Kama mzazi mwenye akili timamu siwezi kumchoma moto mwanangu hata kwa dk 2, Je, Mungu anaweza kumchoma moto mwanadamu aliyemuumba milele na milele?

Walioandika vitabu vya dini walikuwa na akili sana walikuwa na malengo yao. Mafundisho ya kuchomwa moto milele ni mafundisho ya uongo lengo likiwa ni kuwatisha watu wasiendelee kutenda maovu, ni kama kumtisha mtoto asipokula au akiiba utamchoma vidole.

Mafundisho kama haya ndiyo yanatumiwa na wachungaji walio wengi manabii wa uongo wanaoanzisha makanisa kama uyoga ili kujipatia utajiri kwa kuwadanganya waumini kuwa watoapo sadaka wanajiwekea akiba mbinguni, which is not true.

Hakuna moto wa milele wewe tenda mema uishi vizuri na walimwengu basi.
Kwa hyo moto upo lakini sio wa milele bali ni kwa muda tu..?
 
Wakuu salama?
Muumba na mzazi mwenye mamlaka na uchungu zaidi juu ya mwanadamu ni Mungu muumba.
Yaani kama unamvumilia, kumjali na kumpenda mwana wako basi jua Mungu aliyemuumba anampenda zaidi.
Mwanangu hata afanye kosa gani, maadamu tu nina akili timamu siwezi kumtosa jikoni aungue hata kwa dk 2.
Je, Mungu muumba anaweza kumtupa mwanadamu dhaifu motoni milele na milele?
Je, Mungu hana upendo unaomzidi mzazi?
Nikifungua makabrasha yangu naambiwa kuwa yeye ni zaidi ya mama.

Mungu atachoma milele viumbe vyake sio watoto wake. Kuna tofauti ya kiumbe cha Mwenyenzi Mungu na wana wa Mungu.

Wanadamu wasiomkiri Yesu Kristo kama ni Bwana na Mwokozi wa maisha yao wanaitwa VIUMBE na hawana tofauti mbweha au fisi watakaotupwa motoni milele pamoja na mashetani (Marko 16:15;Mathayo 25:41).

Wana wa Mungu au watoto wa Mungu ni wale waliotubu dhambi zao na kupokea muujiza wa kuokoka au wokovu kama Lutu na binti zake alivyookolewa katika moto wa Sodoma na Gomora.
 
Good for nothing except for burning... Hao ni watu ambao walimkasirisha Mungu kwa matendo yao yasiofaa. Hawakuwa tayari kutubu dhambi zao na kupata msamaha ili Mungu awasamehe. Hawakuwa tayari kuacha njia/ nyendo zao mbaya na kumgeukia Mungu ili wapate rehema zake... Waliendelea katika njia zisizofaa mpaka mauti yalipo wakuta na sasa wanachuma matunda ya uharibifu wao...
Jehanam haikuundwa kwa ajili ya binadamu bali malaika waasi pamoja na shetani. Kwa kuwa Mungu hana sehemu nyingine ya kuwaweka hawa binadamu waovu basi atawamix humo humo pamoja na shetani.
Ole wao watakaoikosa Mbingu. Their trouble will be for real and for sure...
 
Mungu atachoma milele viumbe vyake sio watoto wake. Kuna tofauti ya kiumbe cha Mwenyenzi Mungu na wana wa Mungu.

Wanadamu wasiomkiri Yesu Kristo kama ni Bwana na Mwokozi wa maisha yao wanaitwa VIUMBE na hawana tofauti mbweha au fisi watakaotupwa motoni milele pamoja na mashetani (Marko 16:15;Mathayo 25:41).

Wana wa Mungu au watoto wa Mungu ni wale waliotubu dhambi zao na kupokea muujiza wa kuokoka au wokovu kama Lutu na binti zake alivyookolewa katika moto wa Sodoma na Gomora.
Kwahiyo kuumba hakutoshi kwa Mungu kumhurumia mwanadamu.
Yeye huruma yake ni kwa waliomkiri Yesu tu?.
Kati ya muumbaji na mzazi aliyemzaa mtu yupi mwenye sympathy na mwanadamu?.
Kuna mzazi anaweza kuchemsha maji kwenye sufuria kubwa na kisha kumtosa mwana wake kwakuwa hajaosha vyombo baada ya kula?.
If yes, Hugo mzazi ni mwendawazimu.
If No. Je, mwanadamu anahuruma kuliko Mungu?.
Mimi binafsi hata vyombo vya dola vyote ulimwenguni vikiwa chini yangu na kwamba si dhambi kufanya tukio kama hill siwezi kumfanyia mwanangu Praise unyama mkuu hivi
 
