Kama ni kweli na ushahidi upo....

Kama ni kweli na ushahidi upo....

He/she who alleges must prove.

Allegations don't just prove themselves.

So did I miss the memo or something?
Tutazodoa tu, na akikasirika yeye akafungue kesi ya kuchafuliwa jina. Hapo ndipo tutakapotoa ushahidi tulionao ili kuthibitisha kuwa hatumsingizii.
 
Mke wa makonda huyu January 2016 anajiita mama daudi na hana mtoto...ushahidi upo NECTA...sie tunapiga kelele haki itendeke
 

Attachments

  • Screenshot_2017-02-28-07-12-51.png
    Screenshot_2017-02-28-07-12-51.png
    435.5 KB · Views: 30
Wakwetu, mpaka sasa mlalamikaji hajulikani ni nani. Inawezekana hawampeleki mahakamani kwa vile hakuna anayefaidika au watu wanasubiri waone action za Mkuu kwa vile toka aingie alitangaza kuwashughulikia wenye vyeti fake!!

Anyway, kuna mahali nimeuliza, hivi kweli hakuna mwanachama wa JF kutoka Koromije?

Hivi kweli hakuna vijana waliosoma naye Pamba Secondary ambao ni wanachama wa JF!!?

Bahati nzuri Gwajima wanatoka kijiji kimoja ila hawakuwa wanafahamiana. Sasa tusubiri huo ushahidi wa Gwajima tuone kama ni kweli ............ tatizo hakutoa time frame ya lini atautoa kama hataombwa msamaha au kama Mh. hatawajibishwa!!
Nina imani wapo, lakini wanaogopa kushughulikiwa kwa nguvu ya dola.
Serekali ina mkono mrefu, na kabla haujasaidiwa na sheria, unaweza kujikuta umeshasota ndani nusu mwaka kama Lema
 
Oh wow!

Shukrani katheeran Bw. Wakili 'Msomi'.

Umenifunza jipya leo.

Sasa swali kwako, je kwa ufahamu wako, hao wanaodai kuwa wanao ushahidi kuwa Paul Makonda anaitwa Daudi Bashite wameshawasilisha huo ushahidi wao kwenye mamlaka husika?
Ushahidi watawasilisha mahakamani ikkiwa wataitwa kuwa mashahidi wa upande wa Jamhuri.
 
Hapo niki imagine nitakuwa nabashiri, kudhani, na kuhisi tu.

Sitaki kufanya hivyo na ndo maana naomba wote wanaodai Paul Makonda si jina lake wanipe ushahidi ili niridhike halafu nianze kumshukia na yeye.
Achana naye huyo Makonda.
Kwani lazima umshukie?
Nina hakika unayo mengi ya kufanya zaidi ya kuhangaika kulazimisha watu wamshitaki Makonda.
Au unajitahidi kumsafisha kinyumenyume?
 
"unabisha nini wakati Mange ametuambia"

MsemajiUkweli hapo ulinena kaka!
Kaka;
Huyo mwanamama ni dummy god kule Instagram!

Sikuwahi kuamini kama Joseph Kibwetere aliwahi kuwaaminisha na kuwafanya watu wakajichoma moto ili waende ''mbinguni'' lakini kinachoendelea kule Instagram nimeanza kuamini kuna uwezekano hata Tanzania kuna watanzania wenye akili na fikra zinazofanana na wafuasi wa Kibwetere.

Huyu dummy god anaweza kuwaambia wafuasi wake ambao ndani yake kuna wahitimu wa UNI wavue nguo na kutembea uchi na watavua nguo na kutembea uchi.

Hakuna umasikini mbaya duniani kama umasikini wa fikra.
 
Wanaotafutwa kazini ni kuomba kazi kwa vyeti feki. Mkuu wa mkoa hateuliwi kwa cheti. Na hata hivyo ingekuwa vizuri wenye vithibitisho watuwekee mtandaoni living certificate ya Paul na ya Daudi lazima zitakuwa na picha tuwajue ni kina nani hao.
Naelewa hili, suala si ukuu wa mkoa, ni kuwa na watumishi waliofoji vyeti.

Sijui mwakilishi wa Rais anasimama wapi, sina uhakika!
Lakini kubwa zaidi ambalo nimeliongelea ni la kisiasa

Huwezi kusema una kampeni ya kuzuia kughushi ukafumbia macho jambo lile lile kwa kisingizio cha uteuzi. Hilo tu linaondoa public trust ikizingatiwa kuwa yeye ni mwakilishi wa Rais na zoezi hilo linamgusa kama kiongozi wa mkoa

Kama hatajisafisha, atasimamia vipi sheria na maagizo ya Rais akiwa hana public trust?
 
Lazima tufike hadi mahakamani?? Yeye ni Mtumishi wa umma tuhuma zipo mezani...ajitokezi na vyeti halali afute tuhuma hizi....very simple na maisha yaendelee...!!
Huyu wanalazimisha kumwita msafi
How can you trust, they are FAKE VYETI in the first place wakati hata vyeti vyenyewe hatujaviona - aliyeibiwa JINA na Vyeti hajazungumza chochote kama yupo - Tushaanza kuamini tu kwasababu Mange kasema
Unadhani aliibiwa jina na vyeti au aliuza?
Kama aliuza, unategemea atajitokeza kwa namna yoyote katika sakata hili?
 
Mke wa makonda huyu January 2016 anajiita mama daudi na hana mtoto...ushahidi upo NECTA...sie tunapiga kelele haki itendeke
hii nayo una izungumziaje bwana Ngabu???
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
 
Achana naye huyo Makonda.
Kwani lazima umshukie?
Nina hakika unayo mengi ya kufanya zaidi ya kuhangaika kulazimisha watu wamshitaki Makonda.
Au unajitahidi kumsafisha kinyumenyume?
Unasema niachane na Makonda kwani mimi ndo nimemganda?

