Kama ni kweli basi CCM ni master mind na imefanikiwa!

Kwa sasa Lowasa ndio mtu maarufu Tanzania.

Wachache wanajadili hao waliopenya.

na kama angekuwa kati ya hao watano,umaarufu wake usingekuwa hivi.Wangejadiliwa walioteuliwa!
Fikiri,kama ccm wakimrudisha watavuna watu kiasi gani?Huu kama ulikuwa mpango wa makusudi huoni kama wamefanikiwa?
 
mkuu na lengo la mimi kuuweka uzi huu hapa mapema kabisa ni baada ya kuona wadau wengi wanaanza kufall in love na Lowassa out of sympath,nikaona pia hakuna anayeangalia other possibilities!Hata wahariri walioalikwa leo Azam tv nikaona nao wamejaa wazima wazima!
Mpaka sasa kikao kimeahirishwa wakati ilikuwa warejee saa 10

Dah kweli hapo ccm wanapima upepo na nguvu ya lowassa kwa wananchi kwani kipindi kile cha kutangaza nia walijua jamaa anafanya maigizo so they want to come in reality dah hapa ndo maona matumizi tiss cdhani kama wale wazee wanaweza ku push brains to the limit namna hii
 
usiwe mvivu wa kusoma,soma uzi mpaka mwisho na utafakari

Inawezekana amesoma hadi mwisho lakini tatizo liko kwenye kuelewa. Hata kama uliyoyaandika yasiwe hivyo, lakini nilitegemea mtu akisoma maelezo yako aielewe point yako.
 
na kama angekuwa kati ya hao watano,umaarufu wake usingekuwa hivi.Wangejadiliwa walioteuliwa!
Fikiri,kama ccm wakimrudisha watavuna watu kiasi gani?Huu kama ulikuwa mpango wa makusudi huoni kama wamefanikiwa?
Mawazo yako yanaonyesha hujui undani wa mchakato mzima. Ni hivi... Lowassa NEC na mkutano mkuu anapita kwa kishindo kabisa kwani huko amepandikiza watu wake wengi wa kutosha. Na akipita hapo kwenye uchaguzi kutakuwa hamna shida kwani tume ya uchaguzi ni yao. Sasa hai-make sense wafanye harakati zooote hizi kama unavyo-suggest kwani Kikwete atakuwa anajidhalilisha mwenyewe na kuonekana kama kiongozi mwoga na asiyejua mbele wala nyuma.
 
lowasa kashapotea tayari hata iweje. kwisha habari yake. ccm hawana jipya

Kwahiyo katika mtazamo wako ni kwamba CCM wangelikuwa na jipya pale tu ambapo wangelimweka Lowasa, ama una maana gani!? Na kama hiyo ndo maana yako basi pole sana lakini endapo humaanishi hivyo basi hongera sana!
 
low-hasa kutumika kugawa kula za ukawa, il CCM IPATE NAFUU YA KUSHINDA.
atagombea kupitia ACT ili kuua nguvu ya ukawa.

Mi nilidhani akifanya hivyo atapunguza nguvu ya CCM. Kwani hao wanaomuunga mkono, hilo kundi linaloambatana naye kila aendako katika mchakato huu ni la UKAWA au CCM?
 
Kwahiyo katika mtazamo wako ni kwamba CCM wangelikuwa na jipya pale tu ambapo wangelimweka Lowasa, ama una maana gani!? Na kama hiyo ndo maana yako basi pole sana lakini endapo humaanishi hivyo basi hongera sana!

wala sijamaanisha hivyo. lowasa hawezi kuwa rais wa nchi hii kwanini tuendelee kuongozwa na ccm wakati wote mafisadi. tunahitaji mabadiliko ccm tuwatoe madarakani tu
 
Inawezekana amesoma hadi mwisho lakini tatizo liko kwenye kuelewa. Hata kama uliyoyaandika yasiwe hivyo, lakini nilitegemea mtu akisoma maelezo yako aielewe point yako.

asante kwa kunielewa mkuu,wanaosoma uzi huu juu wanaweza hisi nampigia chapuo lowassa lakini kumbe ndio nawaonya wasiingie kwenye mtego wa kumpenda kwa kumwonea huruma!
 
hahaaaaa,ina maana viongozi wetu hawawezi kutengeneza draft kama hiyo?
Hivi kiongozi mtiifu kwa chama kama nchimbi ambaye alikuwa waziri,anaweza kweli toka kwenye mkutano mkuu na kukimbilia kwenye media kutoa mapungufu ya ndani ya chama?Kweli anaweza mkosea heshima JK hadharani kwa kuanika udhaifu wa kamati yake JK?Weka tafakari

He he..Waziri kumuogopa JK sasa hivi ni sawa na mtoto kumuogopa baba yake kwa hofu ya kutopewa hela ya kula wakati ameshamaliza shule na kupata kazi - JK ni obsolete, ameshakuwa kama Benjamin Mkapa tu sasa hivi - muda wa yeye kuweza kutoa favors umeisha kwa hivo hana tena lake jambo
 
Nchimbi amezoea, alikuwa kwenye mtandao wa kumuingiza Ikulu JK. Akapewa cheo cha uwaziri. Alikuwa na matumaini tena kuwa akiukwa urais Lowasa attateuliwa kuwa Waziri Mkuu. Sasa ndoto zimeyeyuka. Kwa nini asiropoke yote
unachukuliaje suala la kundi la akina Nchimbi?Je ni watu ambao wanaweza kutoa siri za kamati kuu?Ni watu wa aina hiyo
 
He he..Waziri kumuogopa JK sasa hivi ni sawa na mtoto kumuogopa baba yake kwa hofu ya kutopewa hela ya kula wakati ameshamaliza shule na kupata kazi - JK ni obsolete, ameshakuwa kama Benjamin Mkapa tu sasa hivi - muda wa yeye kuweza kutoa favors umeisha kwa hivo hana tena lake jambo

pamoja na yote JK bado ni mwenyekiti wa chama na Rais wa JMT kwa miezi mitatu ijayo!Ulishawahi sikia lini mjumbe wa kamati kuu anatoka nje na kumkosoa mwenyekiti kwa shughuli za kwenye kikao na asiadhibiwe?Maswala ya ndani ya chama humalizwa ndani ya chama
 
Kumbe waziri mkuu chini ya Lowassa angekuwa Nchimbi na waziri wa mambo nje chenge..kweli Lowassa ni mpuuzi na mtu wa ajabu sana
 
Back
Top Bottom