Historia ya Nyuma inambeba IGP Wambura

Idofu

Senior Member
Oct 24, 2022
108
187
Katika Mabadiliko yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi,nadhani mpaka Sasa atakuja kulibadilisha Jeshi la Polisi kuliko Ma IGP waliomtangulia ukiachana na IGP Mstaafu Mwema,Mchango wa IGP Mwema utakuja kukumbukwa kwa vizazi vijavyo bahati mbaya Sana walimfuata walishindwa kuendelea na Mipango yake,kwa wakati huu amekuja IGP Wambura!!

IGP Wambura,tangu zamani sio mtu wa Media,Lakini Kazi zake ndani ya Jeshi ni ya Kutukuka,sio kwa Upande wa KiUpelelezi tu hata Kiutawala,wakati Jeshi likianza Program ya BRN wakati wa Utawala wa Rais JK,walianza na Mkoa wa Kinondoni kabla ya kwenda Mikoa mingine na wakati huo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni ndio huyu IGP wa sasa!!

Katika Kipindi chake,Mkoa wa Kinondoni ukipata mafanikio makubwa,ukiachana na Kupungua kwa matukio ya uhalifu ni Ujenzi wa MiundoMbinu ya Kisasa,Vituo vikubwa vilianza kujengwa kwa nguvu zake kwa wakishirikiana na Wadau mbalimbali,angalia Kituo Cha Polisi Mbweni,Kituo Cha Polisi-Gogoni Kiluvya,Kituo Cha Polisi- Madale,Jengo kubwa la Kubwa lenye vyumba 4 lililopo Kunduchi Karibu na Hotel ya Kunduchi beach,na mradi mkubwa ambao aliuacha ni Ujenzi wa Kituo Kikubwa Cha Mburahati ambao alikuja kuumalizia CP Suzan Kaganda ambaye alikuja kuja kuwa Kamanda wa Polisi Kinondoni baadaye kidogo baada ya Afande Wambura kuhamishwa.

Kwa hiyo,Kuteuliwa kwake kuwa IGP,Mheshimiwa Rais hajakosea hata kidogo,na angalieni anavyoanza kupanga safu yake,hana papara anaenda taratibu lakini ni kwa uangalifu Mkubwa,hata Uteuzi wa CP Kaganda nahisi itakuwa ni chaguo lake,mtu ambaye atamsaidia Sana hasa kwa Upande wa Rasimali ndani ya Jeshi,wale ambao walikuwa na tabia kununua vyeo na madaraka muda wao umefika mwisho,Kitu ambacho IGP na CP wa Utawala waliopita walishindwa kukidhibiti!!

Kwa Upande wa Vyeo vya Juu ndani ya Jeshi la Polisi, nadhani kumeshaanza kukaa sawa,kasoro Makamishna wawili nadhani hawataweza kwenda na Kasi ya sasa kwa muda umeshawatupa mkono,CP Sabas na CP Mkumbo,Kwa Upande wa Sabas ni mzuri amebobea Sana kwenye Upelelezi Ila kukaa kwenye fedha hapawezi na hatapaweza, CP Mkumbo kuwa Intel hapawezi panahitaji damu changa ili aweze kuendana na CP Awadhi ambaye naye damu changa!!, CP Awadhi Kamishna wa Operesheni ili aweze kufanikiwa vizuri anatakiwa alishwe vizuri na CP Mkumbo kutoka Intel!!, Kwani hizi Kamisheni zinategemeana (Kwa hali iliyopo sasa hawawezi kuwa Pamoja,kwani nakumbuka huko Nyuma wakati Awadhi akiwa na Cheo Cha ASP,Mkumbo alikuwa DCP na Sasa Wana rank sawa,Kuna Makovu katika Mioyo yao hususani Awadhi!!.

Kwa hiyo, Vetting ya IGP Wambura na CP Kaganda,ni Bora mno ambayo Mheshimiwa Rais ameifanya ndani ya Jeshi la Polisi!!
 
Unalisifu jeshi la polisi wakati wa JK?.

Enzi za giza kabisa.

