Kumekucha: Michael wambura aujibu waraka wa kamati ya uchaguzi ya tff.

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,755
YAH: TAARIFA ILIYOTOLEWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA
UCHAGUZI WA TFF JUU YA TUHUMA MBALI MBALI DHIDI YANGU YA
6/3/2012


Nimepokea taarifa za shutuma mbali mbali dhidi yangu
zilizotolewa na Bw Lyatu kupitia kwenye magaazeti mbali kupitia
kwenye mitandao pamoja na taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Bw Lyato 6/3/2012.

Awali ya yote ningependa watanzania wafahamu kuwa Kamati
hiyo ya uchaguzi ya TFF haijawahi kuwa huru na haijawahi
kufanya maamuzi ya haki dhidi yangu hata mara moja,
silazimishi wafanye hivyo ila katika kufuatilia haki kuna siku
ukweli utajidhihiri, labda niwakumbushe, baada ya uchaguzi
2004 kuisha ambapo niligombea uraisi wa TFF na ndugu
L.Tenga ambapo tenga alishinda, baada ya hapo mambo mengi
juu yangu yalianza kujitokeza .


Mwaka 2005 iliamuriwa ufanyike uchunguzi wa mahesabu
(Auditing) tangu nilipoingia madarakani wakati huo FAT
2002,2003 na2004 kampuni iliyopewa kufanya ukaguzi huwo
ilitoa orodha ya watu na malipo mbalimbali ambayo
hayakuambatana na hati za malipo zilizoidhinishwa "List of Un
approved vouchers with no supporting Documents" ambazo
kimsingi ni kama Hoja za kiukaguzi "Audit Querries" lakini
haikuwa hivyo.

Tarehe 14/01/2006 TFF ilifanya mkutano wake mkuu wa
kawaida wa mwaka 2005, katika mkutano huo yaliwasilishwa
mahesabu ya fedha ambayo sio final Audited Accounts ambayo
yalilenga kunidhalilisha na kunishushia heshima mbele ya jamii,
wakati huo mimi nilikuwa mjumbe wa mkutano mkuu kupitia
Klabu Simba kama mwenyekiti nilihoji utaratibu huo, taarifa
hiyo ya fedha ilitolewa ndani ya ukumbi bila wahusika nikiwemo
mimi kupewa hoja zinazonihusu na muda wa kujibu hoja hizo,
Kwa kawaida mkutano mkuu hupelekewa Taarifa kamali ya
mahesabu iliyokaguliwa(Audited Accounts) baada ya kupata
majibu ya hoja za kiukaguzi kutoka kwa wanao husika jambo
ambalo halikufanyika kwenye hili.

Baada ya kulalamika miezi mitatu baadae Tarehe 21/4/2006
niliandikiwa Barua na TFF yenye kumbukumbu TFF/ACC.06/2
yenye kichwa cha habari "QUERIES ON PAYMENTS MADE TO
YOU" yaani hoja zinazohusiana na malipo yaliyofanya kwako,
aidha barua hii ilinitaka mimi nikiwa mmoja wa watu waliotajwa
kwenye orodha ya watu waliolipwa malipo mbali mbali ambayo
hayana viambatanisho hivyo kupewa siku 30 kutoa maelezo na
majibu stahilli ili kufanikisha ukaguzi Maalum (SPECIAL AUDIT)
katika maenoa matatu(3):
1. Kutathmini malipo ambayo hayakuidhinishwa yaliyofanywa
kwa viongozi wa FAT kamailivyo ainishwa kwenye
pendekezo 12.
2. Kuanisha uhalali wa madeni ya FAT mpaka 2004.
3. Kutathmini uhalali wa gharama za vifaa (Fixed Asset) zilizo
nunuliwa 2002-2004.
Tarehe 28/5/2006 niliandika maelezo na majibu yote ambayo
nilitakiwa kuyatolea maelezo, hoja zote zilizo letwa kwangu
zilijibiwa, sikupata maelezo mengine yoyote au maswali ya
kutaka ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu ukaguzi.


