Nililipia haja ndogo kwa 7000/=
Nimetoka zangu kuripoti Form Five pale Ilboru Secondary nikasema ngoja nikatalii jiji la Arusha wanapaita Arachuga.
Kufika mjini nikabanwa sana na mkojo.
Nikawa naogopa kuulizia choo cha kulipia kiko wapi SABABU nishaambiwa Arachuga kuna wahuni. Basi pembeni palikua na makaburi, nikasogea kwenye mti nikaanza kukojoa.
Ile namaliza tu, jamaa wawili wamevaa makoti wakaja.
Wakanipiga sana mkwara, kuwa wao ni maafande wa mazingira. Wakasema twende kituoni nikawekwe ndani.
Nikaanza kuwabembeleza, wakasema nitoe 30,000 waniache. Daaah, mfukoni nilikua na 7000 tuu.. Nikawapa wakaniachia.
Nikashukuru sana. Nikarudi shule fasta mkojo mwingine usije kunibana nikaumbuka tena.