Kama nikiulizwa kuwa nimeridhika na Utawala wa Rais Samia au ninamkumbuka Hayati Magufuli

Katika hili la kutokutaka kurithi maadui wa mtangulizi wake amefanikiwa sana toka aliposhika hatamu kwasababu aliwafutia kesi watu wengi waliowekwa kizuizini kwa ishu za kisiasa, uhujumu uchumi nk

Ila wapuuzi wachache kama kina Mdude Nyangali, Mbowe, Heche nk waliopo Chadema wakaanza kutoa kauli za kumdhihaki na matendo ya kumchokoa chokoa, hapa Mamá akaamua kufungua makucha yake ili akili ziwakae sawa
Yap!! Walimu underate sana na kumdharau. Wakaanza kudai vitu ambavyo hawakuthubutu kwa Mwendazake kwa miaka 5
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Mbowe aliomba katiba mpya leo yuko nyuma ya nondo akiwa na title sawa na Abubakar Al Baghdad na Abubakar Shekau
 
Twitter na JF huwez AMINI kama nao ni watanzania. Huko FB na Ista ktk comment 1000,hazifiki 20 za kumponda Magufuli. Maoni sahihi na ya watanzania wengi huwez yapata Twitter au JF

JF asilimia kubwa yamejazana manyumbu ya Chadema,
JF imekuwa kama tawi la mtandaoni kwa Chadema hvyo kila kitu wao ni kupinga tu, kutwa kucha ni kuliombea Taifa mabaya na kuwaombea mabaya viongozi wa nchi hii

Ila ni ukweli ulio wazi kwamba Watanzania walio wengi hawatumii hii forum na ukitaka upate picha halisi ya maoni yao basi nenda FB, Insta, comments za YouTube clips na kwenye hili nenda katafute video clip yoyote ya Magufuli YouTube alafu soma zile comments utaona namna commentators wanavyomkubali Magufuli
 
Wewe umejuaje ana hofu ya mungu, wewe umekua mungu hadi umsemee?

Unafiki na kujipendekeza hakutawasaidia.

Kuna mwenzako jana alisema akienda jehanamu sijui peponi asipomkuta samia anaondoka, sasa sijui yeye amejuaje kama huko peponi ataenda kama kweli kupo.
Mbona wewe ulikuwa unajipendekeza kwa jiwe
 
Tutakuwa na Rais Samia kwa kipindi cha miaka takriban mitano kabla ya Uchaguzi Mkuu kama mambo yakienda hivi bila Mungu kufanya yake. Inshallah naomba asifanye.

Kama nikiulizwa leo hii je unauonaje Utawala wa Samia?
Je, kwa jinsi Samia anavyoongoza unaona ni vema Magufuli angekuwepo?
Unajua katika Maisha huwa kuna wakati huwa tunawakumbuka Marehemu kwa uwezo wao na nafasi zao katika jamii kuanzia ngazi ya familia.

Jibu langu katika maswali hayo ni moja tu.

Ni afadhari mara mia Samia abaki miaka 10 kuliko Miaka mitano ya Magufuli.

Samia na Magufuli ni mbingu na ardhi.

Samia ana utu,ana hofu ya Mungu,hana kiburi,hana dharau,hana chuki,hana visasi,msikivu,hana roho mbaya,ana nidhamu,sio mkatili,ana heshima,ana heshimu wataalamu,viongozi wa dini,wazee na vijana.

Samia mtoto wa mjini hana mambo ya kishamba.

Anaeheshimu wakulima ,wafanyakazi na wafanyabiashara.

Hawazi kupoteza watu,
Ana huruma,hawezi kufurahia kuona mtoto wa mtu akipotezwa kwa sababu ya tofauti za kisiasa.

Hata ukiangalia body language za watu mitaani,Wana amani Sana.

Hana hotuba za vitisho wala dharau.
Ana vijimaneneo vyake tu vya kipwani,au kimamamama lakini sio sio maneno makali.

Kitu pekee kitamharibia Samia kama asipocheza karata zake vizuri ni Kesi ya Mwamba Mbowe tu.

Vyovyote itakavyokua Samia Sio Mkatili.
Hawezi kuruhusu au kufurahia mambo kama yaliyompata Lisu yatokee ndani ya awamu yake,

Hawezi kupanua barabara na asiwalipe wahanga.

Ukweli ni kwamba Kwangu mimi ni bora Samia kuliko Jiwe.

Nchi ilikokuwa inaelekea Ni Mungu tu ndio ajuaye.

Hivi kw mfano mambo haya ya kuogofya na kutisha aliyokuwa akiyafanya Sabaya Intelijensia za akina Sirro hazikuyaona?
Ukiweka tofauti za kibinadamu Magufuli alikua kiongozi Bora kuliko Mama Samia.... Moja ya sifa kuu ya Kiongozi ni kuweza kufanya maamuzi na kuya simamia hata kama wengine hawakuelewi... The late President Magufuli alipinga chanjo hata wakati wa mwisho wa uhai wake japokua Dunia nzima ilimdhihaki.... Sisemi alikua sahihi au laa lakini naonyesha namna gani alivyokua tayari kulipa gharama ya kile anachokiamini kua ni Bora kwa niaba ya watu wake.... Sikua nikimpenda lakini Kuna vitu kafanya he must be credited for
 
Tutakuwa na Rais Samia kwa kipindi cha miaka takriban mitano kabla ya Uchaguzi Mkuu kama mambo yakienda hivi bila Mungu kufanya yake. Inshallah naomba asifanye.

Kama nikiulizwa leo hii je unauonaje Utawala wa Samia?
Je, kwa jinsi Samia anavyoongoza unaona ni vema Magufuli angekuwepo?
Unajua katika Maisha huwa kuna wakati huwa tunawakumbuka Marehemu kwa uwezo wao na nafasi zao katika jamii kuanzia ngazi ya familia.