Baada ya taarifa ya ukaguzi maalum kutoka niliipata kwa njia
zangu na kuisoma nikagundua kuwa ukaguzi huo huenda
ulinilenga mimi maana watu wote waliotoajwa kwenye ukaguzi
wa awali hawakutajwa tena, taarifa haikusema kama majibu yao
yalitosheleza matakwa yao na haikutaja kama majibu yangu
hayakuwatosheleza na kukidhi mahitaji yao.
Katika Taarifa ya ukaguzi Maalumu (Special Audit) Kifugu 4.0 (a)
mkaguzi anasema viongozi wa FAT hawakuweza kupatikana
kutoa maelezo kuhusiana na hoja za kiukaguzi, hii inamaanisha
kuwa majibu ya hoja niliyoyawakilisha TFF tarehe 28/5/2006
hayakupelekwa kwa wakaguzi na kama mkaguzi alinihitaji basi
TFF ilimweleza sipatikani, ili report ionekane mimi ni mbadhilifu.
Kifungu 4.0(b) cha taarifa hiyo pia kinasema kazi ya
ukaguzi maalum imekuwa ngumu kwa kuwa viongozi wa FAT
hawajakabidhi ofisi hivyo nyaraka zinazohusiana na ukaguzi huo
kutokupatikana, hili ni jambo la kushangaza kwani nilkabidhi
ofisi siku mbili baada ya uchaguzi 29/12/2004 na wakati
ukaguzi huo unafanyika mwezi 7-8/2006 iliisha pita miaka 2
swali linakuja kazi za TFF zilikuwa zinafanyikaje? Mimi sikuwa
mhasibu wa TFF ambaye nina tunza nyaraka za malipo, mhasibu
wa TFF mpaka hivi sasa yupo walishindwa nini kumuuliza?
Ninachokiona mimi hizi zilikuwa ni njama zilizofanywa kuficha
nyaraka ili majibu yasipatikane ili nionekane mbadhilifu na
mwizi. Kifungu4.0(e) cha ukaguzi kinasema wamegundua
makosa mengi ya uandikaji wa kumbukumbu za mahesabu
katika vitabu vya FAT, hiyo inamaanisha kumbukumbu
walizopatiwa hazikuwa sahihi na hivyo zilipaswa kuwekwa sawa
kwanza ili ukaguzi ufanyike jambo ambalo lilikuwa gumu kwa
mkaguzi kwa kuwa nyaraka nyingi hazikuweza kupatikana
Mfano PV 5322 ya tarehe 22/6/2004 inaonyesha malipo $ 3250
kwa ajili ya posho za safari kwenda Ruanda halafu maombi ya
idhini ya malipo iliyoambatanishwa nayo inataja PV 5322 Mr
Wambura malipo ya PTA's for match kamisaa ya $350.
Ili nionekane mbadhilifu Nimegundua maombi mengi ya
uongo na kutunga ya idhini ya malipo yameandikwa kuonyesha
nilipokea malipo bila sahihi yangu ili mradi yaonekane
yalifanyika kwangu mfano 28/07/04 PV 5324.
Pamoja na Mkaguzi katika repoti zake nyingi tangu ya awali
kuitaka TFF iwasiliane na mimi ili majibu yapatikane TFF
haikuwahi kufanya hivyo kwa makusudi na kwa hila na nia
mbaya na mimi .


Mwaka 2008 niligombea nafasi ya Makamu wa pili wa rais
wa TFF katika mchakato huo jina langu liliondolewa katika
orodha ya wagombea, nilikata rufaa katika kamati ya Rufaa ya
TFF, katika moja ya hoja za TFF ni kwamba kuna hoja za
kiuhasibu ambazo sikuwa nimezijibu, hii ndio ilinionyesha ni
kwa jinsi gani majibu yangu yalifichwa na mkaguzi hakupewa,
kwani mjibu yale yalikuwa na nakala 3 na niliyakabidhi TFF
2006 iweje 2008 hawajayapata? , hivyo ikaamuliwa nipewe hizo
hoja nizijibu.


