lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,154
- 33,365
Tutakuwa na Rais Samia kwa kipindi cha miaka takriban mitano kabla ya Uchaguzi Mkuu kama mambo yakienda hivi bila Mungu kufanya yake. Inshallah naomba asifanye.
Kama nikiulizwa leo hii je unauonaje Utawala wa Samia?
Je, kwa jinsi Samia anavyoongoza unaona ni vema Magufuli angekuwepo?
Unajua katika Maisha huwa kuna wakati huwa tunawakumbuka Marehemu kwa uwezo wao na nafasi zao katika jamii kuanzia ngazi ya familia.
Jibu langu katika maswali hayo ni moja tu.
Ni afadhari mara mia Samia abaki miaka 10 kuliko Miaka mitano ya Magufuli.
Samia na Magufuli ni mbingu na ardhi.
Samia ana utu,ana hofu ya Mungu,hana kiburi,hana dharau,hana chuki,hana visasi,msikivu,hana roho mbaya,ana nidhamu,sio mkatili,ana heshima,ana heshimu wataalamu,viongozi wa dini,wazee na vijana.
Samia mtoto wa mjini hana mambo ya kishamba.
Anaeheshimu wakulima ,wafanyakazi na wafanyabiashara.
Hawazi kupoteza watu,
Ana huruma,hawezi kufurahia kuona mtoto wa mtu akipotezwa kwa sababu ya tofauti za kisiasa.
Hata ukiangalia body language za watu mitaani,Wana amani Sana.
Hana hotuba za vitisho wala dharau.
Ana vijimaneneo vyake tu vya kipwani,au kimamamama lakini sio sio maneno makali.
Kitu pekee kitamharibia Samia kama asipocheza karata zake vizuri ni Kesi ya Mwamba Mbowe tu.
Vyovyote itakavyokua Samia Sio Mkatili.
Hawezi kuruhusu au kufurahia mambo kama yaliyompata Lisu yatokee ndani ya awamu yake,
Hawezi kupanua barabara na asiwalipe wahanga.
Ukweli ni kwamba Kwangu mimi ni bora Samia kuliko Jiwe.
Nchi ilikokuwa inaelekea Ni Mungu tu ndio ajuaye.
Hivi kw mfano mambo haya ya kuogofya na kutisha aliyokuwa akiyafanya Sabaya Intelijensia za akina Sirro hazikuyaona?