Mwanamke usibebe mimba kama huna 1.5M uliyoi-save kama akiba ya dharura mwenyewe

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
* Haijalishi una kazi au hauna kazi mchune mumeo au mpenzi wako unayetaka kumzalia ficha hela mpaka zifike 1.5M ndiyo ubebe mimba utakuja kunishukuru*

Najua kabisa wnaume wezangu mtakuja hapa kunipopoa , na wale wanawake wasiojali wala kupenda uhai wao binafsi wanaosema mwanaume majukumu mtakuja hapa kutema cheche na kunitukana , wengine watasema siyajui maisha ila ukweli acha niwaambie hawa dada zangu kwa sababu mimi binafsi napenda sana wanawake ukitoa hela, pombe na wazazi wangu japo kuna muda naonekana kuwakandia sana lengo ni kusema ukweli ili kuokoa kizazi chetu na wanawake wabadilike

Wanawake leo nipo hapa kuwaambia ukweli kwamba kamwe usibebe mimba kwa namna yeyote ile iwe kwa makubaliano, iwe kwa masharti ya ndoa, mapenzi , kudanganywa , kulaghaiwa, iwe kwa hamu na tama zako wewe uwe na mtoto kama huna milioni moja na laki tano (1.5M) ya kwako binafsi uliyojiwekea akiba kwaajili ya heka heka za ujauzito,usalama wa leba pindi unapojifungua, afya yako binafsi pamoja na mtoto , pia na kwa usalama wa uhai wako mwenyewe na malezi ya mtoto mwanaume akiwa anagoma kuhudumia au akianguka kiuchumi au kutelekezwa kwa namna yeyote ile

wanawake wengi wanafariki mahospitalini , njiani au majumbani pindi wanapofikia muda wa kujifungua au wanapotoka kujifungua , wengine wanabakia kuwa walemavu sana na wengine watoto wao waliojifungua wanafariki huku wengine wanaopona wanakua walemavu na wenye maradhi ya kujitakia ya kudumu na hili husababishwa na uzembe wa manesi katika vituo vya afya kwa mianya ya rushwa na kukosa chochote kitu cha kumpa kama posho, hela ya kununulia vifaa vya maandalizi ya kujifungua, mazingira salama ya kujifungua ,pamoja na hata kujifungulia hospitali za hadhi angalau na zenye huduma nzuri

Pia hili huchagizwa na wanaume wao wajinga waliowapa mimba, ubahili wa wanaume , kutokujali thamani ya mwanamke uliyempa mimba na uhai wake mama na mtoto pamoja na ubinafsi wa ndugu zao wa pande zote hasa wa mwanaume kwa kisingizio chakukosa hela za dharura kipind cha mimba na kujifungua pamoja na malezi.

hakikisha mwanaume akitaka kukupa mimba hata kama ni mumeo, rafiki au mpenzi wako kabla ya zoezi la kutafuta mtoto umehifadhi shilingi 1.5M kama akiba ya dharura kipindi chote cha ujauzito na kipindi chote cha malezi ya mtoto akiwa mdogo mpaka afikishe miaka 3 angalau, usisikilize maneno ya mwanaumr hakikisha hiyo ela unayowewe mwenyewe tena iwe kwenye bank a/c yako yenye details zako mwenyewe pasi na kumshirikisha mtu na sii kwenye a/c ya mwanaume.
 
Nyingi sana hyo mkuu acha kutisha watu,unajua hali ya mtanzania wa kawaida hyo 1.5m anaisave ndani ya mda gan?

Juzi tu hapa kuna jamaa kaleta thread analipwa 400k kwa mwezi na ni mtumishi je anatumia sh ngap na anasave kiasi gani?

Huyo ni mtumishi vp kwa watanzania wa kawaida?

Jambo la kushauri watu ni kujiandaa kwa kununua vifaa vya kujifungulia ambavyo mahospitalin wanasisitiza na kiakiba kidogo walau kuanzia 50k na kuendelea..
 
Cheza hapo kwenye na kuendelea .....
1.5M ni ndogo sana kuliko uhai wa mwanamke wako na mtoto
 
Kwa wastani wanaume huwa hawasemi au kutaka kuwapa ujauzito mabinti bali mabinti kwa utashi wao binafsi huamua kuwa sasa nabeba ujauzito halafu nitamwambia halafu yeye ataamua iwaje.

Katika mazingira hayo sasa I think its fair kusema mabinti waanze kuwa responsible na maisha wanayochagua kuishi.
 