Tarehe 1/12/2008 TFF iliniandika barua nyingine yenye
Kumbukumbu TFF/ADM/AP.08/07 yenye kichwa cha habari
"YAH: HOJA ZA MAHESABU YA FAT (TFF)" iliyosainiwa na
Mtemi Ramadhani, katika barua hii tff ilinitaarfu kuwa kamati ya
Rufaa iliyoketi tarehe 5/12/2008 imenitaka nijibu hoja za
kiukaguzi kabla ya tarehe 10/12/2008 saa 6.00 mchana na ofisi
itakuwa wazi kushirikiana na mimi kupata nyaraka hizo ili
zijibiwe, Jitihada za kupata nyaraka kutoka TFF ziligonga mwaba
hakuna aliyekuwa tarayari kutoa ushirikiano, 7/12/2008
nilimwandikia katibu mkuu wa TFF nikimueleza juu ya
malalamiko yangu kutokupa ushirikiano kutoka katika ofisi
yake, na kuomba nipatiwe nyaraka muhimu kabala ya tarehe
8/12/2008 saa sita(6.00) mchana pamoja na nyaraka zifuatazo:
1.Nakala ya Ukaguzi maalum(Special Audit Report)
2.Vivuli vya Nyaraka mbali zikiwemo receipt na hoja za kiukaguzi
wa mahesabu.
Tarehe 8/12/2008 TFF kupitia barua yake
TFF/ADM/GC.08/105 ilinijibu ikinitaarifu kuwa ofisi yake
itanikabidhi nyaraka mbali mbali zinazonihusu niende nizifuate,
nilipozifuata kama barua katibu mkuu ilivyosema, sikupewa
ushirikiano wowote na niliyemkuta offisini nd Mtemi Ramadhani
alikataa kabisa kutoa ushirikano, niliiandukia TFF barua
nyingine kuelezea kukosa ushirikiano, tarehe 9/12/2008 siku
moja kabla ya deadline nilipigiwa simu niende kuchukua
nyaraka, nilipewa vivuli vya profoma invoice, Accounts ledger na
barua moja ya kutoka kwa Marehemu Charles Masanja.
Tarehe 10.12.2008 kampuni ya Uhasibu na Ukaguzi ya E.K
Mengesho & Company ilitarifu TFF kwa niamba yangu
wakabidhiwe vielelezo na hoja hizo za kiukaguzi, kampuni hiyo
kupitia barua yake Kumb MACO/AQR-MRW/12/08 iliitaka tff
iwakabidhi nyaraka zifuatazo ili zijibiewe:
1. Copy of complet the complete Special Audit Report
2. Copy of all relevant documents touching Mr Wambura
namely


2.1 Payment vouchers,
2.2 Invoices
2.3 Receipts
2.4 Personal Ledger
2.5 Journal Vouchers
Barua hiyo haikujibiwa hadi hii leo, aidha nilichukua jitihada za
ziada kuwasiliana na wanasheria wa kampuni ya Uwakili MSK
LAW PARTNERS(ADVOCATES) nao waliwaandika TFF barua
yenye kumbukumbu MSK/TFF/08/01 yenye kichwa cha habari
MICHAEL. R. WAMBURA –Audit Queries kuwasisitiza TFF
iliwaweze kunikabidhi nyaraka hizo bila mafanikio, hata hivyo
barua zote mbili hazikujibiwa hadi hii leo.


Pamoja na vikwazo vingi vya kupata nyaraka kutoka TFF
nilioomba kamati ya rufaa ikubali kupokea majibu ya hoja za
kiuhasibu niliyoyatoa mwaka 2006 ili yaweze kuongoza kikao,
aidha kamati hiyo ilikubali na kupitia hoja mbalimbali na
kuridhika kuwa sikuwa na hatia ya ubadhilifu kama pingamizi
lilivyowasilishwa, aidha sababu ya kuondoa jina langu ni
waswasi na suala la Uadilifu (Intergrity) wa kuwa kampuni MIN
INVESTMENT PROMOTION CO iliyofanya biashara na TFF
ilikuwa inamilikiwa na Mimi Michael Wambura, ukweli ni
kwamba kampuni hii inamilikiwa nd Josea Samuel kama
inavyoonyesha katika Extract From Register No 93017 ya Msajili
wa Makampuni, Mnamo tarehe 10/12/2008 Bw Josea aliiandika
TFF barua akiambatanisha na vivuli vya Cheti cha Usajili
akiitarifu TFF kuwa yeye ndie mmiliki halali wa Kampuni hiyo na
ni yeye ndiye aliefanya biashara na TFF na kama kuna maelezo
ya ziada yuko tayari kufiki pindi wakimhitaji, Kwa kuwa TFF
walikuwa na agenda ya Siri juu yangu waliamua kuificha kamati
ya rufaa juu ya taarifa(barua)hiyo na hatimaye kamati ya rufaa
kuondoa jina langu kwenye uchaguzi huo kwa sababu ambazo
sio za kiubadhilifu.


