Kama mzazi mwenye akili timamu siwezi kumchoma moto mwanangu hata kwa dk 2, Je, Mungu anaweza kumchoma moto mwanadamu aliyemuumba milele na milele?

soma biblia vizuri mzee, ameua hadi watoto sembuse kukuchoma moto tu!, kama kusamehewa dhambi tu ilibidi hadi mwanaye wa pekee ateseke na kufa sasa unadhani wewe utaachiwa tu kirahisirahisi?
 
Ninachozungumzia Mimi ni suala la mwanadamu kuchomwa moto kisa dhambi zake. Hili halipo, Bujibuji akatolea mfano wa Sodoma na Gomora, ndipo nami nikamuuliza je, mpaka leo wanateketea?
Maana pale kwenye Yuda 1:7 pameandikwa waliteketezwa na moto wa milele.
Ndugu kuna mambo mawili debatable katika uzi asilia wa mleta uzi; (1)suala la mdhambi KUCHOMWA MOTO (2) suala la mdhambi KUCHOMWA MOTO WA MILELE.Hii namba 2 inakubaliana na namba 1,ila yenyewe ikaenda mbele zaidi kwa kuongeza kitu kingine;muda (duration) ya hukumu hiyo.

Mimi katika comment yangu nimeishia kujikita katika namba 1 pekee,hiyo nyingine namba 2 sijaigusia.MIMI NAAMINI MUNGU ATAWAANGAMIZA WADHAMBI KWA MOTO.Wewe unaamini nini?tuanze na hili kisha twende kwenye namba 2.
 
Ngo

Yudu 1:7, Kama vile sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uesherati kwa jinsi moja na hawa.....Wakaadhibiwa katika moto wa milele.
Nini maana ya neno milele?
Je, mpaka sasa wanaendelea kuteketea?
Moto wa milele....nionavyo mimi si kuwa utawaka milele...ila moto huo una matokeo ya milele. Yaani watakaounguzwa nao watapotea milele.

Yaani wataunguzwa na wataisha na hivyo hawatakuwepo milele zote. Maana somewhere kwenye maandiko Mungu anasema waovu wataunguzwa wawe majivu, na watu wema watatoka nje wakanyage majivu yao.

Lakini pia moto huo hauwezi kuwaka milele kwa vile Mungu anasema ataumba dunia hii upya na kuondoa kila doa la uovu.

Sasa dunia mpya haiwezi ku exist at the same time na Jehanum ya moto inayowaka milele. Hali ikiwa hivyo maana yake dhambi na wadhambi watakuwa bado wako hai milele. Na hivyo tatizo la dhambi litakuwa halijatatuliwa bado.

Kwa kuhitimisha, moto wa milele haumaanishi kuwa utawaka milele...kama ilivyokuwa kwa wakazi wa Sodoma na Gomora, hawaungui mpaka leo...moto huo ulikuwa na matokeo ya milele, yaani wakazi wa miji hiyo ndiyo wamepotea milele.

Hivyo na moto wa milele maana yake una matokeo ya milele, utawaunguza waovu mpaka wawe majivu kabisa, then hawatokuwepo milele zote
 
Moto ni kwa ajili ya shetani na malaika zake. Mwanadamu ana uamuzi wa kuchagua. Ukichagua kutenda maovu basi utachomwa na shetani. Lakini kumbuka Mungu alimtuma mwana wake wa pekee Yesu Kristo ili kila amwaminie aweze kusamehewa dhambi zake na kuepuka kwenda motoni. Sasa yeye MUNGU amekupa njia ambayo ni Yesu Kristo. Tukimkataa huyo Jehanum inatusubiri. Kumbuka wakati wa Nuhu. Mungu aliteketeza watu wengi tu. Dunia ya sasa itachomwa na moto na kila kilichondani kitateketea. Lakini kabla ya siku hiyo mateso mengi yanatusubiri mbeleni kwa vile tumeacha kumcha Mungu na kupenda kutenda dhambi. Mwisho tutubu na tumrudie Mungu na tuache kutenda maovu na Mungu ataturehemu na kutusamehe.
 
Swali kwako: Wewe na Mungu nani mwenye huruma zaidi juu ya mwanao Neema?
Je, kuna kosa Neema akilifanya utamchinja?
Kama yes, basi akili yako ina mushkiri, na kama No. Je, wewe umempita Mungu kiwango cha huruma?
Kama wewe unampenda baba yako unaweza kumdharau kwa maagizo yake ukayapuuza na kumpinga baba yako..?

wewe unapomaliza kula mihogo yale maganda huyatupi unayahifadhi ndani kuonesha upendo wako dhidi ya muhogo..?
 
