Mkuu tupe hata kwa ufupi kwani utasaidia wengine watu watajifunza. Please fanya hivo
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kwanza nikiri kuwa ujinga wangu na pupa yangu ndio vimechangia kwa asilimia kubwa kuingizwa mjini kiasi hicho.
Kipindi hicho ndio naanza chuo mwaka wa kwanza, nilipata boom nikiwa nimechaguliwa kusoma koz ya Afya. Boom kwa wanafunzi wa kozi za Afya ni kubwa kuliko la waafunzi wa kozi ambazo sio za afya.
Nilifanya hatua zote za usajili chuoni na kufungua account ya CHAP CHAP (NMB) kwa ajili ya kuwekewa boom. Sasa baada ya hapo nikawa nasubiri boom liingie nianze kuonja mkwanja wa serikali. Boom lilipoingia rafiki yangu akanishtua kwa simu mida ya usiku akaniambia mpunga ndani ya kikapu, moyo ukashtuka paaa!! Nikasema asubuhi nitaenda kudrawal laki 2 kwanza nikafanyie shopping na mazagazaga mengine ya chuo.
Wakati kabla nasubiri boom liingie nilijaribu kufanya practice ya kutumia ATM lakini ilikuwa ni juu sana.
Kesho yake asubuhi na mapema saa 12 kasoro mwanaume nikatinga ATM pale Ubungo Shell, nilipofika tena kwa shauku kwenye hiyo ATM ambayo ilikuwa na sehemu tatu za kutolea hela nilikuta kuna jamaa anatoa hela kwenye tundu moja lilikuwa ndani kidogo halafu mengine mawili yapo kwa mbele, mimi nikaenda kwenye haya matundu ya mbele ambapo moja lililkuwa halifanyi kazi na maelezo yalikuwa yameandikwa pale kwenye kioo kuwa haifanyi kwa muda huo.
Bila kukawiwa nikaingiza card yangu ya Chap Chap kabla sijaanza kuandika neno la siri yule jamaa ambaye alikuwa kwenye tundu la ndani akaja fasta na kubonyeza kitufe chakusitisha process za kutumia ATM halafu kadi ikarudi na akaishika huku akiniambia hii haifanyi kazi njoo huku kwenye tundu ambalo alikuwa anatolea yeye, na nikifikiria jinsi kadi ilivyorudi fasta bila kujua kuwa ndio yeye kairudisha nikaamini na akiwa ameishikilia kadi yangu tukaongozana hadi alipokuwa anatolea pesa na akaingiza card fasta bila mimi kugundua kuwa kanibadilishia kadi na kaingiza fake. Akaniambia(huku amesimama pembeni yangu kwa nyuma kidogo) weka namba ya siri. Nilipoingiza namba zikasomeka live bana tofauti na kawaida ambapo zinaonesha ****, kumbe kazikariri fasta na akabonyeza OK mashine ikaniambia weka namba ya siri ya mtu aliyekutumia pesa(hapo nikapigwa shot kwanza), akaniambia iweke sasa hiyo namba nikamwambia siijui, kumbe kitendo cha kubonyeza fasta fasta ilikuwa mbinu ya kunipoteza alipoona nishapotea halafu tayari namba ya siri kaiona kasepa na kuniacha nikiwa nang'ang'ana na mashine.
Baada ya kuona jambo limenigomea nikaamua nijaribu kuitoa kadi ikagoma, ghafla mashine ikaanza kupiga kelele, daahh! Kumbe ile kadi ambayo ilikuwa fake imeshamezwa. Nikamfuta mlinzi nje nikamueleza tatizo nikmuomba anisaidie kuitoa kadi, alipoenda kuangalia akaniambia ishamezwa hiyo, pia akaniuliza kama kuna mtu alikuwepo na amejaribu kunisaidia nikakiri nikamueleza movie ilivyokuwa. Akanishauri niende Mlimani city ifikapo saa mbili nikasaidiwe kuhusu hilo tatizo, ilipofika saa mbili tayari nilikuwa nishafika hapo Mlimani city nikawaona wahusika pale nikaeleza mkasi ulivyokuwa halafu nikawapa account namba wakacheki tukakuta jamaa kashajizolea mzigo kitambo(yaani baada ya nusu saa aliponiibia kadi) halafu kanibakishia buku 8 tu.
Sikuwa na ujanja zaidi na nguvu za kufuatilia zikawa zimeniishia nikabaki naugulia maumivu ya hatari sana maana boom limesepa lote.
Aisee huo mkasa sitausahau labda utokee mwingine wa kureplace