SoC02 Kama ni kweli tunataka kushirikiana na Wananchi wanyonge kujiletea maendeleo basi yafanyike haya!

Stories of Change - 2022 Competition

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Kwanza nisema huwezi kuunganisha nguvu ya Tajiri na Mtu mnyonge maskini zikawa kitu kimoja, Simba yenyewe pamoja na kwamba Ina Mashabiki wengi na wanachama Bado inajiita Nguvu Moja!! (Hapa nimetania tu😆).

Jana wakati mheshimiwa waziri wa Fedha anatetea Tozo alisema mambo mengi sana lakini Mimi nilichukua mawili tu kwakuwa Kuna sehemu nilikua nawahi!

Kwanza alisema Tozo inayoendelea ni wanachi wenyewe ndio walioomba! Katika hili nilikumbuka Mheshimiwa zungu ndie alitoa hoja bungeni na kwakuwa ni mbunge tuseme alitumwa na wanachi wake wa Dar aseme vile vile alivyosema vinginevyo tuseme walioomba tozo ni Wananchi. (Yaani wananchi kama Yanga hivi 😆😆😆 hapa pia nimetania).

Lakini jambo la pili ambalo mheshimiwa Mwigulu alisema ni kuwa Tozo hizi zinamaanisha kuunganisha nguvu ya pamoja kama nchi Ili kujiletea Maendeleo! Kwa hili likanifanya kuleta tafakuri na maoni Yangu kwakuwa Sina uwezo wa kufika ofisini kwake ila alisema tuweke maoni yetu popote watayasoma uzuri ni kwamba yeye ni mtumiaji na verified kabisa wa JamiiForums! Na hivyo napendekeza yafuatayo:

Kwanza mishahara ya mawaziri ikatwe angalua laki Mbili Kila mmoja na laki Moja na Nusu Kwa manaibu mawaziri Kwa kipindi chote hiki Cha mkwamo.

Kwa idadi hii ya mawaziri na manaibu waziri Kwa mwaka hatuwezi kukosa milioni 70 au 80.

Lakini pia posho za wabunge ambao Ndio waliotunga hii sera ipunguzwe laki Moja badala ya laki 3 wapewe laki Mbili Kwa Idadi ya wabunge 360 tutakuwa tumeokoa shilingi million 36.

Pesa ambayo inaweza kujenga chumba Cha Darasa na ofisi ! Hapo ni kikao kimoja tu! Vipi kama mkutano mmoja wa bunge? Ni pesa nyingi inaweza kusaidia kabisa!
Tukitoka hapo Kuna wakuu wa idara na taasisi za juu wizarani na taaisi za Uma kama TRA, NBS, TPA n.k Hao nao watoe elf 50 Kila mmoja hatukosi milioni 30-50 Kwa mwezi!

Jambo lingine la Pili lingeweza kuonyesha ushirikiano na kuunganisha nguvu ya pamoja ni kupitia huduma za afya na huduma za elimu.

Waheshimiwa wakiumwa au kuugua Basi watibiwe hospitali hizi zetu nao wapange foleni kama sisi! Huwezi kusema unaunganisha Nguvu lakini mmoja anatibiwa muhimbili na mwingine atibiwe jarkata Indonesia Kwa ugonjwa Huo Huo!

Lakini pia viongozi Wote wa serikali watoto wao walazimishwe kusoma shule za serikali!
Hii itaonyesha umoja na Ile Nguvu ya pamoja ambayo mheshimiwa Mwigulu anaisema! Itaonyesha Kweli viongozi na wanachi la kwao Moja!

Jambo la mwisho ni kupunguza matumizi yasiyo na lazima Kwa viongozi,

Hakika tukifanya hayo tutaonyesha umoja na nguvu ya Pamoja!

Vinginevyo zilongwa Mbali zitendwa Mbali!
 
Back
Top Bottom