Kama mzazi mwenye akili timamu siwezi kumchoma moto mwanangu hata kwa dk 2, Je, Mungu anaweza kumchoma moto mwanadamu aliyemuumba milele na milele?

Kama wewe unampenda baba yako unaweza kumdharau kwa maagizo yake ukayapuuza na kumpinga baba yako..?

wewe unapomaliza kula mihogo yale maganda huyatupi unayahifadhi ndani kuonesha upendo wako dhidi ya muhogo..?
Tunawapenda sana baba zetu. Tunawaudhi na kuwasikitisha sana lakini bado wanatupenda, kutupa moyo na kutusupport.
 
Jifunze kutoa mifano na kuweka kitu mahala pake,huu mfano hapa si mahala pake,sababu hiyo ni kauli ambayo haina mkanushaji,na atakae kanusha yeye ndio anae wajibika kutoa sababu kwanini anakanusha,na hapo kwenye kauli hiyo msemaji angewajibika kuthibitisha hilo,endapo mwenye kuambiwa ambae ni nafsi ya pili,angesema hivi "Kwanini unasema mimi nitakufa kesho ?", hili ni swali ambalo nafsi ya pili haja kanusha bali amehoji sababu nafsi ya hajui kwanini na nafsi ya kwanza anatakiwa athibitishe. Hii ni tofauti na wewe.

Fikiria hili kwa umakini,kisha uniambie kwanini umekanusha.
Kwaheri naona tutakesha.
 
Good for nothing except for burning... Hao ni watu ambao walimkasirisha Mungu kwa matendo yao yasiofaa. Hawakuwa tayari kutubu dhambi zao na kupata msamaha ili Mungu awasamehe. Hawakuwa tayari kuacha njia/ nyendo zao mbaya na kumgeukia Mungu ili wapate rehema zake... Waliendelea katika njia zisizofaa mpaka mauti yalipo wakuta na sasa wanachuma matunda ya uharibifu wao...
Jehanam haikuundwa kwa ajili ya binadamu bali malaika waasi pamoja na shetani. Kwa kuwa Mungu hana sehemu nyingine ya kuwaweka hawa binadamu waovu basi atawamix humo humo pamoja na shetani.
Ole wao watakaoikosa Mbingu. Their trouble will be for real and for sure...
Kama Mungu Hana sehemu ya kuwaweka awaache hapa hapa duniani waendelee na maisha, hao anaotaka kwenda nao awachukue kwenda mbinguni
 
Kwaheri naona tutakesha.

Tuko pamoja.

Siku nyingine ujifunze kusoma kwanza kabla ya kukanusha jambo,yaani ukikanusha jambo hakikisha unalijua,hili tatizo nimeliona sana kwa wakanushaji wa mambo ya kiimani hasa Dini,yaani wanakanusha tu mambo kirahisi rahisi wakati elimu ya mambo hayo hawana,yaani vituko tu ilimradi wajijitutumue,mathalani jana kuna mtu alikuwa ameshupalia kwamba Mungu hayupo,ukimuuliza kwanini hayupo anasema "Sababu hayupo" ukimuuliza tena "Nini chanzo cha maisha ?" anakujibu "Sijui", sasa kama jambo hulijui unapata wapi nguvu ya kulikanusha ?

Huu ujinga huwa nauona humu jf tu. Lazima ifikie hatua muwe mna adabu juu ya elimu.

NIMEMALIZA .........!
 
Umejuaje kama ni uongo ? Je ukweli ni upi ?

Kwako wewe ili jambo liwe la ukweli au uongo linakuwa na sifa gani ?
weka ushahidi kama mafuriko hayo yalitokea America, Afrika , China Japan, Australia kipindi hicho kwa pamoja
 
Kama Mungu Hana sehemu ya kuwaweka awaache hapa hapa duniani waendelee na maisha, hao anaotaka kwenda nao awachukue kwenda mbinguni
By then, Dunia itakuwa haipo. Dunia hii itakunjwa kama karatasi na ulimwengu huu wa mwili wa nyama utatoweka. Wafu watafufuliwa. Wengine kwa ajili ya uzima wa milele na wengine kwa ajili ya mauti ya milele!
 
Wakuu salama?
Muumba na mzazi mwenye mamlaka na uchungu zaidi juu ya mwanadamu ni Mungu muumba.
Yaani kama unamvumilia, kumjali na kumpenda mwana wako basi jua Mungu aliyemuumba anampenda zaidi.
Mwanangu hata afanye kosa gani, maadamu tu nina akili timamu siwezi kumtosa jikoni aungue hata kwa dk 2.
Je, Mungu muumba anaweza kumtupa mwanadamu dhaifu motoni milele na milele?
Je, Mungu hana upendo unaomzidi mzazi?
Nikifungua makabrasha yangu naambiwa kuwa yeye ni zaidi ya mama.
Mungu wa kweli anafanya anavyotaka, hapangiwi wala hakuna mwenye haki ya kumuuliza, yeye ndiye aliyeumba na anamiliki ya alivyoviumba, sisi tulioumbwa ndo hatuna uhuru wa kufanya tutakavyo, hivyo tukifanya asiyoyata anaweza kutupunish vyovyote atakavyo. Yeye si binaadamu. Hata hizo mamlaka za ulimwengu ukifanya kinyume na sheria zao zinakupunish kwa nini ushangae kwa Mungu mwenye nguvu kubwa kuliko mamlaka za duniani? Wewe kama binaadamu hutaki hata mwanao aumwe lkn binaadamu wanaumwa, wanakufa, wanapata ajali, wanapata mafuriko na maporomoko, jee haya kwako yanaonesha mungu hana huruma? Au unazungumzia kuchomwa moto kwa sbb bado hatujashuhudia. Yapo mengi duniani ambayo binaadamu hatuwezi kuyafanya tunaamini yanaletwa na Mungu, au huyakubali, mbona unakufa au kufa binaadamu unapenda? No, ni kwa sababu Mungu ametaka. Ikiwa ni hivyo unavyodhani basi ni upuuzi kuleta mitume, vitabu,sheria...halafu iwe hata tusipofuata mitume na sheria hakuna adhabu. Huo ndo Uungu wa kuamua atakalo wala haulizwi. Bali Mungu ana huruma zaidi kuliko binaadamu. Tunaishi kwa pumzi alotupa yeye, vyakula, ardhi yake, na kila kitu na bado tunakanusha na kumpinga uwepo wake lkn bado anaendelea kutupa neema nyingi tu duniani. Ni logic kuwa lazima awatenganishe waliokuwa wakimtii kwa kuwapa zawadi na wasiomtii kwa kuwaadhibu atakavyo. Anatuhurumia na kutupa warning za kutosha hapa duniani tusipokuwa watiifu yeye si wa kulaumiwa bali ni sisi wenyewe.
 
