Kama wewe ni mpambanaji na ambitious mambo kama UTT, Bonds na Savings Accounts sio type yako, waachie waoga na watumishi

Teslarati

JF-Expert Member
Nov 21, 2019
1,735
6,796
Naongea sana mambo yasio serious humu jukwaani ila ngoja nifunge mwaka kwa kuongea sense kdg.

Kuna nyuzi humu zinaongelea mambo ya UTT na Bonds, niwaambie ukweli haya mambo ili ikulipe kwa zile monthly returns ni lazima kwanza uweke hela kubwa sana, more than 500m, na incase ukiweka 1 billion ndipo utakua una uhakika wa kupata angalau million 5 kila mwezi.

Bonds (hata UTT) zina muda mrefu sana wa kuexpire, hapo ukifactor in inflation unajikuta hela yako ni ile ile. Mfano kama uliweka 100m mwaka 2012 ambapo dola 1 ilikua almost 1200 tzs, sasa ukaja kuvunja kibubu mwaka 2018, factor in thamani ya tsh ya muda huo utakuta 'value' (thamani) ya hela yako ni ile ile.

Fanya smart investing, vitu kama land, gold na profitable businesses havipigwi thamani na inflation, hizo ni constant stores of value. Wewe kama una 100m ya kuwekeza nenda kanunue gold au land au wekeza kwenye biashara (tafuta mtaalam akufanyie analysis kwanza) ukiweka UTT au kwenye Savings account au ukanunua bonds ujue unaenda kuwatajilisha watu. Sababu kuna watu tutatumia hela zako hizo kupiga mabilion na kukupa ww return ya 0.001

Ngoja nikupe mfano, personally mm na-manage utajiri wa watu na mashirika kadhaa hapa mjini na nchi nyingine. Sasa kuna baadhi ya wateja wangu niliwatengenezea mchezo mmoja mwaka fln, tunakopa banks(hela zenu za savings) kwa kuweka baadhi ya assets za hao wateja kama collateral, hio mikopo inatumiwa kwenye real estate, tunanunua maeneo potential kuna michezo hapo inafanyika kuservice hio loan na mwisho wa siku hata kodi inapungua sababu natumia debt (nikiendelea kuna watu tutapotezana hapa). Yaan kiufupi matajiri wanazidi kuwa matajiri kwa kutumia hela zako.

Na kingine, jitahidi kuwekeza sehemu ambapo unaweza control (Business, Gold, Real estate), ukiweka sana bank hela yako siku hio bank ikifilisika utajua hujui, ukinunua bonds za serikali siku serikali ikidefault (kama zinavyofanya nyingine) utajua hujui. Bonds pekee safe kununua ni za Japan na USA pekee

Sisemi kwamba bonds ma savings sio sahihi, lakini hapa naongelea watu 'ambitious' wanaotaka kutajirika, do not lock your money, mfano elon musk ni tajiri namba 1 lkn hela yake yote ipo tied na stock, ofcoz situation ya elon ni complicated sababu ina faida na hasara. Lakini ukisikia elon musk anasema hana nyumba wala yatch sio kwamba anapenda, uchumi haumruhusu sababu 90% ya utajiri wake ni locked.

Sasa ww kama ni mpambanaji wekeza kwenye biashara, real estate na gold, hayo mengine waachie watumishi na waoga wa maisha.

Note: huu uzi ni kwa ajili ya those 'fearless and ambitious financial motherfvckers'

Happy new year in advance!
 
Kama utaweza kufikia level ya kutumia Debt kujitajirisha basi wewe umefikia Nirvana kwenye finance.

Wengi Debt inawafirisi lkn wachache wanajua kucheza nayo ili kutajirika, na hao wana assets ambazo mara nyingi wamezipata kutumia debt, ni endless game hadi utakaporidhika.

Na nikuibie siri, ukitumia debt sheria zinakulinda kukwepa kodi.
 
Huu uzi mzuri hivi ilikuaje sijauona. Mkuu elezea zaidi hapo kwenye kutumia dept. Mi sina hata mia bank yaani bank ni inapita tu,siwez eka hata milion 10 in a week yote inangia kwa mzunguko. Hivi kwanini watu wanazificha ela bank?
 
Bank sio shm nzr kutunza hela, bank ni sehemu ya kuzungushia hela yaan kutengeneza credit score

Mfano ww umekopa ukawekeza kwenye real estate, hutowahi kulipia income tax. Tunza hela yako huko, hata uwe gaidi hawatozuia huo mzunguko, na kuna njia nyingi kama hizo.

BTW sijasema watu wanaficha hela bank, huko mda wwt wanakufungia tu ukikosana na wakuu.

Somo kama hili kwa mtoto mzr kama ww linanoga ukiwa unapiga wine na mm nashushia Jagermeister, then nakuambukiza mautaalam.
 
Bank sio shm nzr kutunza hela, bank ni sehemu ya kuzungushia hela yaan kutengeneza credit score

Mfano ww umekopa ukawekeza kwenye real estate, hutowahi kulipia income tax. Tunza hela yako huko, hata uwe gaidi hawatozuia huo mzunguko, na kuna njia nyingi kama hizo.

BTW sijasema watu wanaficha hela bank, huko mda wwt wanakufungia tu ukikosana na wakuu.

Somo kama hili kwa mtoto mzr kama ww linanoga ukiwa unapiga wine na mm nashushia Jagermeister, then nakuambukiza mautaalam....
Oooh I don’t drink but thanks
Sina elimu yoyote ya fedha lakini kimtaa tukikutana utashindwa kutofautisha kati ya jager na mimi nani master
 
Back
Top Bottom