Katika kuhakikisha majibu yanapatikana na kuweka wazi
juu ya suala hili, na kama TFF inanituhumu kwa ubadhilifu ni
kwanini nitumie nguvu zote hizo kupata nyaraka ili nipate kujibu
hoja zao? Kulikuwa na sababu gani niwaandikie TFF barua 3 na
nyingine kutoka kwenye makampuni ya ukaguzi na hata kutoka
kwa wnasheria nabado walishindwa kunikabidhi hizo nyaraka
hizo hata kujibu barua?
Ununuzi wa Samani za Hostel
Mwaka 1998 Fifa kupitia mradi wa FIFA Goal project iliipitisha
Tanzania kuwa moja ya nchi wanachama wa Fifa ambao
wangepatiwa mradi wa mendeleo katika awamu ya kwanza,
Msimamizi Mshauri(consultant) MD Consultancy-architect
aliteuliwa kusimamia mradi huu, mpaka 29/12/2001 uongozi
mpya unaingia madarakani ujenzi mradi huu uliukuwa
haujaanza kutekelezwa, aidha sababu zilizoleteleza
ucheleweshaji pamaoja na nyingine ilikuwa,
1. Kuwasilishwa kwa mapendekezo ya kubadili mchoro
uliokuwa tayari umeidhinishwa na fifa kutoka Hostel ili
ujengwe uwanja wa mpira (Stadium)
2. Kuchelewa kupatikana kwa vibali pamoja na hati mbali
mbali zinazoonyesha manispaa husika iliridhia ujenzi
huo,
3. Kujua mmiliki halali wa karume Staduim
4. Makandarasi kuandika maakadirio ya ujenzi kwa
kutumia TSHs badala ya UDS($)
Mwaka 2002 tulianza kusimamia ili kuhakikisha mradi huo
unaaza kwani baadhi ya nchi zilikuwa zimeisha kamilisha
awamu ya kwanza na kuanza kuitumia.
Wakati mradi huo unaidhinishwa na FIFa, viwango vya
kubadilisha fedha (Exchange Rate) itakuwa ni sh 436 kwa dola
mpaka mradi utakapo kamilika ili kuondoa uwezekano wa mradi
kushindwa kuendelea.


Mwaka 2004 wakati mradi unakaribia kufika tamati ilioneka
kuwa gharama za mradi ziliongezeka na FAT haikuwa na uwezo
wa kulipia, tarehe 7/7/2004, Fifa ilihamisha kiasi cha Dola
$71,590.00 kutoka kwenye Accounti yetu ya FAP(Financial
Assistance Programme) na kuifanya akaunti hiyo kubaki salio
sufuri, uamuzi kama huo ulifanywa na fifa na mwanachama
alikuwa anataarifiwa kwa kuwa malipo yalifanywa na wao moja
kwa moja.
June 2004 mradi ulikuwa umefikia hatua za mwisho kukamilika
lakini katika BOQ(bills of Quantity) haikujumlisha Vifaa vya
Hostel Pamoja na ukuta wa kuzunguka eneo lote la karume,na
kwa kuwa jambo hilo halikuwemo kwenye mradi mshauri ujenzi
alishauri zitafutwe hela kwa kuwa mradi huo ni mwingine tofauti
na wa awali.
Msimamizi wa Maendeleo wa kanda yetu nd Ashford Mamelodi
alipokuja alikuta na kusema haiwezekani mradi ukazinduliwa
katika hali hiyo,hivyo aliagiza yatafutwe makampuni yanayoweza
kufanya kazi na yeye atashawishi fifa igharamie kazi hizi
1. Kujenga uzio(ukuta)
2. Kusupply furnitures za hostel


Makampuni mengi yalikuwa hayapendi kufanya kazi na FAT/TFF
kwa kuzingatia rekodi zake za fedha na ulipaji wake wa madeni,
Makampuni machache yaliweza kukubali kufanya biashara na
FAT tena kwa gharama kubwa kufidia muda na hasara
nyinginezo ambazo wangeweza kukutana nazo ,makampuni
kadhaa na yalileta Makisio ya gharama zao.Tulizipeleka FIFA,
Nd Mamelodi alipokuja alikutana na wawakilishi wa makampuni
hayo na alikubali kuwa atawalipa moja kwa moja. Mjenzi wa
ukuta alilipwa moja kwa moja baada ya kumaliza kazi na
kuikagua Malipo ya zabuni ya vifaa vya hostel yaliletwa FAT kwa kuwa
sehemu ya fedha tulizoomba zingetusaidia kuiweka kambini na
kuisafirisha Serengeti Boys na twiga Stars kwenda Zimbabwe na
Kigali. Lilikuja wazo la kununua Basi ili leweze kusaidia timu
zetu za Serengeti na Twiga kusafiri mara kwa mara kwa kuwa
basi lilokuwepo la FAT lilikamatwa na kupigwa mnada kutokana
na madeni ya FAT ya mwaka 2000-2001, hivyo tulikubaliana
katika $ 25,000/ zilizokuwa zimekuja tutoe Usd 10,000.00 ili
kufanya malipo ya awali ya kununua Basi, kwa kuwa Fedha hizo
zinatoka FIFA ilikuwa lazima Mwenyekiti wa FAT aidhinishe
kwanza ndio hatua nyingine ifanyike kama inavyoonekana
kwenye PV 5324 ya tarehe 29/7/2004 na barua ya mwenyekiti
kwa wakaguzi, mpango wa kununua basi ulishindikana kwa
kuwa FIFA iliagiza mzabuni alipwe pasipo maelezo mengine hivyo
salio lililobaki la USd 8,400.00 lisingeweza kununua basi hivyo
zilihamishiwa kwenye matumizi ya maandalizi ya timu ya
Serengeti Boys kwenda Ruanda kwa basi la kukodi na posho na
Twiga stars kucheza na Zimbabwe ikiwa ni usafiri na posho zao,
kumbukumbu za malipo na matumiz yako kwa mhasibu.
Kwa mujibu wa katiba ya FAT ibara 42(3) (e)&(k) katibu
mkuu ndiye Afisa mhasibuwa chama (Accounting Officer) na
atabuni njia mbalimbali za kuongeza mapato ya FAT hivyo
mamlaka yalikuwa yaniniruhusu kufanya na kuhamisha
mafungu ya fedha(Realocation of Funds) kutoka katika kifungu
cha matumizi ya kununua basi na kupeleka katika matumizi ya
timu za Taifa.


Tuhuma zote alizozitoa Nd Lyato kuhusu ubadhilifu zilitolewa
pia, lakini kamati ya rufaa chini ya JAJI Mkwawa ili iliona sikua
na hatia nazo na ushahidi wake unaweza kupatikana katika
kumbukumbu za majadiliano (Proccedings),pamaoja na maamuzi
yaliyotolewa hayakuwahi kunitaja mimi kuwa mbadhilifu au
mwizi , hata kamati ya Uchaguzi chini ya Ng Lyato katika chaguzi
2 ambazo ni za Simba na Mara (FAM) katika barua zake
haikuwahi kutaja kuwa jina langu linaondolewa kutokana na
Ubadhilifu jambo linaloonyesha kuwa maneno aliyo yasema
Lyato kwa waandishi wa habari ni yake binafsi na sio ya Kamati
ya Uchaguzi ya TFF.


Ninapenda kumfahamisha bwana Lyatu Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inasema " mtu hawi na hatia mpaka
atakapo tiwa hatiani na Mahakama" hivyo kuendelea kunizuia
kugombea kwa mambo ya kufikirika na ya kizushi ni kinyume na
sheria jambo ambalo huenda likahitaji mkono wa mahakama
kutafsiri. Bwana lyatu alijua mimi ni mbadhilifu ni vipi nilipogombea
uongozi wa FAM(Mara) alisahau kutumia kigezo hicho kwani
sababu pekee iliyotolewa na kamati yake ilikuwaa ni mimi
kuipeleka Simba Mahakamani, lakini hata kama ni kosa adhabu
yake ni nini na imetajwa kwenye kifungu kipi cha kanuni na
Katiba ya TFF? Ni wazi bwana lyatu amejazwa jazba na upepo
hata kutumia maneno ambayo kwa mtu anayefikiri kwa kutumia
ubongo asingeweza kuyaandika ni wazi bwana Lyatu ameingia
kwenye siasa za Uchaguzi wa TFF 2012,hivi sasa imegundulika
kuna binadamu wawili (ufaransa na Uingereza) wamezaliwa na
wanaishi bila ya kuwa na ubongo.
Napenda kumhakikishia bana Lyatu umri wa kugombea uongozi
TFF ni miaka 18 ambayo mimi niliisha ipita na hata kama
ningechaguliwa leo ukomo wa uongozi wa TFF ni miaka 70 kwa
mantiki hiyo sina sababu ya kudanganya umri,mimi nimezaliwa
hospitali hivyo nina cheti cha kuzaliwa, nina passport, kadi ya
kupigia kura nimesoma shule kuanzia Msingi, sekondari na
Chuo kikuu DSM(UDSM) ambapo kumbukumbu zangu zote za
kuzaliwa zinapatikana, kwa kuwa nakala za form hizo sijaziona
siwezi kukubali au kukataa tofauti iliyojitokeza na kama ipo
itakuwa ni kosa la bahati mbaya amboyo sikuidhamiria lakini pia
nitapenda nione nakala halisi, mtu anayedanganya umri ni Yule
ambae atakaefaidika kwa kufanya udanganyifu huo, iwapo sifa
za kikatiba ni miaka 18 na mimi sina nikajaza hivyo hiyo itakuwa
udanganyifu lakini kama nimeipita na nikaandika tofauti na
bado ninakidhi matakwa ya kikatiba hapo nitakuwa
sikudanganya umri bali nimekosea kujaza umri wangu mtu
anayedanganya kama ambavyo nilikuandikia kuwa Katika wilaya
za Temeke Kinondoni na Ilala kuna viongozi waliochaguliwa
hawana elimu ya kidato cha Nne kama kanununi za TFF
unazodai anazisimamia zinavyosema na huku akiendelea kuwa
bubu na kiziwi huku sauti na masikio kufunguka suala
linapokuwa linapomuhusu Wambura, Kwa kuwa hakuwa na nia
njema na mimi, hata kanuni ndogo ya haki za binadamu ya haki
ya mtu kusikilizwa(right to be heard) aliipuuza, kwani
angeniuliza kuhusu utata huo angepata hasara gani? au
angalichelewa kuongea na waandishi? .


Napenda kumkumbusha Lyato niliwahi kusema hawezi na hata
kaa hata siku moja kunitendea haki, kwa mantiki hiyo
nisingeweza kudanganya umri , ninachopenda ieleleweke ni
vizuri kazi za watu zikabaki ofisini na mambo ya kijamii na
kibinafsi (social and personal issues) zikabaki mitaani kwani
unaweza kumfikira mtu na kumhukumu mtu kwa asilo litenda,
kila wakati haki si tu itendeke lakini ionekana kutendeka
"justice must not only be done must seen to be done'' lazima
maamuzi yafanyike posipokutilia chembe ya shaka.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF bila kuheshimu kamati ya
Rufaa ya TFF imeanza kuandikia mikoa wanachama wa TFF
kupinga maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya TFF yote hani kisa
maamuzi yale yalimsaidia Wambura na kwa kuwa mwaka huu
kuna uchaguzi mkuu wa TFF, aidha kamati hiyo imeamua
kunyakua madaraka ya kuwa msemaji wa TFF bila kujali athari
za kisheria zinazoweza kuikumba tff kutokana matamshi na
maamuzi ya kamati hii, ni wazi kamati hii inanyakua mamlaka
ya kikatiba ya usemaji ya Rais na Katibu wa TFF.


Humu duniani kuna aina nyingi za walevi wengine pombe
wengine madaraka na wengine huwa mbumbumbu wa sheria na
mambo mengine lakini hawataki waelimishiwe, Mwl Nyerere
alisema ni bora ukawa mjinga kulikoni mpumbavu maana
mjinga anafundishika, hivi upeo wa bwana Lyatu kuelewa kuwa
Kamati ya Rufaa ni supreme Organ(ni chombo cha cheye
mamlaka ya juu) ndani ya TFF umeishia hapo? Ni kweli
wafanyakazi wanatakiwa kupelekwa kozi mara kwa mara lakini
kwa TFF kumpeleka Lyato kwenye hili itakuwa Ufisadi, hivi lyatu
na kamati yake wanajua na kufahamu Sheria kulikoni Prof
Mgongo Fimbo? Wanaufahamu wa masuala ya utawala wa
michezo kuliko KIPINGU, TANDAU, Mhe MISANGA na Kamanda
RWAMBOW,? Nikisema huu ni ulevi sitakuwa nimekosea,
ninachomshauri Nd Lyatu awaombe radhi watu hawa na ajiuzulu
kwani yeye amekuwa mzigo mkubwa na kusababisha majeraha
na madonda makubwa katika mpira wa Tanzania, kwani TFF na
wadau wote hawazungumzii tena mpira bali uchaguzi za TFF.
Kuhusu swala la kwenda CAS napenda nimkumbushe
bwana Lyato kwa kuwa yeye ni mbumbumbu wa sheria (ignorant
in Law) maamuzi yakiisha fanywa na chombo cha juu yanakuwa
Binding to the parties(yanafunga pande zote) ila yule ambaye
anadhani hakuridhishwa nayo ndie anayepaswa kukata rufaa
kwa chombo cha juu zaidi, maamuzi ya Kamati ya rufaa
yalikuwa upande wangu(in my Favour) hivyo siwezi kukata rufaa
CAS ila kwa kuwa wewe hukuridhika namshauri uende huko ili
upate haki unayoitafuta na kwa kuwa hakuna chombo cha juu
kilichotoa uamuzi tofauti, maamuzi yanabakia valid mpaka hapo
yatakapo tenguliwa, ni jambo la ajabu uamuzi uliotenguliwa ni
wa kamati yake halafu anatangaza kutokutambua, njia nzuri ya
kupinga maamuzi ni kukata rufaa sio kutotambua na kuifanya
kamati ya rufaa kichekesho kwa kuandika barua mikoani
nakuikashifu.


