Kama natoka na mumeo...

hehehe hii sredi imekaa kama wimbo wa rusha roho a.k.a mipasho. wapi mzee yussuf aweke chorus?. acha nisepe!. klorokwini iz not richebo in zis useless sredi.

ungesepa bila kuchangia ningekuona ni usefully (wa maana) zaidi ... vinginevyo u r the most useless bunch of *** in this forum!
 
Kwa hiyo wewe watimiziwa chumbani kwa mke mwenzio? Kweli unajiheshimu dada yangu.
Nikwambie siri
Huyo mke mwenzio siku akiamua kumchanganya mumeo kwa mahaba wewe pasi yako ni rahisi kufutika maana imeandikwa kwa penseli. na kwa maana hiyo anakuja kwako kupoza mapungufu anayoyapata kwa mkewe au kwenye familia yake. ukubali usikubali MAPOZEO ni wewe na wewe utabaki MAPOZEO na vile vile ukishachuja litatafutwa POZEO lingine au atarudi kwa mkewe. Hakunaga nyumba ndogo ya daima bibie!!

Nakwambia hawa watu sijui wakoje kuolewa hawaolewi ila wame za watu wanapenda kweli!! hata huku kwetu kuna msichana mmoja afisa maendeleo ya manispaa anatabia hiyo mpaka hivi karibuni amemruhusu mtu kuoa lakini akasema nitaendelea naye mpaka akome sasa sijui anataka nini nanamlia taimingi nimweke kwenye magazeti ya Shongono tuone kama hiyo kazi ya uafisa maendeleo hataiona chungu
 
Tatizo lako ni kutotaka kuelewa, ushaambiwa siti zimejaa we wang'ang'ana kuingia kwanini usitafute usafiri mwingine na haraka huna? Tafuta wako ufunge nae ndoa na utulie naye!
 
si mpaka niolewe babu wee! na ikitokea nimebahatika hivyo nakuapia hakuna wa kumchukua mume wangu, nazijua mbinu zote! Kwa taarifa yako niliyenaye ananiambia kila kitu kinachotokea huko kwake na mkewe hadi yanamshinda. Na mashosti zangu wengine wananisimulia mambo kibao tu, yaani nina elimu acha. Labda tu asitokee wa kunioa, lakini akija kwangu haendi popote nakuapia, makosa yote ya walioolewa nayajua.

hadi ule mtandao una mpa?? maana nasikia ndo hasa wanachofata huko kwenu......
 
Da Sophy ni dhambi kuiba mme wa mwenzio kwa nn usitafute wako??
Post yako imenichosha ingawa ni short lakini msg send

mume haibwi, unlec uniambie alikupokonya barabarani...vingine ni matamaa yao yanawawasha/wasumbua...
 
sasa ukitulia nae utapata wako lini? manake anakupotezea tu muda, kukubana anakubana yeye akitoka hapo anaenda kwa mkewe wewe wajilalia cku zinasonga, utapataje wa kwako kwa gia hii?au una malengo yae mengine?

Wadada wa dizaini hii wanao penda kudandia waume za watu, huwa hawaolewi inakuwa kama gundu vile,
Si kaonja hata mseme vp kesha ona raha ya mme wa mtu hapo usikute kaaidiwa mkoko au mjengo.
 
hadi ule mtandao una mpa?? maana nasikia ndo hasa wanachofata huko kwenu......

Hahahaha yeah wanaume wanao heshimu ndoa zao huwa wanajiexpress kwenye nyumba ndogo chunguza utabaini.
 
si mpaka niolewe babu wee! na ikitokea nimebahatika hivyo nakuapia hakuna wa kumchukua mume wangu, nazijua mbinu zote! Kwa taarifa yako niliyenaye ananiambia kila kitu kinachotokea huko kwake na mkewe hadi yanamshinda. Na mashosti zangu wengine wananisimulia mambo kibao tu, yaani nina elimu acha. Labda tu asitokee wa kunioa, lakini akija kwangu haendi popote nakuapia, makosa yote ya walioolewa nayajua.

