Kama mzazi mwenye akili timamu siwezi kumchoma moto mwanangu hata kwa dk 2, Je, Mungu anaweza kumchoma moto mwanadamu aliyemuumba milele na milele?

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,601
2,000
Wakuu salama?
Muumba na mzazi mwenye mamlaka na uchungu zaidi juu ya mwanadamu ni Mungu muumba.
Yaani kama unamvumilia, kumjali na kumpenda mwana wako basi jua Mungu aliyemuumba anampenda zaidi.
Mwanangu hata afanye kosa gani, maadamu tu nina akili timamu siwezi kumtosa jikoni aungue hata kwa dk 2.
Je, Mungu muumba anaweza kumtupa mwanadamu dhaifu motoni milele na milele?
Je, Mungu hana upendo unaomzidi mzazi?
Nikifungua makabrasha yangu naambiwa kuwa yeye ni zaidi ya mama.
 
Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,601
2,000
Ngo
Tatizo lako liko hapa;kumlinganisha Mungu na mwanadamu.

Unaamini kisa cha Sodoma na Gomorah?Vipi kuhusu gharika ya Nuhu?Kama haya yaliwezekana ,inakuwaje kesho ashindwe kukuteketeza wewe unayefanya yale yale waliyofanya watu wa miji niliyoitaja?
Yudu 1:7, Kama vile sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uesherati kwa jinsi moja na hawa.....Wakaadhibiwa katika moto wa milele.
Nini maana ya neno milele?
Je, mpaka sasa wanaendelea kuteketea?
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
2,668
2,000
Wakuu salama?
Muumba na mzazi mwenye mamlaka na uchungu zaidi juu ya mwanadamu ni Mungu muumba.
Yaani kama unamvumilia, kumjali na kumpenda mwana wako basi jua Mungu aliyemuumba anampenda zaidi.
Mwanangu hata afanye kosa gani, maadamu tu nina akili timamu siwezi kumtosa jikoni aungue hata kwa dk 2.
Je, Mungu muumba anaweza kumtupa mwanadamu dhaifu motoni milele na milele?
Je, Mungu hana upendo unaomzidi mzazi?
Nikifungua makabrasha yangu naambiwa kuwa yeye ni zaidi ya mama.
Sodoma na gomora ilikuwaje
 
XaviMessIniesta

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
2,080
2,000
Tatizo lako liko hapa;kumlinganisha Mungu na mwanadamu.

Unaamini kisa cha Sodoma na Gomorah?Vipi kuhusu gharika ya Nuhu?Kama haya yaliwezekana ,inakuwaje kesho ashindwe kukuteketeza wewe unayefanya yale yale waliyofanya watu wa miji niliyoitaja?
gharika ilikuwa mafuriko tu mkuu na sodoma na gomora ule moto ulisababishwa na mlipuko wa volcano maeneo yale enzi hizo elimu si unajua ilikua ndogo

ni sawa na kupatwa kwa jua watu walichukulia eti ni mungu kakasirika
 
The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
823
1,000
Ngo

Yudu 1:7, Kama vile sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uesherati kwa jinsi moja na hawa.....Wakaadhibiwa katika moto wa milele.
Nini maana ya neno milele?
Je, mpaka sasa wanaendelea kuteketea?
Ndugu kuna mambo mawili debatable katika uzi asilia wa mleta uzi; (1)suala la mdhambi KUCHOMWA MOTO (2) suala la mdhambi KUCHOMWA MOTO WA MILELE.Hii namba 2 inakubaliana na namba 1,ila yenyewe ikaenda mbele zaidi kwa kuongeza kitu kingine;muda (duration) ya hukumu hiyo.

Mimi katika comment yangu nimeishia kujikita katika namba 1 pekee,hiyo nyingine namba 2 sijaigusia.MIMI NAAMINI MUNGU ATAWAANGAMIZA WADHAMBI KWA MOTO.Wewe unaamini nini?tuanze na hili kisha twende kwenye namba 2.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom