Kamati ya Bunge itakayomuhoji Gwajima ijiandae kukutana na majibu yatakayowaacha wakiangaliana

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kwa msomaji wa Biblia au mtu yoyote aliesikia habari za Yesu, bila shaka atakuwa amesikia habari au visa vya Yesu kutoa majibu kwa wafuasi wake, majibu yaliyokuwa yakiwafanya watu kubaki wanashangaana kama sio kutawanyika au kubaki midomo wazi na wakati mwingine kujiona wajinga.

Rejea kisa cha mwanamke aliefumaniwa na watu kutaka kumpiga mawe, habari ya kaisali na ile ya wafuasi wake kumtafuta Yesu na majibu aliyowapo.Hayo yakiwa kwa uchache tu.

Kwa wasiofahamu habari za Yesu, kisa kimojawapo ni hiki hapa chini:

Yohane 8 | BHN Bibilia | YouVersion

Japo simkubali sana Askofu Gwajima, lakini naamini atawashangaza wajumbe wa hiyo kamati kwani ni wazi Gwajima hana kosa na zaidi Gwajima hayuko Bungeni kwasababu ana shida na hela ya ubunge.

I wish mahojiano yangekuwa live.

Hata hivyo, kwa majibu watayopewa, watahadithiana na tutayajua.

Tusubiri.
 
Gwajima anapinga msimamo wa serikali halali,ni UAMUZI wa serikali kuwa covid 19 ipo na watanzania wapate vaccine jab ila kwa HIARI yao,sasa wewe kutumia nyumba za ibada na kutamka kuwa waumini wako hawatachanja vaccine ni kupingana na government's of the day,na kama Mr.Gwajima hapendi chanjo hiyo ni haki yake pia alikua na haki ya kuipeleka serikali mahakamani kupinga hizi chanjo.

Nchi ina Rais mmoja na ndiye anayetoa directions nchi iende wapi,hukubaliani nayo nenda mahakamani.msimamo wangu binafsi watanzania wenzangu go out there and get a jab,pls do that mimi tayari nimepata jab.
 
Siamini kama anaweza kushindana na maamuzi ya chama chake na akashinda, atawekwa mtu kati hataamini kitachomkuta, hata jamaa yetu huku alikuwa anajiamini kweli, ila alivyotoka kwenye ile kamati hakutaka kuongea na yeyote, mipasho yake mwisho kanisani kwake, nje ya hapo ajipange haswa.
 
Wanamtuhumu kwa “kusema uongo”. Bahati mzuri anayetuhumu ndiye anayepaswa kuprove.

Kama ni kuhusu chanjo, Gwajima atawatwanga KO asubuhi mapema maana ile Kamati haina mtaalamu mwenye majibu. Wakijaribu kumuita mama Waluwalu na yule kilaza mwenzie Mollel ndio wataharibu zaidi
 
Tena ingependeza kama hayo mahojiano yangerushwa live kwenye vituo vya habari vyote nchi ili tujue yupi ni mkweli yupi ni mfata upepo.
Ila hawawezi maana inaweza kuwa ni zaidi ya mahojiano.
 
Gwajima anapinga msimamo wa serikali halali,ni UAMUZI wa serikali kuwa covid 19 ipo na watanzania wapate vaccine jab ila kwa HIARI yao,sasa wewe kutumia nyumba za ibada na kutamka kuwa waumini wako hawatachanja vaccine ni kupingana na government's of the day,na kama Mr.Gwajima hapendi chanjo hiyo ni haki yake pia alikua na haki ya kuipeleka serikali mahakamani kupinga hizi chanjo.Nchi ina Rais mmoja na ndiye anayetoa directions nchi iende wapi,hukubaliani nayo nenda mahakamani.msimamo wangu binafsi watanzania wenzangu go out there and get a jab,pls do that mimi tayari nimepata jab.
Baba Askofu Gwajima watamshugulikia vibaya sana,hawezi kushinda serikali yake mwenyewe.Vinginevyo kesho atangaze kujiuzuru uanachama wa CCM.Hiyo itampa fursa ya kutapika.
 
Kwa msomaji wa Biblia au mtu yoyote aliesikia habari za Yesu, bila shaka atakuwa amesikia habari au visa vya Yesu kutoa majibu kwa wafuasi wake, majibu yaliyokuwa yakiwafanya watu kubaki wanashangaana kama sio kutawanyika au kubaki midomo wazi na wakati mwingine kujiona wajinga.

Rejea kisa vya mwanamke aliefumaniwa na watu kutaka kumpiga mawe, habari ya kaisali na ile ya wafuasi wake kumtafuta Yesu na majibu aliyowapo.Hayo yakiwa kwa uchache tu.

Kwa wasiofahamu habari za Yesu, kisa kimojawapo ni hiki hapa chini:

Yohane 8 | BHN Bibilia | YouVersion

Japo simkubali sana Askofu Gwajima, lakini naamini atawashangaza wajumbe wa hiyo kamati kwani ni wazi Gwajima hana kosa na zaidi Gwajima hayuko Bungeni kwasababu ana shida na hela ya ubunge.

I wish mahojiano yangekuwa live.

Hata hivyo, kwa majibu watayopewa, watahadithiana na tutayajua.

Tusubiri.
Mburumundu hawawezi kuweka mahojiano live wakiogopa aibu itakayowakumba.
Pascal Mayalla, hivi jamaa.walikulipia nauli, malazi na usafiri ya kwenda kuhijiwa Dodoma na kukurudisha Dar?

Au walikwambia ukope dukani kwa Mangi watakurudishia mwaka ujao wa fedha?🥺
 
Hakuna wa kujibu hoja za Askofu Gwajima. Hata wakikesha na madesa bado ni ngumu kusimama na mtu anayesimamia anachoamini.

..Gwajima amesema ukichanjwa unakuwa na nguvu ya sumaku pale sindani ilipoingia. Hivi hakuna Mtanzania anayeweza kum-challenge?

..Pia amesema ukichanjwa pale sindani ilipoingia panaweza kuwasha balbu. Je, hakuna Mtanzania anayeweza kumjibu kwa ushahidi?

..Vilevile amewatuhumu viongozi kuwa wamehongwa ili wa-promote chanjo, na kwamba wamechanjwa chanjo "feki." Hilo nalo hakuna Mtanzania wa kumjibu?
 
Back
Top Bottom