Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,892
- 3,197
Ukweli mchungu sana kwamba katika nchi za kishenzi ili uwe tajiri, basi uingie kwenye siasa.
Lakini katika nchi zinazojielewa kama Marekani na nchi za Ulaya, ili uwe kiongozi wa kisiasa lazima uwe vizuri kiuchumi, yaani ni lazima uwe tajiri.
Hii hali huwa na athari mbaya kwa nchi zetu kwa maana sehemu kubwa ya wanasiasa wetu, wako pale kwa maslahi yao binafsi badala ya kuwepo kwa maslahi ya Taifa na nchi kwa ujumla. Ndiyo maana utakuta waziri anasaini mikataba ya hovyo sana kwa sababu tu amepewa kiasi kidogo cha rushwa.
Kama kweli tumeamua kupiga hatua kama nchi, basi inatupasa ifikie mahali kila mwananchi apigie kelele suala la ufisadi na ubadhilifu wa mali za Umma. Pia tusidanganyike kuchagua watu kwa kuhongwa tshirt, kofia, kanga, vitenge, chumvi, sukari n.k ili kuwachagua viongozi wetu kwa sababu gharama zake ni kubwa sana na imekuwa ikitugharimu sana kama Taifa..