Kama ni kweli basi CCM ni master mind na imefanikiwa!

pamoja na yote JK bado ni mwenyekiti wa chama na Rais wa JMT kwa miezi mitatu ijayo!Ulishawahi sikia lini mjumbe wa kamati kuu anatoka nje na kumkosoa mwenyekiti kwa shughuli za kwenye kikao na asiadhibiwe?Maswala ya ndani ya chama humalizwa ndani ya chama
Labda niongezee hapo kidogo
  • Nchimbi wakati anampigia Kikwete debe alikuwa na matumaini, lakini ni yeye aliyeshughulikia lile Jengo la UVCCM kupata mbia kwa kusaidiwa na Lowassa, sasa alipoona JK kamtupa akajua Lowassa hatamsahau ili wazime kashfa ya hilo Jengo
  • Mzee Kimbisa licha ya kuwa Shemeji yake Lowassa lakini ni wao waliokula hela za Muhimbili, Abbort, na hata Red Cross kipindi hicho ni Meya wa Jiji kwa hiyo usishangae na kina Slaa, Madabida, nayule meya wa Jiji mwenye m (nimesahau jina) walihuzunika kwani kwa Magufuli au membe yatafufuka km ya akina Mramba
  • Sofia yeye alimuingiza JK enzi za Mwinyi kuwa Waziri lakini wakati wa mchakato wa UWT pale ukumbi wa Chuo cha Mipango huyu Mama ndiye aliyepokea Fuba na kuwagawia UWT
  • Umoja wa Vijana (UVCCM) hawakurudi nyuma kina Sadifa na Mavunde kwenye kundi hilo
Kwa hiyo Nchimbi kuwaelezea waandishi yaliyo moyoni jana ilikuwa Kikao kimeshamalizika, na baada ya pale hakupandishwa gari lake sijui alikoenda jielezea zaidi
 
Mawazo yako yanaonyesha hujui undani wa mchakato mzima. Ni hivi... Lowassa NEC na mkutano mkuu anapita kwa kishindo kabisa kwani huko amepandikiza watu wake wengi wa kutosha. Na akipita hapo kwenye uchaguzi kutakuwa hamna shida kwani tume ya uchaguzi ni yao. Sasa hai-make sense wafanye harakati zooote hizi kama unavyo-suggest kwani Kikwete atakuwa anajidhalilisha mwenyewe na kuonekana kama kiongozi mwoga na asiyejua mbele wala nyuma.

ndugu unaonekana wewe ndio huelewi,kamati kuu iliundwa na wajumbe kutoka NEC!Kazi ya kamati kuu ni kuchuja na kubaki na watu 5 na kupeleka NEC iwashughulikie hao na kupata majina matatu ambayo yanaenda Mkutano mkuu!Kama NEC haijaridhika na uteuzi wa hao wajumbe 5 toka kamati kuu basi ina mamlaka ya kuyafutilia mbali na kurudisha mchakato uanze upya na kwa vigezo vp Kamati kuu ivitumie!
NEC haiwezi kupitisha mtu ambaye hayumo kwenye walioteuliwa na kamati kuu,sasa unaposema lowassa atapitishwa kwa kishindo na NEC una maana gani?
 
mkuu yamesha Toka majina ya 3 bora cdhani kama lile wazo lako linaweza kutokea thanx god so tunawasubili on site

hatua ilipofikia ni kupiga kura na NEC tumeambiwa itakaa saa 3 kuendelea na kikao!Sasa sijui hayo majina wamepata wapi?Ila kama ni kweli basi ukawa tutasukuma mlevi
 
Labda niongezee hapo kidogo
  • Nchimbi wakati anampigia Kikwete debe alikuwa na matumaini, lakini ni yeye aliyeshughulikia lile Jengo la UVCCM kupata mbia kwa kusaidiwa na Lowassa, sasa alipoona JK kamtupa akajua Lowassa hatamsahau ili wazime kashfa ya hilo Jengo
  • Mzee Kimbisa licha ya kuwa Shemeji yake Lowassa lakini ni wao waliokula hela za Muhimbili, Abbort, na hata Red Cross kipindi hicho ni Meya wa Jiji kwa hiyo usishangae na kina Slaa, Madabida, nayule meya wa Jiji mwenye m (nimesahau jina) walihuzunika kwani kwa Magufuli au membe yatafufuka km ya akina Mramba
  • Sofia yeye alimuingiza JK enzi za Mwinyi kuwa Waziri lakini wakati wa mchakato wa UWT pale ukumbi wa Chuo cha Mipango huyu Mama ndiye aliyepokea Fuba na kuwagawia UWT
  • Umoja wa Vijana (UVCCM) hawakurudi nyuma kina Sadifa na Mavunde kwenye kundi hilo
Kwa hiyo Nchimbi kuwaelezea waandishi yaliyo moyoni jana ilikuwa Kikao kimeshamalizika, na baada ya pale hakupandishwa gari lake sijui alikoenda jielezea zaidi

