Kama ni kweli na ushahidi upo....

Kama ni kweli na ushahidi upo....

Nilikwambia tangu mwanzo unachofanya si hoja bali unatetea ukabisha sasa unaweza kujipima na kujiona kama bado uko kwenye kutoa hoja au kutetea labda uniambie hujui neon kutetea

Kuna sehemu hata moja niliposema kuwa hizo tuhuma dhidi ya Makonda ni za uongo?
 
Mkuu Nyani Ngabu,mfumo wa kisheria wa nchi yetu ya Tanzania hauruhusu mtu binafsi kumfungulia mwingine,na kuendesha kesi mahakamani,kesi ya jinai. Kinachotakiwa ni kwa mtu mwenye ushahidi dhidi ya jinai ya mwingine kuuwasilisha ushahidi huo kwa mamlaka zinazohusika,mfano polisi au TAKUKURU,ili hatua stahiki zichukukiwe. Mamlaka hizo na nyinginezo,kama Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ndizo zitakazomshtaki mhusika. Ndiyo kusema,wenye kuamua kushtaki au la ni watawala waliopo kwenye mamlaka hizo iwe ushahidi umekabidhiwa au ule walionao wenyewe.
Ckuwa nkilifahamu ili,ahsante kwa elimu.
 
Even vita yake ya Madawa ya kulevya ni Political driven,for whose advantege,Bashite ndiye anajua.
Mbowe ameonesha Mfano kwa kujitetea na kugungua kesi.
Now wamemgeuzia Kibao,its up to him to Clean himself.
Kwani inachukua muda kuja na vyeti vyake na kumaliza mchezo

Mbowe naye alituhumiwa hana cheti lakini bado hajapata kukionesha pia.
 
Unafiki umewajaa hawana jengne na yule.mtu.mfupi mzandk anayefufua watu nahtaj ajifufue mwenyew
 
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
Moja kati wa wabeba box wenye akili kubwaz,lakini haizid ya Le mutuz!
 
Nafikiri ni kwa vile linamhusu mtu wa daraja fulani, na inaonekana wazi nchi hii ni kama vile tumeshayakubali madaraja ya watu. Kwenye madaraja mengine, watu wakitaja taja tu kwamba una vyeti feki, mamlaka zote zinafanya kazi in tandem kukufichua haraka na kukutimua kazi. Ndivyo jamaa mmoja ninayemfahamu alivyopoteza kazi yake mwaka jana. Mbona watu walitaja tu akina fulani wanaweza kuwa wanatumia madawa ya kulevya, na mamlaka zinazohusika zikawaita, kuwahoji, kuwapima na kuwapekua majumbani kwao??? Where is our common sense??
 
A private prosecution is a criminalproceeding initiated by an individual or private organisation (such as aprosecution association) instead of by a public prosecutor who represents thestate. Private prosecutions are allowed in many jurisdictions under common law, but have become less frequent in modern times as most prosecutions are now handled by professional public prosecutors instead of private individuals who retain (or are themselves) barristers.
 
Mkuu, tuhuma dhidi ya Makonda Zipo wazi Sana, na mwenye jukumu la Kumshtaki Makonda si mtu aliyemtuhumu Bali ni mwajiri, aliyemtuhumu amedai anao ushahidi wa kutosha na yupo tayari kuisaidia mahakama.
Sasa hapo mwenye kuchukua hatua ni bosi wake tu na si vinginevyo.
kwani umesahau Makonda alivyowatuhumu watu kuuza wakati akijua kuwa, "A person cannot be made guilty if not proven by the court of law ",Sasa Makonda aliwataja publicly kitendo ambacho ni kuchafua image ya mtu, nadhani unajua kuwa, what goes around comes around ,alianzisha ugomvi wa mawe akasahau kuwa anaishi kwenye nyumba ya vioo, ugomvi umeanza akakimbilia kujificha humo humo.
Watu wenye akili Zetu tuliuona mwisho mbaya Makonda, if his boss won't fire him, his personality and political charisma in the state house will totally get faded.
Hilo haliwezi kufanyika , kwanini waleta tuhuma hawakuzileta mapema kabla ya vita ya dawa za kulevya kuanza?
 
