Kama ni kweli na ushahidi upo....

Kama ni kweli na ushahidi upo....

Say what?

Kabisa unaona sawa kuwa na rais ambaye ni wife beater?
Si malaika na binafsi siwezi kumhukumu kwa mambo binafsi ya familia yake, ilimradi sijasikia mkewe akilalamika inawezekana anaona kupigwa kama sehemu ya kupendwa zaidi.
 
Ahahahaaa....kwa hiyo kumbe huyo Gwajima naye hakuuonyesha huo ushahidi anaodai anao.

Hivyo hatuwezi hata kujua kama kwamba [1] anao kweli na [2] ni ushahidi unaotosha na kuridhisha.

Hivyo hata yeye anaweza akawa anazusha tu ili kupoteza kabisa lengo na kuzua mparaganyiko tu.

Nilimsikia anasema eti hataki kumpeleka polisi and kwamba atakuja onyesha vyeti vyake j2 ijayo sijui, some BS like that I presume, nilimsikia tu juu juu, sikukariri. Yule pastor na waumini wake me nawaona wote makanjanja tu. Nipo na Makonda.
 
How can you trust, they are FAKE VYETI in the first place wakati hata vyeti vyenyewe hatujaviona - aliyeibiwa JINA na Vyeti hajazungumza chochote kama yupo - Tushaanza kuamini tu kwasababu Mange kasema
Sorry Boss, in this context they are not real fake certificates but not his!! And mind that it's not me who is accusing him .... I was only contributing!!!
 
Ukiona hvyo ujue ukweli bado haupo mezani lakn mkuu alisema anampa cku chache vingnevyo atatoa vyeti itakuwa mkuu wetu anasubili watoe vyao afu yy atoe halisi kesi irud kwao kwa kuwa na vyeti feki wawe makin
 
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?


Mkuu nadhani unakumbuka ishu ya Obama kuhusu Je alizaliwa marekani au hakuzaliwa marekani...ikishikiwa bango kweli kweli na sidhani kama kuna mmarekani alienda mahakamani kuhoji kama Obama alizaliwa marekani au la..wewe unaweza kutujuza kwani upo huko.

Mwanzoni Obama alipuuza na kuendelea kuchapa Kazi kama kawaida. Ila maneno yalipozidi nadhani washauri wake walimshauri atoke aonyeshe cheti chake cha kuzaliwa naye anafanya hvo..na kwa kiasi akawa kamaliza minong'ono...kasema kwa kiasi kwani kuna wengine waliendelea kusema Obama hakuzaliwa marekani.

Sasa mkuu huyu RC Wetu katuhumiwa Kununua cheti cha form four...kwa nn asiweke hadharani kuanza cheti chake cha kuzaliwa mpaka hicho cha form four ili amalize hii sintifahamu na aendelee na Kazi zake kama kawaida???

Kama rais wa taifa kubwa duniani aliweka hadharani cheti chake cha kuzaliwa ili kumaliza sintofahamu..nn kinamshinda huyu rais wa mkoa wa watu milioni 8??
 
Nimeanza kupata picha kwamba viongozi wengi hawana washauri wazuri. Wanafikiri wakishakuwa na vyeo vya kimamlaka, basi automatically wanakuwa wajuzi wa mambo ya katika masuala ya utawala au siasa. Wrong! utawala au siasa ni sayansi kama zilivyo chemisty na biology, you need strong minds to guide you through, na hasa inapotokea misukosuko kama hii.
 
Huyu Makonda ameni surprise sana,I never knew in Tanzania mtu unaweza kuunga unga elimu na ukafika-No wonder anaelewana sana na le mutuz,cause jamaa naye kaunga unga elimu baada ya kupata zero standard 8 or was it form four
 
Aonyeshe vyeti ili iweje?

Kwa amri ya nani?

Na akionyesha mtakubali au mtahamisha magoli na kudai hivyo alivyovionyesha navyo ni feki?

Hii nchi bana....
Tulikuwa tunajidili na jamaa zangu kwamba nchi za Afrika zinakuwa maskini kwa sababu watu wengi ni wajinga haijalishi wamefika form six au university maana ni watu wa kufuata upepo tu
 
Makondakta analaana za yule Babu alifariki kwa maneno yake yakumdhalilisha ....lazima laaana hiyo itamuumizaa
 
Nimependa hiyo slogan yako ya pili hapo chini. Jana nilikuwa mahakamani (mimi si "msomi" kama wanavyoitana wao), ila kilichonishangaza ni kuona mawakili (vijana wa kike na wa kiume, wao wanaitwa "juniors") wakijadiliana issue ya Makonda kwa kufanya reference kwa Mange...eti si unaona Mange kaandika! Hata Gwajima naye kasema kanisani!