Hee msikieni huyu hivi wadhani ni huyo wa kwako tu ndie anayetoa siri za mkewe kwako? Mbona karibia wote wanaocheat hufanya hivyo? So usijidanganye kuwa kwako kafika ndo mana anakuelezea mambo ya familia yake. Ni mbinu tu ya kukufanya uendelee kumpa uroda kwa jina la kukupenda!! Bila kukwambia mkewe kashindwa hiki na kile si utamshangaa kwa nini kakufuata?? pole wee

Hao marafiki wanaokueleza ujinga huo its either mko kwenye kundi moja au wanakucheka ujinga! Kalagha baho. Eti wako hatochukuliwa ah mie unanichosha mpenzi hebu nisepe maana unantia hasira ka vile mume wangu ndo unayetembea naye!!
 
Labda tu asitokee wa kunioa, lakini akija kwangu haendi popote nakuapia, makosa yote ya walioolewa nayajua.

Kha naona full maufundi ya uswazi vibwanga kama hivi huwa nasikia Tandale kwa Mtogore, Manzese kwa Mfuga mbwa, tandika, Buguruni huko
 
Hee msikieni huyu hivi wadhani ni huyo wa kwako tu ndie anayetoa siri za mkewe kwako? Mbona karibia wote wanaocheat hufanya hivyo? So usijidanganye kuwa kwako kafika ndo mana anakuelezea mambo ya familia yake. Ni mbinu tu ya kukufanya uendelee kumpa uroda kwa jina la kukupenda!! Bila kukwambia mkewe kashindwa hiki na kile si utamshangaa kwa nini kakufuata?? pole wee

Hao marafiki wanaokueleza ujinga huo its either mko kwenye kundi moja au wanakucheka ujinga! Kalagha baho. Eti wako hatochukuliwa ah mie unanichosha mpenzi hebu nisepe maana unantia hasira ka vile mume wangu ndo unayetembea naye!!

Mkuu mbona kama Dasophy anakufanyia wewe maake hapa ni kweli inawezekana huyo mkewe yupo humu JF ndo maana kaja straight kwa kumpa taarifa huyo aibiwaye.
 
Kha naona full maufundi ya uswazi vibwanga kama hivi huwa nasikia Tandale kwa Mtogore, Manzese kwa Mfuga mbwa, tandika, Buguruni huko

Atakuwa wa huko huko huyu we wamwonaje?? maana ah mtoto kajituliza, full kujiheshimu... mume atatoka saa ngapi?
 
Asante sana hebu waeleze maana kuna wengine hadi wana mashutuma ya kijinga basi wanafikiri kila anayetoka na mume wa mtu basi eti changu, kivipi mbona kuna wanawake wengi tu wameolewa na ni machangu wa kutisha, na tupo tusioolewa tumetulia kiheshima zetu na bwana mmoja

hee bwana 1?....na huyo bwana ana wake wa ubavu na unalijua hilo, umeulizwa hapo juu ukija ckia huyo bwana ana mrembo mwingine utajickiaje?
 
Unapenda wanaume walio oa? Vp kwa wale ambao hawajaoa?
Naona swali langu la awali limejibilika.

Imetokea tu kwamba huyo ndiye aliyenipenda, na aliponionesha nia nami nikawa nimempenda, lakini bahati mbaya ndiyo hiyo kwamba ameoa. Na mimi nahitaji mapenzi na yeye ndiyo anayonipa nami nampa. Ingetokea kuwa hajaoa ningempenda pia kama sasa, na bila shaka tungeoana. Kwa sasa hivi siwezi kuzungumzia hao ambao hawajaoa maana ninaye mpenzi huyu niliyenaye, siwezi kuchanganya wapenzi sina tabia hiyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom