Acheni acheni kabisa, matapeli achana nao. Mimi nimetapeliwa mara nyingi na kwa mambo tofauti tofauti. Ikiwemo ajira, biashara, utajiri na nk. Lakini utapeli mkubwa nisioweza kuhusahau ambao ulihatarisha kuvunja ndoa yangu, ni kutapeliwa uwanja Tegeta masite. Hapo sitakuja kusahau. 2002 niliuziwa uwanja milioni 3, mbele ya wanasheria siwezi kuwaandika, maana kila walichokitaka wanasheria jamaa wali submit tena og. Yalifanyika malipo nikapewa document zote, ilikuwa offer. Sitakuja kusahau nakuambia. Nilikuwa na hamu sana kuwa na nyumba, nikaweka tofari zaidi ya elfu2, mchanga, kokoto nyie acheni tu. Ita mafundi wakafanya setting ya msingi, kazi imeanza nikapata safari ya SA, lakini huku niliacha kila kitu safi yaani nikirudi no kupaua tu. Jamani niko Durban napigiwa simu, huku balaha uwanja huu ni wa mtu. Aiseeh naumia sana, acheni tu ila Mungu anawaona.