Kama Rais wa wanyonge alishindwa kumaliza shida za wanyonge, Katibu wa Itikadi ataweza? Huu ni mzaha

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,033
Tanzania mwaka 2015 tulitangaziwa kama imempata RAIS wa WANYONGE Rais ambaye yupo karibu na Wananchi RAIS ambaye yupo kwa ajili ya Wanyonge Rais ambaye alitangaza atahakikisha Wanyonge wanaishi KITAJIRI na Matajiri wanaishi KISHETANI Pamoja na AHADI hizo bado ALISHINDWA kutatua SHIDA za WANYONGE wa Nchi hii.

SIASA aanazozifanya MAKONDA ni SIASA Alizokuwa anazifanya RAIS MAGUFULI siasa za VITISHO NA KUDHALILISHANA mbele ya WANANCHI kwa Kigezo cha KUTATUA SHIDA ZAO. Siasa hizi ZILIMJENGEA CHUKI MBAYA Rais MAGUFULI kwa VIONGOZI wenzake.

Siasa hizi Hazikutatua SHIDA za Wananchi kwani CCM imewatengenezea SHIDA na MIGOGORO mingi sana Wananchi ktk Miaka 60 ya Utawala wake.Kutokana na Shida na Migogoro kuwa Mingi imewawia VIGUMU SANA CCM kuitatua na Kuimaliza ndio maana SHIDA za Wananchi HAZIISHI.

ANACHOKIFANYA Makonda ni USANII TU wa KISIASA wananchi Wamshangilie kama Walivyokuwa Wanamshangilia RAIS Magufuli lakini SHIDA ZAO zinaendelea kuwa Pale pale.

SHIDA za Wananchi ni MTAJI TOSHA wa CCM ktk UCHAGUZI MKUU wananchi Wanadanganywa kuwa Shida zao zinatatuliwa ili wawe na imani na CCM lakini baada ya UCHAGUZI Shida zao zinaendelea kuwa PALE PALE.

Kutokana na WINGI wa Shida na Matatizo ya WANANCHI CCM hata ikiwatawanya kina MAKONDA 100 Nchi zima HAWATATATUA SHIDA na MIGOGORO iliyopo ya WANANCHI.

SHIDA na MIGOGORO ya WANANCHI uwepo wake ni TURUFU kwa CCM.
 
Back
Top Bottom