Ndugu kuna mambo mawili debatable katika uzi asilia wa mleta uzi; (1)suala la mdhambi KUCHOMWA MOTO (2) suala la mdhambi KUCHOMWA MOTO WA MILELE.Hii namba 2 inakubaliana na namba 1,ila yenyewe ikaenda mbele zaidi kwa kuongeza kitu kingine;muda (duration) ya hukumu hiyo.

Mimi katika comment yangu nimeishia kujikita katika namba 1 pekee,hiyo nyingine namba 2 sijaigusia.MIMI NAAMINI MUNGU ATAWAANGAMIZA WADHAMBI KWA MOTO.Wewe unaamini nini?tuanze na hili kisha twende kwenye namba 2.
Naamini watendadhambi wataangamizwa ila hakuna Moto wa milele.
 
Kama aliweza kuwateketeza watu kwa maji nuhu (immagine unakunywa maji mpaka mishipa inachanika unakosa pumzi unakufa) ,moto luti(hapa waliungua si kitoto) , volcano pompeii(italia hiyo hawa mpaka leo wamebaki masanamu ukumbusho kwetu) ,na aliweza kumuhifadhi farao asioze ili awe ukumbusho pia kwetu WE UNADHANI KUKUWEKA MOTONI NI KITU KIGUMU? USIJIFARIJI MKUU FUATA ANAVYOTAKA UISHI UTAUEPUKA HUO MOTO.
 
Wakuu salama?
Muumba na mzazi mwenye mamlaka na uchungu zaidi juu ya mwanadamu ni Mungu muumba.
Yaani kama unamvumilia, kumjali na kumpenda mwana wako basi jua Mungu aliyemuumba anampenda zaidi.
Mwanangu hata afanye kosa gani, maadamu tu nina akili timamu siwezi kumtosa jikoni aungue hata kwa dk 2.
Je, Mungu muumba anaweza kumtupa mwanadamu dhaifu motoni milele na milele?
Je, Mungu hana upendo unaomzidi mzazi?
Nikifungua makabrasha yangu naambiwa kuwa yeye ni zaidi ya mama.
Hivi kwanini unafikiri upendo unazuia kufanya hivyo? Mfano unasema huwezi kumtosa mwanao jikoni hata dk2 sababu unampenda.
 
Kama aliweza kuwateketeza watu kwa maji nuhu (immagine unakunywa maji mpaka mishipa inachanika unakosa pumzi unakufa) ,moto luti(hapa waliungua si kitoto) , volcano pompeii(italia hiyo hawa mpaka leo wamebaki masanamu ukumbusho kwetu) ,na aliweza kumuhifadhi farao asioze ili awe ukumbusho pia kwetu WE UNADHANI KUKUWEKA MOTONI NI KITU KIGUMU? USIJIFARIJI MKUU FUATA ANAVYOTAKA UISHI UTAUEPUKA HUO MOTO.
Swali kwako: Unaweza kumtosa mwanao kwenye moto hata mdogo tu wa nyumbani na kumwacha ateketetee kwa dk mbili kisa kaasi amri yako ya kuwahi toka shule?
If yes, basi una kichaa.
If No, Je, Mungu umemzidi huruma?.
Use common sense
 
Mimi mwenyewe hainingii akilini.
Mahali fulani Mungu anamuuliza mwanadamu: Je, mwanamke aweza kumsahau mwanawake mwenyewe?
Akajijibu ndio aweza kumsahau, lakini yeye hawezi kumsahau mwanadamu.
Kama upendo wa mama kwa mtoto wake mchanga unapitwa na ule wa Mungu kwa wanadamu. Haiingii akilini kuamini kuwa Mungu atamchoma moto mwanadamu.
 
Swali kwako: Unaweza kumtosa mwanao kwenye moto hata mdogo tu wa nyumbani na kumwacha ateketetee kwa dk mbili kisa kaasi amri yako ya kuwahi toka shule?
If yes, basi una kichaa.
If No, Je, Mungu umemzidi huruma?.
Use common sense
Kama wewe unampenda baba yako unaweza kumdharau kwa maagizo yake ukayapuuza na kumpinga baba yako..?

wewe unapomaliza kula mihogo yale maganda huyatupi unayahifadhi ndani kuonesha upendo wako dhidi ya muhogo..?
 
Walioandika vitabu vya dini walikuwa na akili sana walikuwa na malengo yao. Mafundisho ya kuchomwa moto milele ni mafundisho ya uongo lengo likiwa ni kuwatisha watu wasiendelee kutenda maovu, ni kama kumtisha mtoto asipokula au akiiba utamchoma vidole.

Mafundisho kama haya ndiyo yanatumiwa na wachungaji walio wengi manabii wa uongo wanaoanzisha makanisa kama uyoga ili kujipatia utajiri kwa kuwadanganya waumini kuwa watoapo sadaka wanajiwekea akiba mbinguni, which is not true.

Hakuna moto wa milele wewe tenda mema uishi vizuri na walimwengu basi.
 
Back
Top Bottom