Nimeshasema wazi kabisa kuwa hapo alichemka big time.

So what's your point?
Point yangu ni hii; Mara nyingi tumeona serikali au viongozi wa serikali wakijibu tuhuma dhidi ya serikali au dhidi ya viongozi binafsi zilizotolewa mitandaoni kama hii. Rejea issue ya mshahara wa Rais ilikanushwa tukaahidiwa ushahidi wa salary slip ingawaje hadi Leo kimya. Sasa hii imeshindikana nini mtu kujitokeza na kusema "Mimi sijajawahi kuitwa Daudi tangu kuzaliwa Mimi ni Paulo na ushahidi ni huu hapa. Mfano wa pili; Kama hawafanyii Kazi habari za mitandaoni, yuko wapi Dr.Posi aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa na naibu WAZIRI? Umesahau kilichofanyika alipoteuliwa Bulembo na kugundulika kuwa Katiba imenajisiwa kwa kuzidisha wabunge wa kiume? Kelele zilitokea Ikulu, Bungeni au mitandaoni?
 
Ushahidi ni kwamba hajakanusha has a kwa kuzingatia yeye ni msemaji mahiri na chombo chake cha kusemea clouds kipo angeshasema neno tu tena kwa tambo za kufa mtu.

Suala LA pili ni kwa bahati mbaya Tanzania jinai inapelekwa mahakamani kupitia polisi, japokuwa kwenye penal code kuna kifungu cha 87 kama sijasahau kinamruhusu raia kwenda moja kwa moja Ku lodge shauri LA jinai mahakamani ila kwa sasa sio effective kutokana na mazoea ya kupitia polisi.

Polisi wenyewe ndio hawa hawa tulio nao unadhani ukatia pua kufungua ya bashite utasalimika?!
Huo ni uoga tu,kama ushahidi upo upeleke, vinginevyo utakua hajasaidia umma
 
Hili ni kosa la jinai, Jamhuri ndiyo inaendesha kesi chini ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP). Mtu mwingine yeyote mwenye ushahidi anaweza kwenda polisi kuripoti au kulalamika hivyo litakuwa jukumu la Jamhuri kuchunguza na kufungua kesi. Kuna tofauti kati ya kwenda kulalamika na kwenda kufungua kesi. Watu huenda kulalamika polisi, na kesi hufunguliwa mahakamani.

Chukulia mfano umeshuhudia mama yako akiuawa na x kwa kuwa ni kosa la jinai unachotakiwa ni kwenda polisi kuripoti au kulalamika wao polisi (Jamhuri) watapeleleza na wakiona kuna ushahidi watakwenda wao kufungua kesi mahakamani na wewe uliyeripoti utaitwa kama shahidi.

Kwenye kesi za madai mfano ulimkopesha mtu pesa hajakulipa, au kuna mtu amevunja mkataba wenu hapo ndiyo unaweza kama individual kwenda mahakamani kufungua kesi.
Hii ishu ya Makonda yeyote yule anaweza kwenda polisi kuripoti ili wajue na wafanye uchunguzi na wao polisi wakijiridhisha kuwa kuna kesi basi watapeleka mahakamani. Lakini lengo la kwenda kulalamika ni ili polisi wajue wafuatilie hivyo basi kwa ishu kama hii inayosemwa kila mahali sidhani kama kuna haja ya polisi kusubiri mtu akaripoti ndiyo waanze kufuatilia hili ni kosa la jinai. Je uvumi huu ungekuwa unahusu magaidi waliojificha kwenye mlima fulani wangesubiri mtu aende kuripoti?