so unaonesha hawa watu ni watiifu kwa lowassa na si JK,sofia bado ni waziri!Tusubiri tuone hatua za kinidhamu zikichukuliwa au tutaelewa vinginevyo
 
ndugu unaonekana wewe ndio huelewi,kamati kuu iliundwa na wajumbe kutoka NEC!Kazi ya kamati kuu ni kuchuja na kubaki na watu 5 na kupeleka NEC iwashughulikie hao na kupata majina matatu ambayo yanaenda Mkutano mkuu!Kama NEC haijaridhika na uteuzi wa hao wajumbe 5 toka kamati kuu basi ina mamlaka ya kuyafutilia mbali na kurudisha mchakato uanze upya na kwa vigezo vp Kamati kuu ivitumie!
NEC haiwezi kupitisha mtu ambaye hayumo kwenye walioteuliwa na kamati kuu,sasa unaposema lowassa atapitishwa kwa kishindo na NEC una maana gani?
Angepitishwa ange... kama jina lake lingeenda kwenye NEC. Lakini halikuenda... kwasababu waliliondoa. Na waliliondoa kwasababu HAWAMTAKI (soma bwana mkubwa hamtaki). Sawasawa? Kwa kifupi hiyo theory yako hai-make sense. Halafu basi jaribu kusikiliza watu wanaojua undani wa hili sakata na usibishe kwa theory zako za kijiweni.
 
so unaonesha hawa watu ni watiifu kwa lowassa na si JK,sofia bado ni waziri!Tusubiri tuone hatua za kinidhamu zikichukuliwa au tutaelewa vinginevyo

Wewe mkuu uko kwenye duania ya kipeke yako. Unacheza na madaraka? Unataka wamtii Kikwete ambaye muda wake umeisha waache kuangalia ya mbele? Unajua muda na gharama waliowekeza kwenye huu mchakato? Wewe ulitegemea wakubali na kusema hewala bwana? Tena wanavyofanya ndio vizuri kweli kwani itabidi Kikwete na huo mteule wake wawaite chemba wayamalize.. Unajua juhudi zinazoendelea za kumbembeleza Lowassa na kundi lake ili wafikie muafaka ili nao wapate vyeo? Basi kama hujui funguka! Si ajabu Lowassa na hao frontline wake wakapata ''mgao'' mzuri sana kwa huo ''utovu wao wa nidhamu''
 
hatua ilipofikia ni kupiga kura na NEC tumeambiwa itakaa saa 3 kuendelea na kikao!Sasa sijui hayo majina wamepata wapi?Ila kama ni kweli basi ukawa tutasukuma mlevi

pouwa let's wait en see mkuu
 
Angepitishwa ange... kama jina lake lingeenda kwenye NEC. Lakini halikuenda... kwasababu waliliondoa. Na waliliondoa kwasababu HAWAMTAKI (soma bwana mkubwa hamtaki). Sawasawa? Kwa kifupi hiyo theory yako hai-make sense. Halafu basi jaribu kusikiliza watu wanaojua undani wa hili sakata na usibishe kwa theory zako za kijiweni.

ange za nini,hajapitishwa!Na kama NEC ikitaka arudi itabidi irudishe mchakato kamati kuu!Huko akipitishwa atakuja NEC na mchakato utaendelea,huu ndio utaratibu!swali langu ni je,hilo likifanyika litamweka lowassa mazingira gani?Umaarufu wake haujaongezeka?Kama umeongezeka,je kulikuwa na uwezekano wa mtu kuona namna ya kumtakatisha lowassa?je,unadhani kama ni mbinu,imefanikiwa?

Ndugu kwenye mchezo wa mpira,shangwe kubwa hutokea pale mnaposhinda from behind,yaani mlikuwa mmepigwa goli moja then dakika mbili za mwisho mnasawazisha na kuongeza!Hapo shangilia yake mji mzima watajua!
Ndio kama sakata la lowassa,kama akipewa nafasi na akapita kukiwakilisha chama basi shangwe lake mtaani litasababisha hata mtoto mdogo ajue kuna jambo!
Hili likitumika vema,ni silaha nzuri ya kujitangaza bila kutumia nguvu!
Wake up,hata kama hawakupanga mbinu hii,huoni kuwa inaweza kuwa ni master mind yenye advantage
 
Really not applicable. CCM imeshapata doa kubwa hasa kwa kumatwa kwa marundo ya pesa. Maamuzi ya namna hiyo hayataaminiwa kabisa
 
ange za nini,hajapitishwa!Na kama NEC ikitaka arudi itabidi irudishe mchakato kamati kuu!Huko akipitishwa atakuja NEC na mchakato utaendelea,huu ndio utaratibu!swali langu ni je,hilo likifanyika litamweka lowassa mazingira gani?Umaarufu wake haujaongezeka?Kama umeongezeka,je kulikuwa na uwezekano wa mtu kuona namna ya kumtakatisha lowassa?je,unadhani kama ni mbinu,imefanikiwa?