Kwa mujibu wa mtiririko wa vyombo vya haki katika katiba
ya TFF inaanza Kamati ya Nidhamu,kamati ya Rufaa na
Mahakama ya usuluhishi ya Michezo, Kanuni zinaundwa ili
kurahisisha utekelezaji wa katiba hivyo kanuni haiwezi kuipinga
katiba, Katiba ya TFF inasema Maamuzi ya kamati ya Rufaa ni
ya mwisho na hayatajadiliwa na chombo kingine chochote
isipokuwa CAS, wakati mamlaka ya kamati ya uchaguzi kuwa
mwisho sio ya kikatiba ni ya kikanuni ambayo yanatungwa na
Kamati ya utendaji ya TFF ila katiba inatungwa na kupitishwa na
mkutano mkuu hivyo kwa Bw lyato kuipinga maamuzi kamati ya
rufaa hii inaonyesha ni jinsi gani mawazo yake yamekosa nuru
na yamefubaa kutokana na upofu wa fikra sababu tu ya
kujaribu kulinda maslahi yake na ya wenzake ili kiongozi
wanayemtaka aweze kuchaguliwa ili waendelee kuwa na nafasi
ya kulivuruga soka la Tanzania.


Bwana lyatu alikuwa mwenyekiti kamati ya kuchunguza
mazingira na sababu zilizopelekea Serengeti Boys 2005
kuondolewa mashindanoni kama alijua kuna CAS na Tanzania
ilikuwa na uewzo wa kushinda rufaa kama walivyo kata CAF ni
kwanini aliacha nafasi ya Tanzania ikapotea bure na Tanzania
kifungiwa miaka 2, ili hali anajua pahali kwa kukatia rufaa ?
hiyo ilitosha yeye na kundi lake kujiondoa TFF kwani kwa
Tanzania kufungiwa mashindano ya U17 kumeliumiza sana soka
la Tanzania.


Haikuwa nia yangu kutoa maelezo yote haya ila nadhani wakati
mwingine mototo akipaliwa ukimgonga ngongoni maisha
yanaanza upya kwa gharama nafuu, hivyo nimesema haya labda
bwana Lyatu na kundi lake watapata ufahamu bila TFF kutumia
fedha kwa ajili ya semina, ninapenda kusisitiza ni "kheri kuwa
mjinga kuliko mpumbavu"(Nyerere J.K).
Ninapenda kusisitiza kwakuwa tuhuma za bwana Lyatu
zinazotokana na hoja za kiuhasibu(Audit Queries) ambazo zote
ni za uongo zenye nia ya kunifanya nipoteze hadhi mbele ya jamii
aidha napenda kumhakikishia Nd lyato hili halitaniziba mdomo
tutaendelea hadi wababaishaji mtakapo rudi mlipotoka, aidha
ninapenda kumhakikishia bw lyatu katika uchaguzi 2012
utakapotangazwa nitachukua form na kugombea katika nafasi
nitakayo iona ni mwafaka kwangu bila kujali hila ghilba na fitna
anazoniwekea, aidha kama yeye anavyodai ni muadilifu ni vizuri
kutumia fursa hii aliyopendelewa kushughulikia Suala la wilaya
za DSM kwani kuna fununu kuwa amepewa au amepokea
zawadi/ahadi ili suala hili lipite katika mazingira ya upendeleo
kwani baadhi ya viongozi wa TFF ni maswahiba na ni washiriki
wa kambi moja ya uchaguzi ya TFF.


Ninamtaka bwana lyato awaombe msamaha watu wa Mara
kwa udhalimu wa kuingilia mchakato wa uchaguzi huku
akishindwa kuweka wazi mgongano wa kimaslahi na baadhi ya
wagombe jambo linalopelekea kutilia shaka uadilifu wake.
Ninapenda pia kuwapongeza wana CCM wenzangu wa jimbo la
ukerewe walioona ndugu lyato hafai kuwa mbunge wao kwa
kumyima kura 2010 , kwani kuwanyima kura watu wenye uwezo
kama balozi Kamanda, Mhe Mongela, na kumchagua kiongozi
kama lyatu ingekuwa ni hasara ambayo wana ukerewe na taifa
kwa ujumla tungejutia kwa muda mrefu kama kwenye mpira
tunavyojuta.


