Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu Imeendelea Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya ya Bariadi, Halmashauri ya Bariadi DC

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu chini ya Mwenyekiti wake Ndg Shemsa Seif Mohammed leo tarehe 25/11/2023 imeendelea na ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 ndani ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Bariadi, Halmashauri ya Bariadi DC​

Katika Halmashauri ya Bariadi DC Jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya zaidi ya bilion 5 iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekaguliwa.
Miradi hiyo ni pamoja na;
1. Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati ya Mwamondi uliyogharimu Tsh 53,000,000/-

2. Ujenzi wa Darasa Shule ya Msingi Ikungulyabashashi uliogharimu Tsh 12,500,000/-

3. Ujenzi wa Mradi wa Maji Matongo uliogharimu Tsh 235,000,000/

4. Kuona Maendeleo ya Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa, Igegu utakaogharimu Tsh 3,000,000,000/-

5. Kuona Mradi wa Shule ya Msingi Mlimani Kijiji Cha Sengerema kata ya Dutwa uliogharimu Tsh 540,300,000/-

6. Kuona Mradi wa Maji Byuna uliogharimu Tsh 586,896,061/-

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu imetoa Ushauri na kuielekeza Serikali ya Mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahya Nawanda kukamilisha Miradi ya Maendeleo Kwa Wananchi kwa wakati.
Huku Kamati hiyo ikiwa imeridhishwa na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Lumen Mathias Ngunda
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Simiyu.

WhatsApp Image 2023-11-26 at 00.17.21.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-26 at 00.17.23.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-26 at 00.17.26(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-26 at 00.17.26(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-26 at 00.17.24(1).jpeg
 
Back
Top Bottom