Nikajiuliza sana kama wasomi wetu ndiyo hawa, ambavyo kwa uelewa wangu, tuna mamlaka kama NECTA, NACTE au TCU, ambao ndiyo wenye kuthibtisha madai hayo, kwa nini basi madai dhidi ya Makonda yasipelekwe huko? Maana hata kubadili majina sheria inaruhusu. Sasa accusers wake sijui kwa nini wako kwenye limbo kufanya yale ambayo tunadhani ni sahihi
Waafrika wangu ni wajinga ndo maana tukatawaliwa,now maana hata baada ya uhuru tungali maskini ukitoa nchi ambazo zilitawaliwa na wazungu mda mrefu!!
 
Mkuu Nyani Ngabu,mfumo wa kisheria wa nchi yetu ya Tanzania hauruhusu mtu binafsi kumfungulia mwingine,na kuendesha kesi mahakamani,kesi ya jinai. Kinachotakiwa ni kwa mtu mwenye ushahidi dhidi ya jinai ya mwingine kuuwasilisha ushahidi huo kwa mamlaka zinazohusika,mfano polisi au TAKUKURU,ili hatua stahiki zichukukiwe. Mamlaka hizo na nyinginezo,kama Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ndizo zitakazomshtaki mhusika. Ndiyo kusema,wenye kuamua kushtaki au la ni watawala waliopo kwenye mamlaka hizo iwe ushahidi umekabidhiwa au ule walionao wenyewe.


Heri yenu nyie akina BigBro na Nyani Ngabu mmeishia form four. Mwenzenu miye niliambulia kile cheti wanachoita "leaving certificate" nadhani mnaelewa yaliyonikuta.

Mkuu Petro E. Mselewa kwa ujinga wangu tu, na mimi naungana na wakuu hapo juu, kwanini aliye na ushahidi hata asiupeleke kwa mamlaka husika ili huyo anayetuhumiwa aburuzwe mahakamani?
 
Mimi nimeishia form four A haaa haaaa.

Kwakuwa nimeishia form four nadhani makosa ya jinai yanapaswa kuwa handled na serekali kupitia taasisi zake DCI au DPP.Hivyo wewe kama raia huna nafasi ya kumshtaki Bashite nafasi uliyonayo ni kumzodoa tuu na si vinginevyo.Mfano kama umeshiriki kutoa uhai wa mwanao mkeo atakuwa shahidi wa jamhuri (DPP) mwenye kesi au atakayekushtaki atakuwa mkurugenzi wa mashtaka.

Una nafasi ya kumshtaki Bashite katika makosa ya civil eg kesi ya madai ya kuchafuliwa jina ambayo nadhani bado kidogo tu zitaanza kunguruma katika mahakama zetu tukufu.


Mkuu Ngongo hata huko kumzodoazodoa mitandaoni inabidi uwe macho maana kale ka sheria kalikosainiwa haraka sana, kana meno sana aisee.
 
Kama kasingiziwa basi aje na uthibitisho kuwa kasingiziwa

Mambo ya "who alleges must prove" hiyo ni kanuni ya mahakamani lakini siyo katika uwanda wa siasa!.

Umma ukianza kukutuhumu, siyo suala la kusubiri mahakama ikusafishe, bali ni wewe kuja clean ili kulinda imani ya umma kwako!, kwa kuwa wewe ni mtumishi wa umma!

Otherwise kukaa kimya ni "Tacitly accepting the allegations".

Huwezi kuwa Mtumishi wa ofisi kubwa ya Umma ukaacha kujibu tuhuma nzito dhidi yako , maana umma unapoteza confidence kwako kitu ambacho kiuongozi hakikubaliki!
 
Makonda hango'ki kwann mnakua na roho mbaya hivyo kwan yeye ni kwa kwanza kutumia vyeti vya wengine nendeni kwa Mwifoot, Kigwengele, nyie veep kwani hiyo veep vip
 
Back
Top Bottom