Polisi wafanye kazi zao mbona kesi za uchochezi wakiona tu habari kwenye gazeti wanakwita na kukushitaki? Hii ishu inaandikwa kila mahali why not this?

Mwisho kuhusu kupeleka kesi kwa maslahi ya umma, hii siyo kesi inayoweza kupelekwa mahakamani kwa maslahi ya umma na mwananchi, zipo kesi za haki za binadamu ambazo zinagusa haki za binadamu za watu walio wengi rejea kesi ya kikatiba ya mtikila vs AG.
 
Wa Tanzania wengi ni bendera fuata upepo


Mangi kasema ,gwajima kasema ,nanihi kasema

Mtanzania unaweza kumchezea na kumshika akili ,mpe gossips tu utamhamisha kwenye agenda

Hii inaumiza sana...
 
Point yangu ni hii; Mara nyingi tumeona serikali au viongozi wa serikali wakijibu tuhuma dhidi ya serikali au dhidi ya viongozi binafsi zilizotolewa mitandaoni kama hii. Rejea issue ya mshahara wa Rais ilikanushwa tukaahidiwa ushahidi wa salary slip ingawaje hadi Leo kimya. Sasa hii imeshindikana nini mtu kujitokeza na kusema "Mimi sijajawahi kuitwa Daudi tangu kuzaliwa Mimi ni Paulo na ushahidi ni huu hapa. Mfano wa pili; Kama hawafanyii Kazi habari za mitandaoni, yuko wapi Dr.Posi aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa na naibu WAZIRI? Umesahau kilichofanyika alipoteuliwa Bulembo na kugundulika kuwa Katiba imenajisiwa kwa kuzidisha wabunge wa kiume? Kelele zilitokea Ikulu, Bungeni au mitandaoni?

Okay, ina maana kila tuhuma huwa zinajibiwa?

Zile za Magufuli kumpiga mkewe hadi kupelekea kulazwa Muhimbili nazo zilijibiwa?
 
Na yeye kwa nini asilete vyeti?

Au anaupenda huu mchezo?


Tunaichelewesha Tanzania!

Tena siyo kuleta vyeti, hata akienda kufafanua tu kwamba kinachosemwa si kweli na akaonyesha his side of story wengi tutamwamini. Akina Mbowe na akina Gwajima wangekaa kimya, kila mtu leo angeamini ni drug dealers. Kwenye haya mambo negative, you have to fight back and cleanse your name.
 
With all due respect, kuwa mbeba box siyo tatizo, tatizo ni wewe kujiingiza mzima zima na kung'ang'ania ndani ya box!.

Wanachofanya watu ni kufanya REFERENCE on related issues /decisions made wala siyo kwa sababu mange/gwajima kasema. Nikikuambia according to the late Nyerere, kuna waziri uingereza alituhumiwa kutembea na kimada na boss wake alivyokuwa infuriated (Kama ambavyo tulitegemea magu awe, kwa jinsi alivyojipambanua), akamteua mwingine bila kujibu resignation yake utasema tunafuata upepo?
Si lazima tuige ya huko Uingereza.
 
Post ya mia moja kumhusu Makonda hii leo!
Mie na hesabu tu!
 
Mbowe naye alituhumiwa hana cheti lakini bado hajapata kukionesha pia.
Kwa hiyo kama Mbowe kakataa kuonesha cheti chake ndio excuse kwa Bashite kuonesha vyeti vyake ????
 
Tena siyo kuleta vyeti, hata akienda kufafanua tu kwamba kinachosemwa si kweli na akaonyesha his side of story wengi tutamwamini. Akina Mbowe na akina Gwajima wangekaa kimya, kila mtu leo angeamini ni drug dealers. Kwenye haya mambo negative, you have to fight back and cleanse your name.

Mimi siamini kama mtaamini.

Naamini mtahamisha magoli tu.
 
Back
Top Bottom