Kamishna Camillus Wambura ateuliwa kuwa IGP Mpya. Sirro apewa Ubalozi Zimbabwe, Kingai ateuliwa kuwa DCI

Mzalendo39

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
882
1,029
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi.

Aliyekuwa IGP Simon Sirro ateulikuwa kuwa balozi nchi Zimbambwe.

Wakati huo huo amefanya mabadiliko ya Makamanda wengine kama inavyoonesha hapa chini


20220720_024629.jpg
Screenshot_20220720-022726_Instagram.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

Amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Amempangia kituo Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Amemteua Dkt. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi. Dkt. Suleiman ni Afisa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Julai, 2022 na uapisho utafanyika leo tarehe 20 Julai, 2022 saa 05:00 Asubuhi Ikulu, Chamwino Dodoma.

Wakati huo huo, Mhe. Rais amewateua wafuatao kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jeshi la Polisi: -

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Liberati Sabas Materu kuwa Kamishna wa Fedha na Logistiki. Anachukua nafasi ya (CP) Hamad Khamis Hamad.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji.

Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Awadhi Juma Haji kuwa Mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu;

Amempandisha Cheo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Faustine Constantine Shilogile kuwa Kamishna wa Polisi Jamii. Anachukua nafasi ya CP Mussa Ali Mussa ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Amempandisha Cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

PIA, SOMA: Rais Samia, asema kuna mabadiliko makubwa zaidi yanafuata, ameanza na Jeshi la Polisi
 
Kesho itakuwa or not kesho, sorry i mean leo asubuhi-mchana na siku nzima itakuwa sherehe kwa wale waliokuwa wakiombea hilo libwana mukubwa sirro lihamishwe vitengo kama sio kutolewa nyazifa, kumbe ni usiku na ishapia saa6 ni siku mpya.

Ngoja waje wazee wa hashtag za nanilii mpya
 
Back
Top Bottom