Ndugu kwenye mchezo wa mpira,shangwe kubwa hutokea pale mnaposhinda from behind,yaani mlikuwa mmepigwa goli moja then dakika mbili za mwisho mnasawazisha na kuongeza!Hapo shangilia yake mji mzima watajua!
Ndio kama sakata la lowassa,kama akipewa nafasi na akapita kukiwakilisha chama basi shangwe lake mtaani litasababisha hata mtoto mdogo ajue kuna jambo!
Hili likitumika vema,ni silaha nzuri ya kujitangaza bila kutumia nguvu!
Wake up,hata kama hawakupanga mbinu hii,huoni kuwa inaweza kuwa ni master mind yenye advantage

Kalakabaho. Baki na theory yako wakati wenzako wameshagawana vyeo vyote!
 
My wish hv been granted,sasa UKAWA ni mwendo mdundo!Hofu yangu ilikuwa watu wasifall in love na lowassa kwa sympath!
 
Sasa ulivyokuwa unaambiwa unabisha ni nini? Lowassa wamekosana na Kikwete siku nyingi halafu wewe unakuja na theory isiyoeleweka. Kwa taarifa yako CCM wanamsimamisha Magufuli na Amina
 
Nimepata wakati mgumu kufikiri kwanini ccm imemtema lowassa tena kwa kuvunja katiba ya chama kwa kuwasilisha majina pungufu kwenye kamati kuu kwa ajili ya mchujo,ikumbukwe kwa mujibu wa kanuni majina yote yanatakiwa yawasilishwe pale!

Lowassa anakubalika ndaani na nje yaa chama,japo kuna watu walishachoka ccm na kwenda upinzani lakini bado wana imani na mtu huyu:

Sasa CCM wamemuacha vp mtu huyu hata kwenye tano bora wakati ndiye mgombea aliyekusanya wadhamini wengi na kuungwa mkono kuliko yeyote kati ya watia nia?

Huu waweza kuwa mchezo uliochezwa vizuri kupima upepo ili hata wale walioko upinzani wamuunge mkono lowassa kuwa hakustahili kuenguliwa!Hapa ndipo ngoma itachezwa mpaka,watumwe akina Nchimbi kwenda kutangaza kupinga maamuz ya kamati kuu ili kuwashtua wananchi kuwa lowassa kaonewa!

Then Baadae NEC ipinge maamuzi ya kamati kuu ili kurudisha nafasi kwa mchakato kurudiwa upya na hapa ndipo lowassa apitishwe!

Kwa style hiyo ataungwa mkono na hata wale ambao hawakumhitaji kama angepitishwa in the first place!

Tufikiri nje ya box,if this is the plan bas CCM noma!

Did u see it coming?je,kuna possibility hiyo?

Tusubiri

ama kweli tusubirie.
 
Sasa ulivyokuwa unaambiwa unabisha ni nini? Lowassa wamekosana na Kikwete siku nyingi halafu wewe unakuja na theory isiyoeleweka. Kwa taarifa yako CCM wanamsimamisha Magufuli na Amina

Hahaaaa,kumbe hukuelewa na wewe!Ingekuwa hivyo delays zote za nin?Mimi nimefurahi coz ts better kwa ukawa kuliko lowassa angepitishwa
 
Hahaaaa,kumbe hukuelewa na wewe!Ingekuwa hivyo delays zote za nin?Mimi nimefurahi coz ts better kwa ukawa kuliko lowassa angepitwa

Mkuu delays zimetokana na hali halisi. Lowassa alishajipanga vizuri. Ukitaka kumchinja kobe..... Anyway hata mimi naona Lowassa kuondolewa ni vizuri lakini bado tuna kikwazo cha tume ya uchaguzi.... Watatumia nguvu kumshindisha mtu wa CCM. Labda watanzania tuache woga na tutumie nguvu ya ziada....
 
Hahaaaa,kumbe hukuelewa na wewe!Ingekuwa hivyo delays zote za nin?Mimi nimefurahi coz ts better kwa ukawa kuliko lowassa angepitishwa
yaani Lowasa angepitishwa IKAWA wangechukua hilo CCM ilishaligundua
sasa kwa Magufuli ni vipindi viwili CCM itamsimamisha hivyo kitu km UKAWA wasubiri miaka 10 ijayo yaani 2025
leo Dr Slaa kaimaliza UKAWA maana kajipitisha kuwa mgombea bila kumshirikisha Lipumba wala wenzake wa NCCR, TLP nk
sasa sijui Magufuli na Slaa wapinzani wataambulia nini tena?
 
Back
Top Bottom