Nimesikia kajukuu. Namsubiria anipruvie kuwa hazinitoshi. Otherwise nitaprove otherwise.
Na yeye ametulia na wewe???:A S 39:
Samahani kaka zinakutosha sana, ulimi uliniteleza. Lakini napenda ujue kuwa sikuhitaji wewe wala bwana mwingine, ninaye huyu ananitosha upo hapo? Na usitegemee eti atanitema nije kwako, hilo halitatokea ng'o. Kwanza sina shida na mwanaume wa alimradi anavaa suruali au ana pesa, no. Kama suruali hata mie navaa na pesa ninazo za kunitosha, sihitaji buzi. Penzi ninalohitaji ndilo huyu bwana ananipatia nami namkidhi vilivyo, watu wazima tunajilia vyetu kwa raha zetu, wa kununa wakinuna hainihusu. Anayechunguza achunguze, akichoka ataacha. Mwanamke mzima na elimu tele midigrii kibao hadi ya ulaya anahangaika hadi kumnyang'anya mume wake simu eti akae nayo aone wanaompigia, kang'ang'ania simu ya mtu miezi 3 anaenda nayo ofisini anarudi nayo kaambulia patupu, vya kuliwa vimeendelea kuliwa. Kama hulipi hulipi tu, halohaloooo msitake ncheke mie.
Da Sophy nimepata picha halisi sasa!!
unayemwibia mume wake amekupata!!!
Kutoka na mume wa mtu ni utovu wa nidhamu, nafikiri kuna vijana wengi tu wako wanakuhitaji kwa nini ujipe karaha na lawama zisizo za msingi? Ni ushauri na siyo lazima uuchukue: imagine wewe unachukua mume wa mtu kesho unaolewa wenzio wanachukua utajisikiaje?
nafikiri siyo kitendo kizuri kutembea naa wanaume wa wenzenu.
na yupo humuhumu JF hapo nakwambia leo nikuomba talaka kwenda mbele kumbe????????
Na si ajabu ndo mapya yaani hata miezi kadhaa hayana so ni ile novelity hali ya upya wa mapenzi ndo unampa wendawazimu. Ngoja jamaa akinai atafute makazi mapya. Atajibeba
mm bado sijaoa naweza fikiriwa hiyo nafasi??
with a mentality like this kisha useme unajiheshimu?! hujiheshimu my dear .................mwenye kijiheshimu hawezi kumvunjia heshima mwenziwe kwa maneno ya kifedhuli ya namna hii hata siku moja
Kwa hiyo wewe watimiziwa chumbani kwa mke mwenzio? Kweli unajiheshimu dada yangu.
Nikwambie siri
Huyo mke mwenzio siku akiamua kumchanganya mumeo kwa mahaba wewe pasi yako ni rahisi kufutika maana imeandikwa kwa penseli. na kwa maana hiyo anakuja kwako kupoza mapungufu anayoyapata kwa mkewe au kwenye familia yake. ukubali usikubali MAPOZEO ni wewe na wewe utabaki MAPOZEO na vile vile ukishachuja litatafutwa POZEO lingine au atarudi kwa mkewe. Hakunaga nyumba ndogo ya daima bibie!!
Tatizo lako ni kutotaka kuelewa, ushaambiwa siti zimejaa we wang'ang'ana kuingia kwanini usitafute usafiri mwingine na haraka huna? Tafuta wako ufunge nae ndoa na utulie naye!
Thubutuuu! Si ampe basi kama anacho cha kumpa.
Wadada wa dizaini hii wanao penda kudandia waume za watu, huwa hawaolewi inakuwa kama gundu vile,
Si kaonja hata mseme vp kesha ona raha ya mme wa mtu hapo usikute kaaidiwa mkoko au mjengo.
hadi ule mtandao una mpa?? maana nasikia ndo hasa wanachofata huko kwenu......