Sijamuelewa huyu binti

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,220
56,867
Ni kama jini si jini!,labda niseme mzuka lakini ni mzuka gani unawezakuwa mzuri kiasi kisichoelezeka..??!

Kufupisha mambo sitasimulia nimekutananae vipi ila baada ya majuma kadhaa yakuzoeana akanikaribisha anapoishi.

Ilikuwa mida fulani ya mchana ambao jua lilikuwa likipambana na mawingu kuhakikisha mionzi yake inatufikia wana wa adam na kutunyoosha vilivyo!,lakini halikufanikiwa ushindi ulipokwa na mawingu.

Kwa sauti yake nzuri na tabasamu jepesi akanikaribisha. nami nikiwa mwingi wa furaha nikakaribia.
wakati ananiongoza kwenda kuketi ndipo hapo nikaanza kuufaidi uzuri wake wa nyuma ambao kila siku ulizidi kushamiri kama ua rose nyakati za mvua.

Jini mimi jicho langu moja kwa moja likatua kwenye uno lake ambalo hazina iliyokuwa imetuna kwa viwango vyakimataifa ilihanikiza kutazamwa.

Mwendo wake wa maringo ulienda sambamba na mgongo wake ulioingia kwa ndani kana kwamba ulihitaji uangalizi wa daktari!,lakini la hasha labda alihitaji daktari fundi wakucheza na mgongo huo.

Kabla sijamfaidi vyema akanikaribisha niketi sofanpoi,nikaketi ndipo hapo tena tabasam lake likanishambulia kwa tashtwitwi! kisha akaniuliza"

Vipi utakunywa juice au maji," aka pose kisha akamalizia "maana ndo vinywaji nilivyonavyo kwasasa..." alipotaka kuendelea kujitetea nikamkatisha kwa kumuambia usijali maji yatanitosha.

Taratibu akageuka nakuliendea fridge ndipo tena nikapata wasaa wakuidalizi miguu yake iliyojaa barabara!, nafikiri hata miguu yake ilijionea fahari kuubeba mwili wa binti mzuri ambae kama utashindwa kumfananisha na malkia wa sheba basi utamfananisha na malaika japo malaika huyu amekosa mbawa tu.

Nikiwa bado nashangaa akanigutua kwa kunikaribisha na glass ya maji ambayo ilikuwa imeshatua mezani!!,baada ya hapo zikafuata stori mbili tatu ndipo akaamua afanye tendo ambalo aidha sikudhania.

Akiwa ameketi ubavuni mwangu taratibu akanisogelea nakunishushia busu maridadi.
nikajikuta nimenasa kama mtu aliekoswakoswa na risasi ya jambazi sugu.

Taswira ya tabasam lake ndio ikanichanganya zaidi!,nikakosa lakuzungumza,akaona isiwe tabu akanikumbatia kabisa nakuniambia ananipenda.
Umotomoto wakumbatio lake ukanifanya nisahau kama nimeambiwa ninapendwa!.
akaniachia nakuniuliza "mbona husemi kitu!"

Kabla hata sijajibu simu yangu ikaita.
Ilikuwa simu ya kazi ikinitaka nijipeperushe kurudi kazini nakumuacha huyu malaika aliekoswa mbawa peke yake.
Niliondoka nakumuacha.

Zikapita siku kadhaa tukiwa na mawasiliano ya simu tu pasipokuonana!..
Weekend fulani nikaamua nimtoe out ili sasa huko nikapate kusikia anayotaka kunena nami ninene ili tunene ikibidi nimpatie na unene hapo baadae!.

Ilikuwa mahali swafi karibu na ufukwe fulani hivi tukaketi vitini, mahanjumati fulani mezani huku stori mbili tatu zikisindikiza.. baada ya mlo glass ya white wine ikatua mikononi mwake nami ikatua glass ya red wine.

ule wasaa wakujua kinagaubaga ukawa ndio huu,nikamkumbushia ile siku aliyonikaribisha kwake akaitikia vyema kabisa kuwa anaikumbuka kisawasawa pia nikagusia na swala aliloniambia!. ndipo hapo lile zimwi ambalo lilikuwa limelala likaamka.

Just from no where akaamka kama mtu mwenye jaziba hadi waliokuwa wameketi karibu yetu wakagituka!, akanitazama kwa tuo! akataka kusema kitu hakusema! nami nikainuka lkn kabla sijainuka vizuri akaukwapua mkoba wake nakuanza kuondoka kwa spidi kali.

Nikabaki kama kituko mbele za watu wote, sura zao waliokuwa wakinitazama ziliongea mengi!..
wengine kana kwamba zilinena "huyu mlugaluga kakosea kutongoza!"

Sura nyengine zilionyesha cheko tu hata zisijue zilichekea nini!
Wengine walihisi labda ni filamu tulikuwa tukiigiza.

Chap nikamfata lakini tayari alikuwa ameshapandia boda nakutokomea mbali!.
Dakika chache simu yake haikupatikana na baadae nikalambwa block!!

Sijui nimekosea wapi,au napimwa ama nimekutana na mtu mwenye matatizo ya afya ya akili?
sielewi bado!
 
😂 kijana akikumbuka alikuachia uwanja upambane ukaondoka mpaka leo hajakumaliza

Tulia utampata tu

Nawewe hukutakiwa kukumbushia
Automatikale ungejipa jimbo😁👍🏽
 
giphy (1).gif


PambanaZaidi/CottonandMore
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom