Wanaotajwa kumrithi Chongolo Ukatibu Mkuu CCM

Asphalt1961

Member
Jan 7, 2022
5
13
Wamo Mabalozi, Wastaafu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Vijana Chipukizi.

Kufuatia Katibu Mkuu Daniel Chongolo kuachia ngazi, wimbi la kupata Mrithi limezidi kuongezeka Mtaani huko Dar es Salaam.

Makada wanaotajwa kwa ukaribu kurithi mikoba hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Misri, Balozi Emmanuel Nchimbi; Mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Wazazi, Alhaji Abdalah Bulembo; Mbunge wa Isimani, William Lukuvi na Mwenezi Taifa, Paul Makonda

Aidha, Mawaziri wanaotajwa kwa kuvaa Mikoba hiyo ni Waziri wa Habari, Nape Nnauye; Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile na Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene.

Pia, yumo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Juma Homela-Mbeya; Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makala na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda.

Taarifa zinaonesha kwamba Katibu Mkuu mpya anatarajiwa awe ni mbombezi kwenye Mipango na Mwenye haiba lakini mwenye umri wa Ujana ili kuleta mvuto wa kundi kubwa la Vijana wa Nchi hii ambao wanatajwa kufikia 75% ya Watanzania.

Kadhalika Katibu huyo anatarajiwa awe Mtiifu asiye na mashaka kwa Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hasaan ambaye kama ilivyo desturi ya CCM anatazamiwa kuwa Mgombea pekee kwenye uchaguzi ujao wa 2025 ndani ya CCM.

Kwenye barua ya Kujiuzulu Katibu Mkuu, Chongolo amehitimisha kwa kutoa tahadhari ya kumsihi Rais Samia awe makini dhidi ya watu wenye hila dhidi yake Rais, Chama na Taifa na akahitimisha kuendelea kuwa mtiifu kwa Chama siku zote. Kauli hii imeibua minong'ono na imezidi kutoa mwanga pengine ndani ya Chama hicho wako Makada ambao wangekuwa hawana nia njema na Rais na Chama chao kwa mwaka 2025.

Soma Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu
 
Wamo Mabalozi, Wastaafu, Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Vijana Chipukizi.

Kufuatia Katibu Mkuu Daniel Chongolo kuachia ngazi, wimbi la kupata Mrithi limezidi ongezeka Mtaani huko Dar es Salaam...
Hiyo para ya mwisho ya barua ya Chongolo nafikiri alikuwa anamlenga Makonda ambaye ameapa kwa mizimu yote kuwa yeye atakuwa mtiifu kwa Magufuli hata angewekewa bunduki kichwani.
 
Wamo Mabalozi, Wastaafu, Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Vijana Chipukizi.

Kufuatia Katibu Mkuu Daniel Chongolo kuachia ngazi, wimbi la kupata Mrithi limezidi ongezeka Mtaani huko Dar es Salaam...

Hakuna jema lolote watakalolifanya , nchi na wanyonge wakafaidika, yote ni MI CCM Wacha yote ijiuzulu haina heri hata moja
 
Aisee Kwa siasa za Sasa lazima tuangalie kundi kubwa la vijana ambalo ndio asilimia kubwa la watu na katibu mkuu awe mtu ambaye atashika makundi yote naibu waziri kijana aliyetajwa anaweza kutufaa kabisa.
 
CCM wana macho sana sana wanajua kuona Nani anafaa kwa wakati gani katika hao wote tajwa naona wananafasi labda watatu tu.

1. Simbachawene sababu Ana utulivu huwa hakurupuki.

2. Namuona Naibu waziri Uchukuzi David Kihenzile Ana uwezo mkubwa ndani ya Mda mfupi Bunge kaendeshe vyema kapewa Wizara Kama msaidizi kazunguka Nchi nzima kukagua viwanja vya ndege bandari na taasisi tanzu.

3. Namuona Paul Makonda moja sababu Ana pendwa sana na mama pili ni Mtiifu kwa mamlaka
 
Mh naibu Waziri wa Uchukuzi,ni muwajibikaji,ni kiongozi anayeonesha mfano kwa kizazi na vizazi,tunapaswa kuangalia viongozi ambao wana maono kama Kiongozi huyu,natumaini anafaa kuwa katibu Mkuu
 
Back
Top Bottom