Kwanza we mwenyewe mbona umeshindwa kuachana na mimi hapa?
 
Ndugu Nyani Ngabu kinachonisikitisha ni kwanini mnawalaumu hawa "walalamikaji" wa kwenye media badala ya kuwalaumu mamlaka husika polisi na vyombo vingine kwa kukaa kimya na kutokufanya uchunguzi na kuja kuclear doubt au wamuombe Makonda mwenyewe aje afanye clearance kama si kweli:
Hili ni kosa la jinai (uhalifu) kuwa umefanyika kwanini polisi wapo kimya.

I wonder why police need to be moved to take action on this. Tumeona hata practice polisi wetu si lazima wamuvuzishwe popote pale wanapoona pana harufu ya uhalifu huingia hata bila kuambiwa iweje sasa this criminal offense is alleged to be done nao wapo kimya?

Polisi utendaji wao ni tofauti na mahakama tumezoea mahakama wanamsemo kwamba "the court is not your mother cannot give you what you didn't ask" kwamba mahakama ni lazima imuvuzishwe hata jaji akiwa amepata taarifa kuwa kuna mtu ameuawa au umezurumiwa hawezi kujihusisha na hiyo kesi mpaka imeletwa mahakamani na usipoileta shauri yako hiyo ndiyo maana ya "mahakama siyo mama yako haiwezi kukupatia usichokiomba"

Lakini kwa polisi ni tofauti akipata taarifa kuwa kuna mtu ameuawa lazima achunguze haijarishi taarifa hizo ameziona kwenye gazeti, mtandaoni au popote.

Iweje hili swala la Makonda wasubiri mtu akaripoti eti? Hizo taarifa za kiintelejensia zipo wapi?
Mbona linapokuja swala la uchochezi wanafanyia kazi taarifa za mtandaoni? Kwanini?.

Mwisho.
Hii ni kesi ya jinai polisi ndiyo wanatakiwa kuonesha interest mpaka sasa wapo kimya eti wanasubiri taarifa rasmi isipopelekewa hiyo ripoti basi mtuhumiwa aendelee kuenjoy good life in the cape of Good Hope of south Africa?

Na hao waliosimamisha ajira zote wakikagua vyeti nao wanasubiri taarifa rasmi?

Just imagine hizi tetesi zingekuwa juu ya uwepo wa magaidi wa amboni au ujambazi BOT wangebaki ofisini wakisubiri taarifa rasmi?
 
Naelewa hili, suala si ukuu wa mkoa, ni kuwa na watumishi waliofoji vyeti.

Sijui mwakilishi wa Rais anasimama wapi, sina uhakika!
Lakini kubwa zaidi ambalo nimeliongelea ni la kisiasa

Huwezi kusema una kampeni ya kuzuia kughushi ukafumbia macho jambo lile lile kwa kisingizio cha uteuzi. Hilo tu linaondoa public trust ikizingatiwa kuwa yeye ni mwakilishi wa Rais na zoezi hilo linamgusa kama kiongozi wa mkoa

Kama hatajisafisha, atasimamia vipi sheria na maagizo ya Rais akiwa hana public trust?

Ni kweli kama iko verified amefoji vyeti. Lakini kwa vile Mange ama Ngwajima kaongea ndo wote tuamini kafoji vyeti ?? wengine hatuko hivyo. Sasa kama kila katuhuma Mange anakokasema lazima katolewe maelezo itakuwa Taifa la ajabu sana.

Mie naamini tuhumu za kutolea maelezo ni zile zilizoambatana na ushahidi, kama vile living certificates za Paul na Daudi zilizo na picha. Lakini mtandaoni tu ujibu tuhuma, itakuwa uhuni uliopita kiwango.
 
Hapa Nyani Ngabu ana hoja, kuwa kughushi cheti ni kosa kisheria.
Wanaodhani alifoji wana fursa ya kumfungulia kesi kisheria kama wale wanaoghushi na kufunguliwa kesi na serikali.

''The onus is on complainant to prove guilty'' otherwise kuna presumption of innocence

Kwa upana wa suala hili, nje ya sheria lina impact kubwa sana

1. Kwamba, zoezi zima la kutafuta vyeti fake lina shaka unless uwepo ufafanuzi
2. Viongozi hawatendi wasemayo 'walk the talk'
3. Waliowajibishwa 'wameonewa' kwasababu ya double std

Hayo yote ni dhana ambayo inaweza kupata miguu kama Paul hatajitokeza ili kujitakasa au kukiri na kuwajibika. Ni suala la muda tu

Kama ulivyosema mtumiaji wa media kama yeye anapoamua kukaa kimya ni 'tacitly accepting the allegations'
Right on the money!
 
Kama kasingiziwa basi aje na uthibitisho kuwa kasingiziwa

Mambo ya "who alleges must prove" hiyo ni kanuni ya mahakamani lakini siyo katika uwanda wa siasa!.

Umma ukianza kukutuhumu, siyo suala la kusubiri mahakama ikusafishe, bali ni wewe kuja clean ili kulinda imani ya umma kwako!, kwa kuwa wewe ni mtumishi wa umma!

Otherwise kukaa kimya ni "Tacitly accepting the allegations".

Huwezi kuwa Mtumishi wa ofisi kubwa ya Umma ukaacha kujibu tuhuma nzito dhidi yako , maana umma unapoteza confidence kwako kitu ambacho kiuongozi hakikubaliki!
Kwa hiyo unakubali hapa kikubwa kilichopo ni siasa tu, siyo?
 
Back
Top Bottom