Matapeli wako na akili Mingi Sana



Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa naka grocery changu some where, kuna mzee mmoja alikuwa mteja wangu Sana kipindi hicho, isitoshe ndio alikuwa amekula pesa ya mafao baada ya kustaafu uwalimu. Hivyo kifedha alikuwa mtamu.
Kipindi hicho ndio Brevirs zinaingia bila Mil 13+ huwez pata, kuna majamaa walikuwa wawili walikuja na hiyo gari, chombo ilikuwa mpya...haina plate number zaidi ina chasers no. kwenye kioo ilikuwa rangi ya Silva.
Wakaja pale na story nyingi wakijifanya watu wa madini..na walikuja mjini kwa ajili ya kutumia baada ya mgodi wao kutema..hvy muda wote wanazungumza na hayo mambo wanakunywa bia za kutosha huku wanamnunulia na yule mzee.
Basi wakasema mwaka huu umekuwa wa neema kwao kwani wamepata simu mgodi umelipua Tena(umetema) hivyo hawawezi kukaa Tena mjini inabidi warudi pori.
Hivyo inabidi hilo gari wauze kwa bei ya hasara, kutokana muda wa kulitumia watakuwa hawana...ht hvy wakitoka huko watachukua chuma kingine kikali.
Mara mzee mstaafu kaingia mkenge kawauliza mnauza Tsh ngapi...wale majamaa wakacheka, wakamuuliza mzee unapesa ya kununua gari wewe?
Mzee akasema sio moja



nyie vijana wa siku hizi mnatudharau Sana wazee...wakamwambia kama unayo Mil 10 tunaenda kukuchukulia kadi tunakuachia gari Hy hata nuksi haina.
Mzee akasema kama ni 7Mil Sasa hv tunaenda bank...majamaa wakaangalina wakamwambia ngoja tufanye tumekupa sadaka...wakatoka wakaenda kumpa kadi feki...baada ya mzee kuwapa fedha wakarudi baa kugonga mvinyo kwa kwakuwa mzee hajui kuendesha wakamwambia mpigie dereva aje kukuchukua wakamwachia funguo feki na kadi feki wakatoka nje wakachukua ndinga wakasepa.
Biashara ilifanyika kama masaa matano hv mzee anarudi analia amepigwa Mil 7 Kama mchezo




Sent using
Jamii Forums mobile app