Jibu langu katika maswali hayo ni moja tu.

Ni afadhari mara mia Samia abaki miaka 10 kuliko Miaka mitano ya Magufuli.

Samia na Magufuli ni mbingu na ardhi.

Samia ana utu,ana hofu ya Mungu,hana kiburi,hana dharau,hana chuki,hana visasi,msikivu,hana roho mbaya,ana nidhamu,sio mkatili,ana heshima,ana heshimu wataalamu,viongozi wa dini,wazee na vijana.

Samia mtoto wa mjini hana mambo ya kishamba.

Anaeheshimu wakulima ,wafanyakazi na wafanyabiashara.

Hawazi kupoteza watu,
Ana huruma,hawezi kufurahia kuona mtoto wa mtu akipotezwa kwa sababu ya tofauti za kisiasa.

Hata ukiangalia body language za watu mitaani,Wana amani Sana.

Hana hotuba za vitisho wala dharau.
Ana vijimaneneo vyake tu vya kipwani,au kimamamama lakini sio sio maneno makali.

Kitu pekee kitamharibia Samia kama asipocheza karata zake vizuri ni Kesi ya Mwamba Mbowe tu.

Vyovyote itakavyokua Samia Sio Mkatili.
Hawezi kuruhusu au kufurahia mambo kama yaliyompata Lisu yatokee ndani ya awamu yake,

Hawezi kupanua barabara na asiwalipe wahanga.

Ukweli ni kwamba Kwangu mimi ni bora Samia kuliko Jiwe.

Nchi ilikokuwa inaelekea Ni Mungu tu ndio ajuaye.

Hivi kw mfano mambo haya ya kuogofya na kutisha aliyokuwa akiyafanya Sabaya Intelijensia za akina Sirro hazikuyaona?
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa
 
Madam President ni tofauti mno na JPM, kwa hulka, haiba na hata tabia binafsi. Ni kiongozi msikivu na mwenye kuchagua maneno ya kuongea na kuchunga mno kauli zake pale anapoongea hadharani, tofauti na mtangulizi wake.

Ana jambo moja tu muhimu analipaswa kulifanya kwa sasa, asirithi maadui wa kisiasa wa mtangulizi wake, bali atafute suluhu nao kwa mustakabali mpana na bora wa nchi yetu.
Tayari amesha haribikiwa
 
Ndugu yangu unataka kuniambia wakati wa Magufuli ufisadi uliisha?haukuwepo.
Sasa Makonda alivusha makontena Bandarini,
Ndugai alitibiwa India kwa Mabilioni n.k
Hivi ni nini kilichomfukuzisha CAG Assad?
Hawa akina Sabaya je walikua ni Mafisadi,majambazi au wanyaNg'anyi?
Kwa taarifavyako Hawa dizainj ya akina Sabaya wapo wengi Sana na wote walikua awamu ya Magu.
Ndio kwa mara ya kwanza Mkuu wa Wilaya anashitakiwa kwa ujambazi alikua analindwa na Magu hii haijawahi tokea enzi za Nyerere,Mwinyi,Mkapa wala Kikwete.
Uongozi wa Magu tumeshuhudia kiongozi wa Upinzani akishambuliwa na hakuna Kesi,Mbunge alipigwa risasi hakuna Kesi .sio chuki ni nini?
Wagombea wa Upinzani wamepigwa hadharani ni wengine kutekwa wananyang'nganywa fomu na kukataliwa kuwa wamekosea au wamechelewa kurudisha fomu.
Utawala wa hovyo kabisa .
Angalia Tukio la Akwilina,angalia Uchaguzi wa serikali za mitaa hovyo kabisa .mambo ni mengi sana.upendeleo wa wazi kabisa amedhulumu hata haki za watu kwenda mahakamani. Kudai fidia za maeneo waliyovunjiwa huku Mkoa mwingine akisema wasivunjiwe .raisi gani huyo?
Kwangu zote ni awamu mbaya sn hakuna yenye unafuu
 
AAcha wale,hii nchi ukijifanya kiongozi mzalendo utatukanwa na kuuawa,ni bora kuiba na kupiga tu pale unapopata nafasi ,watoto wako na vizazi vyako viishi kwA amani na ukwasi🤣
NaWenzako wameanza kuruka we piga tararira tu JF. Week ijayo wanaenda Glasgow kwenye environmental summit na posho kibao.

Watabebana wizara ya nishati, TPDC, TANESCO, wizara ya mazingira, NEMC na kila taasisi yenye vinasaba na huo mkutano huko Glasgow ‘mama oyee’.

Si ndio nchi mnayoitaka.
 
Swadaktaaaa! Jiwe was an animal.
Dah....tatizo mnasahau sana.....mnapotafuta uongozi mnaupata kwa kutumia nguvu za wengi (wapigakura).....sehemu kubwa ya hao wengi ndiyo hao "wanyonge" Sasa Kuna tatizo gani ukiongoza kwa kutetea wanyonge? Kazi kuu ya kiongozi wa umma Ni kulinda rasilimali za nchi na kuhakikisha zinamfaidisha kila mwananchi kwa mgao sahihi. Sasa kwa mfano Mheshimiwa Rais Samia ana uhakika Waziri wa nishati Kuna sehemu amepiga....Kuna tatizo akiwauliza wananchi (umma) kwenye hadhara kama amtumbue au asimtumbue Waziri?
Tusidanganyane.....Rais makini kazi yake kuu ni kutetea wanyonge wasinyanyaswe na wateule wake Wala wafanyabiashara wakubwa..... 🤣🤣🤣🤣🤣🤭
 
Back
Top Bottom