Wewe umekosea mkuu, Moto wa milele means unaungua miaka nenda rudi hauzimiki.
Yaani kufa hufi ila cha moto utakiona!
Huo moto wa hivyo haupo...na haiwezekani ukawepo. Jiulize tu huo moto utakaowaka milele ukiwaunguza watu ambao nao hawafi milele...utawakia sehemu gani hapa duniani?

Maana ukisoma kitabu cha ufunuo...moto utakaowaunguza wenye dhambi utawaunguzia hapa hapa duniani. Na at the same time baada ya waovu kutoweka Mungu ataumba dunia mpya.

Sasa haiwezekani kuwe na dunia mpya ambayo haina waovu ndani yake...halafu hapo hapo kwenye dunia mpya pawepo na moto unaowaka ukiwaunguza waovu milele.
 
Aaah unanichanganya mie
 
Tunawapenda sana baba zetu. Tunawaudhi na kuwasikitisha sana lakini bado wanatupenda, kutupa moyo na kutusupport.
Mungu atakuhurumia hapa duniani tu.

Tahadhari ameshatoa zamani atakaye afuate asiyetaka akanushe.

Huko akhera waovu watachomwa milele hakuna kutoka.
 
Mungu atakuhurumia hapa duniani tu.

Tahadhari ameshatoa zamani atakaye afuate asiyetaka akanushe.

Huko akhera waovu watachomwa milele hakuna kutoka.
Ule msemo unaosema Mungu ni mwenye huruma walikosea ama? Au huruma yake ina kikomo?
 
Huo moto wa hivyo haupo...na haiwezekani ukawepo. Jiulize tu huo moto utakaowaka milele ukiwaunguza watu ambao nao hawafi milele...utawakia sehemu gani hapa duniani?

Maana ukisoma kitabu cha ufunuo...moto utakaowaunguza wenye dhambi utawaunguzia hapa hapa duniani. Na at the same time baada ya waovu kutoweka Mungu ataumba dunia mpya.

Sasa haiwezekani kuwe na dunia mpya ambayo haina waovu ndani yake...halafu hapo hapo kwenye dunia mpya pawepo na moto unaowaka ukiwaunguza waovu milele.
Sisi wengine mafundisho yetu hayaoneshi kama moto ni waduniani.

Unasemaje kuhusu sisi ambao mafundisho yetu hayasemi kama moto utawaka hapa duniani..?
 
Inasemekana sisi ni watoto wa Mungu
Hakuna kusemekana semekana mkuu.

قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ

(AL - IKHLAS' - 1)
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.اللَّهُ الصَّمَدُ

(AL - IKHLAS' - 2)
Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ

(AL - IKHLAS' - 3)
Hakuzaa wala hakuzaliwa.وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

(AL - IKHLAS' - 4)
Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.

Hakuzaa wala hakuzaliwa.

Sasa kama hakuzaa manake hana MTOTO KWA MAANA SIO MZAZI.

Na hakuzaliwa wala hana baba wala mama.
 
Ule msemo unaosema Mungu ni mwenye huruma walikosea ama? Au huruma yake ina kikomo?
Mungu ana huruma hapa dunani tu.

Huko akhera Mungu atakuwa na huruma na wema.

Na wala hatakuwa na huruma na watu waovu huko akhera.

Kwa hyo Mungu ni mwema,ana huruma.

Mnaposema Mungu anahuruma kumbukeni pia kwamba Mungu ni mksli kwa waovu.

Msibase uoande mmoja tu mkasahau kwingine.
 
Sisi wengine mafundisho yetu hayaoneshi kama moto ni waduniani.

Unasemaje kuhusu sisi ambao mafundisho yetu hayasemi kama moto utawaka hapa duniani..?
Nadhani pamoja na utofauti huo wa mafundisho uliopo kwenye maandiko ya vitabu vya dini...bado lengo la Mungu ni moja tu. Kuuondoa uovu usiwepo milele.

Kumbuka kuwa universe yote ni mali ya Mungu....so hata akiamua kwenda kuwachomea waovu sehemu fulani mbali na duniani....ambako huko wataungua milele, bado hatakuwa ametatua tatizo la dhambi.

Why? Kwa sababu bado waovu hao watakuwa hai milele wakiteketea pasipo kufa. Hivyo bado ktk himaya ya Mungu uovu utaendelea kuwepo kwa vile waovu watakuwa hai milele somewhere wakiungua.

Napenda nijifunze toka kwenye mafundisho ya kitabu unachokiamini...kinasema huo moto wa jehanum utawakia wapi?
 
Back
Top Bottom