Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Imeendelea Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya ya Itilima

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu chini ya Mwenyekiti wake Ndg Shemsa Seif Mohammed leo tarehe 24/11/2023 imeendelea na ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 ndani ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Itilima​

Jumla ya Miradi 5 yenye thamani ya Mil 700 iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekaguliwa.

Miradi hiyo ni pamoja na;
1. Ununuzi wa Vifaa Tiba Hospitali ya Wilaya (Nguno), Vituo vya Afya na Zahanati uliogharimu Tsh 300,000,000/-

2. Mradi wa kuongeza laini za kusambaza Umeme Kijiji Cha Habiya kata ya Bumela uliogharimu Tsh 76,256,847.80/-

3. Mradi wa kutafiti Maji chini ya Ardhi na kuchimba Visima Vinne Mwaswale vilivyogharimu Tsh 100,000,000/-

4. Mradi wa Matengenezo Barabara ya Lagangabilili-Migato iliyogharimu Tsh 58,000,000/-

5. Kukabidhi Ambulance Kituo Cha Mwanhunda

6. Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 2 na Matundu ya Vyoo 7 vya Shule Mpya ya Sekondari Mwanunui iliyogharimu Tsh 71,280,133/-

Pia, Kamati ya Siasa ya Mkoa ilizungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kijiji Cha Nkololo kata ya Mwamapalala ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe Njalu Daud Silanga kwa ajili ya kuongea na Wananchi.

Kamati ya Siasa ya Mkoa Simiyu imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na Utekelezaji wa Miradi hiyo iliyoikagua ndani ya Wilaya ya Itilima na kumpongea Mhe Njalu Daud Silanga (Mbunge Jimbo la Itilima) kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia Wananchi wa Jimbo lake.

Lumen Mathias Ngunda
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Simiyu.

WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.02(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.21.59(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.05.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.10.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.09.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.11.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.15(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.13(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-24 at 22.22.00(1).jpeg
 
Back
Top Bottom