Kama mzazi mwenye akili timamu siwezi kumchoma moto mwanangu hata kwa dk 2, Je, Mungu anaweza kumchoma moto mwanadamu aliyemuumba milele na milele?

Hakuna Jehananamu wala moto wa milele, Mungu alitoa adhabu moja tu kupatwa mauti yaani kifo chako ndo mwisho wako, ukifa kimwili kama ulikuwa na matendo mabovu hutauona ufalme wa mbingu, kama ulikuwa na matendo mema na unatubu kila ukikosea wewe utafurahia maisha baada ya kifo milele kwani utaondolewa adhabu hiyo.
 
Nadhani pamoja na utofauti huo wa mafundisho uliopo kwenye maandiko ya vitabu vya dini...bado lengo la Mungu ni moja tu. Kuuondoa uovu usiwepo milele.

Kumbuka kuwa universe yote ni mali ya Mungu....so hata akiamua kwenda kuwachomea waovu sehemu fulani mbali na duniani....ambako huko wataungua milele, bado hatakuwa ametatua tatizo la dhambi.

Why? Kwa sababu bado waovu hao watakuwa hai milele wakiteketea pasipo kufa. Hivyo bado ktk himaya ya Mungu uovu utaendelea kuwepo kwa vile waovu watakuwa hai milele somewhere wakiungua.

Napenda nijifunze toka kwenye mafundisho ya kitabu unachokiamini...kinasema huo moto wa jehanum utawakia wapi?
Uovi hautakuwepo bali watakuwepo waovu.

Motoni hakutakuwa na uzinzi bali watakuwepo wazinzi ambao watakuwa wanaungua moto na hawatokuwa na mda wa kuwaza uzinzi kutokana na msumivu ya moto.

Hivyo hapo uovu utakuwa hakuna bali watabakia waovu wakiungua moto na kuteseka kwa hali zote na huko Mungu hana huruma kwao huko sifa ya Mungu ya huruma ni kwa watu wema tu.


Kwa hyo hoja yako ya kuwa uovu utaendelea hoja hyo ni ya kubambikiza tu,uovu ili uwepo manake wawepo watu wakifanya hayo maovu,sasa huko hakutakuwa na maovu bali kutakuwa na waovu peke yake.

Mpaka hapo kuna swali mkuu?
 
ni zaidi ya unyama kwa kweli Mungu wetu hawezi kutufanyia hivyo kabisa tena unachomwa moto afu haufi dah! Mungu ni mkuu wa upendo kamwe hawezi kutufanyia kisasi kibaya cha aina hiyo.
 
Hakuna Jehananamu wala moto wa milele, Mungu alitoa adhabu moja tu kupatwa mauti yaani kifo chako ndo mwisho wako, ukifa kimwili kama ulikuwa na matendo mabovu hutauona ufalme wa mbingu, kama ulikuwa na matendo mema na unatubu kila ukikosea wewe utafurahia maisha baada ya kifo milele kwani utaondolewa adhabu hiyo.
Basi watu watatenda maovu wanajua wakifa wamepotea tu hawatalipwa kwa uovu wao.

Na Mungu huyo atakuwa wa kufoji,yabi wewe ubake watoto wa watu,uibe pesa za watu,ule mali za yatima kwa dhuluma alafu ukifa uwe umepotea tu paaap kusikojulikana?

Hahah huyo Mungu atakuwa hatendi haki kabisa
.lazima ufufuke ulipwe matendo yako uliyofabya aisee hamna kukimbia...

Hahah

وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ اللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

[ YUNUS - 27 ]
Na wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watadumu.

Ila kuna ofa Allah ameitoa hii hapa..

إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُولَـٰئِكَ يَتُوبُ اللَّهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا

[ AN-NISAAI - 17 ]
Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima.
 
ni zaidi ya unyama kwa kweli Mungu wetu hawezi kutufanyia hivyo kabisa tena unachomwa moto afu haufi dah! Mungu ni mkuu wa upendo kamwe hawezi kutufanyia kisasi kibaya cha aina hiyo.
Kati ya anayekupiga mpaka ukafa na yule anayekupiga lakini hakupigi pigo la kukuuwa yupi mnyama zaidi ya mwenzie..?
 
Mahali fulani Mungu anamuuliza mwanadamu: Je, mwanamke aweza kumsahau mwanawake mwenyewe?
Akajijibu ndio aweza kumsahau, lakini yeye hawezi kumsahau mwanadamu.
Kama upendo wa mama kwa mtoto wake mchanga unapitwa na ule wa Mungu kwa wanadamu. Haiingii akilini kuamini kuwa Mungu atamchoma moto mwanadamu.
Ni kweli kabisa. Labda uniambie wanachomwa kwa muda fulani alafu wanasamehewa. Ila sio for eternity.
 
Kati ya anayekupiga mpaka ukafa na yule anayekupiga lakini hakupigi pigo la kukuuwa yupi mnyama zaidi ya mwenzie..?

bora akupige ufe maumivu yatakoma kuliko akupige na uendeleee kupata maumivu kila siku ni zaidi ya unyama kaka, naamini Mungu hawezi kutufanyia hivyo kwanza sio makosa yetu. kama angemuangamiza shetani basi dhambi zisingekuwepo duniani.
 
Mungu wa 7 7 huyo mkuu ...achana na hizo esopo .alfu Lela ulela
 
Hahaha hahahahaha Mungu kakasirika my foot

Halafu watu wa zamani sijui Walikuwa hamnazo ..Mtu akijua kufanya mazingaombwe kidogo tu wanamuita Mtume ...
gharika ilikuwa mafuriko tu mkuu na sodoma na gomora ule moto ulisababishwa na mlipuko wa volcano maeneo yale enzi hizo elimu si unajua ilikua ndogo

ni sawa na kupatwa kwa jua watu walichukulia eti ni mungu kakasirika
 
kabisa.. hao wanaosema sijui moto wa milele, hakuna kitu kama hicho, kama Mungu atafanya hivyo basi Mungu wetu hana huruma na upendo kuzidi sie wanadamu wake. Sifa ya Mungu ni huruma na upendo, negativities kwake hakuna.
Really
 
Hivi binadamu ninaetupwa motoni na kuungua bila kuteketea milele na milele ni mimi binadamu niliyepata kuishi kweli katika dunia hii au ni kiumbe kingine tofauti?
Ni swali gumu kwa wasoamini lakini kwa waaminio hakuna kisichowezekana.
 
Wakuu salama?
Muumba na mzazi mwenye mamlaka na uchungu zaidi juu ya mwanadamu ni Mungu muumba.
Yaani kama unamvumilia, kumjali na kumpenda mwana wako basi jua Mungu aliyemuumba anampenda zaidi.
Mwanangu hata afanye kosa gani, maadamu tu nina akili timamu siwezi kumtosa jikoni aungue hata kwa dk 2.
Je, Mungu muumba anaweza kumtupa mwanadamu dhaifu motoni milele na milele?
Je, Mungu hana upendo unaomzidi mzazi?
Nikifungua makabrasha yangu naambiwa kuwa yeye ni zaidi ya mama.
Una moyo mgumu sana mkuu, yote yanayotokea duniani huyaoni wala huyasikii?Mama kumchoma mwanae, kumtumbukiza chooni, kumtupa jalalani,Baba kumchinja mwanae,kumbaka hadi kufa, mume au mke kumuua mwenza wake? achana na hayo,kuna kujinyonga,kujipiga risasi au kujichoma kisu wewe mwenyewe.vipi mkuu huna taarifa kweli?
 
Back
Top Bottom