Walioandika vitabu vya dini walikuwa na akili sana walikuwa na malengo yao. Mafundisho ya kuchomwa moto milele ni mafundisho ya uongo lengo likiwa ni kuwatisha watu wasiendelee kutenda maovu, ni kama kumtisha mtoto asipokula au akiiba utamchoma vidole.
Mafundisho kama haya ndiyo yanatumiwa na wachungaji walio wengi manabii wa uongo wanaoanzisha makanisa kama uyoga ili kujipatia utajiri kwa kuwadanganya waumini kuwa watoapo sadaka wanajiwekea akiba mbinguni, which is not true.
Hakuna moto wa milele wewe tenda mema uishi vizuri na walimwengu basi.
Sasa kwanini nitende mema kwa faida ya nani? Kwa sababu wakati wengine wanafanya wanavyojisikia bila kujari mema au uovu sasa iweje mie nijinyime kwa kutenda mema tu kwa kumfaidisha nani?
 
Kwahiyo kuumba hakutoshi kwa Mungu kumhurumia mwanadamu.
Yeye huruma yake ni kwa waliomkiri Yesu tu?.
Kati ya muumbaji na mzazi aliyemzaa mtu yupi mwenye sympathy na mwanadamu?.
Kuna mzazi anaweza kuchemsha maji kwenye sufuria kubwa na kisha kumtosa mwana wake kwakuwa hajaosha vyombo baada ya kula?.
If yes, Hugo mzazi ni mwendawazimu.
If No. Je, mwanadamu anahuruma kuliko Mungu?.
Mimi binafsi hata vyombo vya dola vyote ulimwenguni vikiwa chini yangu na kwamba si dhambi kufanya tukio kama hill siwezi kumfanyia mwanangu Praise unyama mkuu hivi
Kwahiyo asingekuwa mwanao uwezo wa kufanya hivyo unao?
 
Km mtoto amekua muasi anashirikiana na adui anataka kupindua utawala wa baba unapiga adui na mtoto pia make akufai Anaweza kukuua wew.
 
Mzazi akiwa anashindwa hata kumkanya mtoto wake pindi anapokosea kwa sababu ya upendo basi hali hiyo itaitwa kumdekeza mtoto hivyo si kitu kizuri sana,lakini pia hata akiwa mkali sana na kumpiga sana mwanae bado hali hiyo haina maana kuwa hana upendo kwa mwanae.

Yani mmoja anaweza kushindwa kufanya jambo fulani kisa upendo ila mwengine akaweza kulifanya japokuwa pia ana upendo,nashindwa kuelewa upendo hasa ni nini?
 
gharika ilikuwa mafuriko tu mkuu na sodoma na gomora ule moto ulisababishwa na mlipuko wa volcano maeneo yale enzi hizo elimu si unajua ilikua ndogo

ni sawa na kupatwa kwa jua watu walichukulia eti ni mungu kakasirika
Na katika mafuriko hayo yalikumba dunia yote wakafa wote isipokua familia ya Nuhu tu,ya moto iliteketea miji miwili Sodoma na Gomora na na miji ya jirani tu,so ni kweli gharika ilikua ile ya mafuriko ya Nuhu
 
Mafundisho ya kuchomwa moto milele ni mafundisho ya uongo lengo likiwa ni kuwatisha watu wasiendelee kutenda maovu, ni kama kumtisha mtoto asipokula au akiiba utamchoma vidole.

Umejuaje kama ni uongo ? Je ukweli ni upi ?

Kwako wewe ili jambo liwe la ukweli au uongo linakuwa na sifa gani ?
 
Anayesema kuna moto wa milele ndiye anayetakiwa ku prove.

Kutokana na kanuni za mjadala wewe unae kanusha unaonekana una elimu ya ziada kuhusu kile unachokikanusha,kwa maana hiyo wewe ndio mwenye haki zaidi ya kuthibitisha kutokuwepo kwa moto wa milele na ndio unatangulizwa.

Sasa hapa hutakiwi kukimbia kwa namna hiyo,wewe si unasema hakuna hilo jambo,ndio swali nimekuuliza umejuaje kama halipo hilo jambo ? Rahisi sana usikimbie swali la msingi.
 
