Kamati za Siasa za CCM Mkoa na wilaya nchi nzima, kama njia ya kupinga ubadhirifu, washughulikie taasisi na watumishi waliotajwa na CAG

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,662
CCM ndio wenye serikali, ilani ya CCM haikubaliani na matendo ya ubadhirifu. Ni wakati Sasa chama kijibainishe kwamba hao wabadhirifu wanawajibika binafsi, na chama hakikuwatuma, tena karibu wote, si wanachama wa CCM kwa mujibu wa ajira zao.

Kuanzia ngazi ya wilaya, hawa wabadhirifu tuwaandame, mpaka waondolewe katika halmashauri zetu, hiyo ndio njia pekee ya CCM kujipambanua kwamba hata yenyewe haikuwatuma hao wezi.

Naona chama fulani kinajaribu kuaminisha umma kwamba CCM ilituma mtu afanye matumizi ya fedha ya umma bila risiti, hapana. CCM iliwaagiza na kuwaapisha wafuate sheria.

Hizo fedha hazikuibiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa au wilaya au Katibu Mkuu wa CCM taifa. CCM ijipambanue kwamba si sehemu ya uchafu huo badala ya kuwaacha wapinzani wakiaminisha umma kwamba CCM ndio inahusika. Wapinzani walisema, na sisi tuseme, na sio kusema tu, na hatua tuzichukue huku tukisema.

Kuanzia ngazi ya Kata, CCM wakae vikao waidadavue ripoti kwa ngazi yao imewagusaje, waende ngazi ya wilaya, Mkoa, yale ya taifa tunamuachia SSH.

Baada ya Kata zote kufanya vikao, na maazimio kupitishwa, CCM wilaya waitishe mikutano wilaya nzima, baadae Mkoa, ili kuzidi kuweka kibano, na kuwaeleza wananchi chama kimedhamiria nini na msimamo wake ukoje.

Katika mlengo ule ule wa ushirikiano wa vyama, CCM na vyama vingine vyote tunapinga ubadhirifu.
 
Yanaweza kuwa mawazo mazuri ila siyo sasa au kwa chama hiki.
 
Hizo kamati za Siasa ili sikutane zinahitaji bajeti na wanaolipia hiyo mikutano ndo hao hao wa kujadiliwa kwa ubadhirifu.

Hebu kuwa serious kidogo
 
Tafadhali omba elimu kuhusu uhusiano wa kiwajibu na kikazi kati ya chama tawala na serikali iliyoko madarakani.
 
Chama kinasimamia serikali, lazima kichukie hatua
NIko pale natumia pain killer nasubiria hatua stahiki zichukuliwe. Usitake nambia mtu kubadilishiwa nafasi au kuhamishwa kituo cha kazi ndo hatua
 
Back
Top Bottom