Believe me, kumiliki cheti feki kunapunguza kujiamini sehemu yeyote ya kazi hata kama una cheo gani.
Confidence alivyokuwa nayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aka Bashite, imeanza kupungua tangu kuibuliwa kwa sakata la yeye kumiliki vyeti feki.
Ni ajabu sana operation muhimu kama hili ya kupiga marufuku matumizi ya viroba kuanza bila kusikia tamko lolote kutoka kwa mwenye mkoa wake.
Awali alikuwa mstari wa mbele kuandaa press conference kutoa matamko kwa mambo mengine yasiyokuwa na maana kama, kutolala gesti mchana, kupaka rangi nyumba zote mkoani kwake, kuorodhesha wageni wanaoingia Dar, ila kwa hili lililo na uzito karibu sawa na madawa ya kulevya yuko kimya kigugumizi hiki kimeanza lini, tatizo cheti, pole sana Bashite.
Nimeamini kweli dunia duara, enzi zile wewe ndio ulikuwa ukiwaita waandishi wa habari, leo waandishi wanakuita wewe lakini hutokei.
Conclusion:
Kuwa na vyeti halisi raha sana (CONFIDENCE).