Kwa kuanza kusave hiyo 1.5 atajua atapataje au atachuna mwanaume wake kikubwa ahakikishe ana 1.5M ndiyo ajibebe mimba. Tumechoka maana wanakufa kama kuku huko kwa kukosa hela za shortcut
 
The same to mwanaume. Kama huna chanzo cha uhakika cha pesa usimbebeshe mimba mtoto WA MTU. Maana utasababisha mateso Kwa mama mtoto na kiumbe
Wanawake ndiyo wanaobeba na wenye kuamua kubeba au kutokubeba mimba. Wakikaza watasaidia san wanaume tupambane zaidi na itatujengea kuwa kabla ya kumpa mwanamke mimba tujiandae kifedha zaid
 
* Haijalishi una kazi au hauna kazi mchune mumeo au mpenzi wako unayetaka kumzalia ficha hela mpaka zifike 1.5M ndiyo ubebe mimba utakuja kunishukuru*

Najua kabisa wnaume wezangu mtakuja hapa kunipopoa , na wale wanawake wasiojali wala kupenda uhai wao binafsi wanaosema mwanaume majukumu mtakuja hapa kutema cheche na kunitukana , wengine watasema siyajui maisha ila ukweli acha niwaambie hawa dada zangu kwa sababu mimi binafsi napenda sana wanawake ukitoa hela, pombe na wazazi wangu japo kuna muda naonekana kuwakandia sana lengo ni kusema ukweli ili kuokoa kizazi chetu na wanawake wabadilike

Wanawake leo nipo hapa kuwaambia ukweli kwamba kamwe usibebe mimba kwa namna yeyote ile iwe kwa makubaliano, iwe kwa masharti ya ndoa, mapenzi , kudanganywa , kulaghaiwa, iwe kwa hamu na tama zako wewe uwe na mtoto kama huna milioni moja na laki tano (1.5M) ya kwako binafsi uliyojiwekea akiba kwaajili ya heka heka za ujauzito,usalama wa leba pindi unapojifungua, afya yako binafsi pamoja na mtoto , pia na kwa usalama wa uhai wako mwenyewe na malezi ya mtoto mwanaume akiwa anagoma kuhudumia au akianguka kiuchumi au kutelekezwa kwa namna yeyote ile

wanawake wengi wanafariki mahospitalini , njiani au majumbani pindi wanapofikia muda wa kujifungua au wanapotoka kujifungua , wengine wanabakia kuwa walemavu sana na wengine watoto wao waliojifungua wanafariki huku wengine wanaopona wanakua walemavu na wenye maradhi ya kujitakia ya kudumu na hili husababishwa na uzembe wa manesi katika vituo vya afya kwa mianya ya rushwa na kukosa chochote kitu cha kumpa kama posho, hela ya kununulia vifaa vya maandalizi ya kujifungua, mazingira salama ya kujifungua ,pamoja na hata kujifungulia hospitali za hadhi angalau na zenye huduma nzuri

Pia hili huchagizwa na wanaume wao wajinga waliowapa mimba, ubahili wa wanaume , kutokujali thamani ya mwanamke uliyempa mimba na uhai wake mama na mtoto pamoja na ubinafsi wa ndugu zao wa pande zote hasa wa mwanaume kwa kisingizio chakukosa hela za dharura kipind cha mimba na kujifungua pamoja na malezi.

hakikisha mwanaume akitaka kukupa mimba hata kama ni mumeo, rafiki au mpenzi wako kabla ya zoezi la kutafuta mtoto umehifadhi shilingi 1.5M kama akiba ya dharura kipindi chote cha ujauzito na kipindi chote cha malezi ya mtoto akiwa mdogo mpaka afikishe miaka 3 angalau, usisikilize maneno ya mwanaumr hakikisha hiyo ela unayowewe mwenyewe tena iwe kwenye bank a/c yako yenye details zako mwenyewe pasi na kumshirikisha mtu na sii kwenye a/c ya mwanaume.
Muhimu kusave hela kuendane na mambo mengine ila kusave kwanza hela ndo ubebe mimba aisee hela yenyewe tunapata kiduchu kiduchu tutafikisha idadi ya watoto tunazozitaka kwel
 
Huu ni ukweli wa kukusaidia usiende kufia leba kizembe zembe sana au ukazaa mtoto kachoka na aliye kunywa maji machafu kwa uzembe
Acha Uoga wewe
Ingekuwa hivi Tanzania ingekuwa na depopulation ya kufa mbwa. Hem tuacheni tuzaliane, hatuna mia ndani na tunawaweka mimba.
Nyie ndio malegend Sasa!watu wanaendelea na shughuli za uzazi kama kawaaaaa
 
Back
Top Bottom