Kama wewe unaupendo inakuwaje tena unachinja viumbe wake na kuwala? unakula nyama huku ukijilamba kwa utamu! Wewe ukiliwa kidogo unatumia sumu na bunduki kuwaua kisa tu wamekuuma au wanakukera wakiwa wanaruka huko na huko? Umeua sisimizi wa ngapi kwa kuwakanyaga tena kwa maksudi kabisa kwani wenyewe hawahitaji kuishi? Upendo wako upo wapi sasa!!?
 
Kutokana na kanuni za mjadala wewe unae kanusha unaonekana una elimu ya ziada kuhusu kile unachokikanusha,kwa maana hiyo wewe ndio mwenye haki zaidi ya kuthibitisha kutokuwepo kwa moto wa milele na ndio unatangulizwa.

Sasa hapa hutakiwi kukimbia kwa namna hiyo,wewe si unasema hakuna hilo jambo,ndio swali nimekuuliza umejuaje kama halipo hilo jambo ? Rahisi sana usikimbie swali la msingi.
Hivi mtu akikuambia kesho utakufa nani anayetakiwa ku prove.
 
Mafundisho ya kuchomwa moto milele ni mafundisho ya uongo lengo likiwa ni kuwatisha watu wasiendelee kutenda maovu, ni kama kumtisha mtoto asipokula au akiiba utamchoma vidole.

Usingesema maneno haya,mimi ndio ningekuwa na wajibu wa kuthibitisha,lakini kukanusha kwako kunaonyesha unakijua vyema jambo hili kuliko sisi tunao lisadiki. Kwa minajili hiyo sasa ndio utuambie ukweli ni upi na kwanini ?

Kufanya hivi itawafanya muwe sana pindi mnapokanusha mambo ambayo hamna elimu nayo,kisha kirahisi rahisi tu mnasema "Uongo" mara "Hayupo". Kufanya hivi bila kuonyesha uongo uko wapi na kwanini au kutokuwepo kwa jambo fulani na kwanini halipo ?, ni matumizi mabaya akili na uvivu wa kufikiria.

Nasubiri jibu ......
 
Moto wa milele....nionavyo mimi si kuwa utawaka milele...ila moto huo una matokeo ya milele. Yaani watakaounguzwa nao watapotea milele.

Yaani wataunguzwa na wataisha na hivyo hawatakuwepo milele zote. Maana somewhere kwenye maandiko Mungu anasema waovu wataunguzwa wawe majivu, na watu wema watatoka nje wakanyage majivu yao.

Lakini pia moto huo hauwezi kuwaka milele kwa vile Mungu anasema ataumba dunia hii upya na kuondoa kila doa la uovu.

Sasa dunia mpya haiwezi ku exist at the same time na Jehanum ya moto inayowaka milele. Hali ikiwa hivyo maana yake dhambi na wadhambi watakuwa bado wako hai milele. Na hivyo tatizo la dhambi litakuwa halijatatuliwa bado.

Kwa kuhitimisha, moto wa milele haumaanishi kuwa utawaka milele...kama ilivyokuwa kwa wakazi wa Sodoma na Gomora, hawaungui mpaka leo...moto huo ulikuwa na matokeo ya milele, yaani wakazi wa miji hiyo ndiyo wamepotea milele.

Hivyo na moto wa milele maana yake una matokeo ya milele, utawaunguza waovu mpaka wawe majivu kabisa, then hawatokuwepo milele zote
Wewe umekosea mkuu, Moto wa milele means unaungua miaka nenda rudi hauzimiki.
Yaani kufa hufi ila cha moto utakiona!
 
Hivi mtu akikuambia kesho utakufa nani anayehitaji ku prove.

Jifunze kutoa mifano na kuweka kitu mahala pake,huu mfano hapa si mahala pake,sababu hiyo ni kauli ambayo haina mkanushaji,na atakae kanusha yeye ndio anae wajibika kutoa sababu kwanini anakanusha,na hapo kwenye kauli hiyo msemaji angewajibika kuthibitisha hilo,endapo mwenye kuambiwa ambae ni nafsi ya pili,angesema hivi "Kwanini unasema mimi nitakufa kesho ?", hili ni swali ambalo nafsi ya pili haja kanusha bali amehoji sababu nafsi ya hajui kwanini na nafsi ya kwanza anatakiwa athibitishe. Hii ni tofauti na wewe.

Fikiria hili kwa umakini,kisha uniambie kwanini umekanusha.
 
Back
Top Bottom