuwa anaandaa kesi za mchongo Ili kufunga wapinzani,leo anakuwa bosi wa idara ya kuchunguza kesi,"mwenye sumu kaingia hotelini kula,akaambiwa na mwenye hotel,njoo uwe mpishi kabisa jikoni"walaji hawapo salama.
Kingai atakuwa amepewa asante kwa kazi ya kijinga aliyopewa na mama ya kumsulubu Mbowe
 
Popularity ya Kingai kwa sehemu kubwa imepaishwa na kesi ya Mbowe huo ndio ukweli, RPC wengi media ndio zimewapaisha.

Nawasilisha nikitokea
Kwa "PUT IN"
Sio kweli..Kingai yupo miaka mingi jeshini, Kesi ya juzi haina uhusiano na kupanda kwake.
Hapa kati yamepita mengi, ila wazuri na wabaya wapo.
 
Sirro alitumika sana wakati wa utawala wa kidhalimu wa Magufuli, sasa akale mali alizochuma kwa dhuluma.
 
Back
Top Bottom