Mwaka 2008 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa TFF
ambapo tangia mwaka 2007 maandalizi ya wagombea yalianza
mimi ni likuwa ni mmoja wa watu waliotangaza azma yangu ya
kugombea tena katika uchaguzi mkuu wa TFF. Mwaka huo huo
2007 nilioonyesha nia ya kugombea tarehe 21/12/2007 TFF
ilifungua jarada la malalamiko kumb CD/IR/5110/2007 kwa
Jeshi la Polisi kuwa kati ya 2002-2004 kulitokea ubadhilifu
katika ofisi za FAT na mimi Michael Wambura nikiwa mtumishi
wa FAT/TFF, Uchunguzi na upelelezi ulifanyika pamoja na
kukusanya vielelezo na maelezo ya mashahidi mbali mbali na
jeshi la polisi , hatimae jalada lilipelekwa kwa Mwanasheria
mkuu wa serekali mwenye mamlaka ya kupitia na kusoma
kuona kama kuna kesi ya kujibu dhidi ya mtuhumiwa .
Tarehe 26/10/2011 jeshi la polisi kupitia barua kumbu
DSM/ILAL/CD/B.I/I/VOL.XI/50 iliyosainiwa na Mkuu wa
upelelezi makosa ya jinai Mkoa wa Ilala nd D. Nyanda-SSP
ikiwataarifu TFF juu ya matokeo ya uchunguzi wao na maelekezo
ya mwanasheria mkuu wa serekali ya barua kumb
J/DSM/ILA/113/11 ya tarehe 1/4/2011 kama ifuatavyo
"Baada ya mwanasheria wa serekali kulisoma jalada hili
aliridhika kuwa mtuhumiwa MICHAEL WAMBURA hakuwa
na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma hizo, Barua ya
mwanasheria wa serikali Yenye kumbukumbu
J/DSM/ILA/113/11 ya tarehe 1/4/2011 yahusika, Kwa
barua hii jalada la kesi limefungwa"


Kwa kuzingatia mlolongo mzima na mchakato mzima wa ukaguzi
wa mahesabu ya TFF pamaoja na vikwazo vingi mbali mbali
kutoka TFF tangu 2005 hadi 2012(miaka 8) ambavyo kimsingi
vililenga kunichafua na kuniharibia jina ili nisiweze kugombea
uongozi na hatimae kuonekana mhalifu mbele ya jamii ni wazi
vilifanywa kwa malengo Fulani ya watu Fulani kwa hila.
Matokeo ya kamati ya Rufaa ya TFF mwaka 2008 hayakuniona
mie mbadhilifu au mwizi, matokeo ya uchunguzi wa polisi na
maelekezo ya mwanasheria mkuu wa Serekali yanatoa picha
kamili ya Usafi wangu katika utendaji ambao kundi Fulani kwa
maslahi yao wanajaribu kunifanya nionekane sifai, swali
ninalojiuliza ilikuaje wakapeleka malalamiko polisi ya ubadilifu
mwezi wa Dec 2007 na mimi kupewe hoja za kiuhasibu kujibu
Dec 2008? Mwaka mmoja baadae, ni wazi kesi hiyo ilifunguliwa
kwa hila na kwa manufaa ya watu Fulani.
nipenda watu wafahamu wakati mwingine haki haipatikani kwa
urahisi ni lazima uipiganie sio tu kwa ajili yako ila pia kwa ajili
ya watu wengine wanao weza kudhulumiwa haki yao
Ninamtaka ndugu lyato nani ya Siku saba(7) aniombe radhi kwa
maneno aliyoyasema juu yangu kupitia utaratibu ule ule
alioutumia kunikashifu na kusema maneno ya Uongo kinyume
chahapo nitachukua hatua za kisheria juu yake, aidha
ninatafakari njia muafaka za kisheria zakufuata ili jambo hili
lifike mwisho.


Michael .R. Wambura,
Katibu Mkuu (mstaafu) FAT/TFF
28/3/2012
 
Huyu jamaaa aliuza Toyota MArk II yake kuvaa Tenga kwenye uchaguzi wa 2004...akapigwa chini ...sasa anatafuta njia ya kurudisha gari lake..
 
Back
Top Bottom