Enzi upolaji kila siku unatangazwa , Kamanda kova kila siku anakamata siraha, sijui hata alikuwa anazitoa wapi?

Wakati ule ukishafika saa mbili usiku tu, uingie ndani. Panya road walikuwa wanazagaa mji mzima.

Wizi kwenye mabenki kila siku. tena mchana kweupe.

Majambazi kila kona ya nchi, ulikuwa huwezi safiri usiku mzima unaogopa kutekwa.

Embu acha kutukumbusha machungu wewe.
 
Ni Vizuri Sana,Silaha zinapokamatwa kuliko kutokamatwa!!,Unyanganyi wa Silaha unapotokea,ndio huwa linawastua watu wa Intelijensia na Wapelelezi kwa Kuna Silaha iko mikononi mwa watu ambao hawastahili kuwa nayo,kwa hiyo nguvu kubwa inatumika kuitafuta!!

Kipindi hicho Cha Kova,unachozungumzia,IGP Wambura alikuwa Incharge CID pale Buguruni na baada ya Buguruni akapandishwa na Kuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni akiwa Charles Kenyella.

Kwa hiyo,ukiona Kamanda wa Polisi anatangaza kuwa wamekamata Silaha,Ujue Kuna watu huku chini wanatimiza majukumu yao ipasavyo!!
 
Kama Wambura ni mweledi na muadilifu basi awakamate waliomshambulia Tundu Lissu.

Haiwezekani watu wameondoa walinzi wa eneo husika halafu jeshi la Polisi lishindwe kuwakamata kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
 
Ni Vizuri Sana,Silaha zinapokamatwa kuliko kutokamatwa!!,Unyanganyi wa Silaha unapotokea,ndio huwa linawastua watu wa Intelijensia na Wapelelezi kwa Kuna Silaha iko mikononi mwa watu ambao hawastahili kuwa nayo,kwa hiyo nguvu kubwa inatumika kuitafuta!!

Kipindi hicho Cha Kova,unachozungumzia,IGP Wambura alikuwa Incharge CID pale Buguruni na baada ya Buguruni akapandishwa na Kuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni akiwa Charles Kenyella.

Kwa hiyo,ukiona Kamanda wa Polisi anatangaza kuwa wamekamata Silaha,Ujue Kuna watu huku chini wanatimiza majukumu yao ipasavyo!!
Issue ni kudhibiti sio kukamata.

Unaacha hadi ziue au zifanye ujambazi ndio ukamate . huo ni upuuzi.
 
Issue ni kudhibiti sio kukamata.

Unaacha hadi ziue au zifanye ujambazi ndio ukamate . huo ni upuuzi.
Kumkamata na kudhibiti ni mafaniko!!

Usifikiri huu utulivu umekuja wenyewe!! hapana,Kuna watu wamefanya Kazi kwa siku za nyuma!!
 
Unalisifu jeshi la polisi wakati wa JK?.

Enzi za giza kabisa.

Enzi upolaji kila siku unatangazwa , Kamanda kova kila siku anakamata siraha, sijui hata alikuwa anazitoa wapi?

Wakati ule ukishafika saa mbili usiku tu, uingie ndani. Panya road walikuwa wanazagaa mji mzima.

Wizi kwenye mabenki kila siku. tena mchana kweupe.

Majambazi kila kona ya nchi, ulikuwa huwezi safiri usiku mzima unaogopa kutekwa.

Embu acha kutukumbusha machungu wewe.
huyo naye ni wale wale na ni wenzio.unawezaje kufuatilia utendaji kazi wa makamanda wa polisi tena kwa majina kama wewe si mwenzao!
 
Kuna haja ya kufumua hili jeshi kimawazo ili liwe na mtizamo wa kihuduma kwa wananchi. Jeshi letu lina shida ya utesaji, pia kutumia nguvu bila sababu kwenye kudhibiti mikusanyiko hasa pale wanapo ingiza siasa. Ukichunguza utaona tatizo kuu ni uchamadola wa ccm ambao unapelekea chama kutumia jeshi ili kibaki madarakani. Matokeo yake ni jeshi kuwanyanyasa wapinzani na kuwafanyia mambo mabaya.
 
Back
Top Bottom