Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi
Kwa Maslahi ya Taifa ya Leo
Screen Shot 2022-08-07 at 4.58.55 AM.png
Screen Shot 2022-08-07 at 4.59.13 AM.png

Wana JF Wenzangu, hebu tuacheni ushamba!, Media kumpongeza Rais kwa kazi nzuri na kufanya vema, sio kujipendekeza au kujikombakomba kunyemelea uteuzi!, rais wetu pia ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote, akifanya vema, anastahili pongezi as encouragement, aendelee kufanya mazuri zaidi na zaidi, lakini baadhi ya watu humu kiukweli mnakera, sisi watu wa media, kila tukimpongeza rais kwa kufanya vema au mazuri yoyote, mnatuzodoa na kutunyooshea vidole kuwa pongezi hizo ni pongezi za kinafki kujipendekeza tuu ili kusaka uteuzi!.

Tangu rais Samia ameingia madarakani amefanya mengi makubwa mazuri ya kustahili sifa na pongezi za dhati, lakini pia Rais Samia sio malaika, hivyo anaweza kukosea na tutamkosoa!. Hivyo katika mazuri, nami nimempongeza kwa mengi, lakini nakereka kila nikipongeza nabezwa kuwa nafukuzia uteuzi!, hivi watu mnaona pongezi tuu?, critics hamzioni?.

Jana Rais Samia kateua majaji wapya 22 wa mahakama Kuu, katika uteuzi huo majaji 11 ni Wanawake na 11 ni wanaume, nikapandisha bandiko la pongezi Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?
wale wazodoaji wakaniibukia eti ni bandiko la kujipendekeza, eti kwa vile sifa za kuwa jaji ni kuwa na LL.B, na mimi ninayo, sasa naupumulia u Jaji!. Acheni hizo!.

Haya sasa Mungu bariki, mimi niko Mbeya, kwenye maonyesho ya Nane Nane nikifanya Vipindi vyangu vya Nane Nane na PPR, na rais yuko Mbeya, ndiye mgeni Rasmi kwenye kilele cha Nane Nane, hivyo kesho ndio itakuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Rais Samia face to face, tangu Mungu alipomteua kuwa rais wetu, hivyo ikitokea katika pita pita za mabandani. ikitokea akapita karibu yangu, nitamsalimia kwa sauti kubwa tuu na atasikia, sijui kama atajibu, shikamoo yangu...

Declaration of Interest: Pascal Mayalla. hahitaji uteuzi wowote wa hisani wa rais kuwa DC, DED, RAS, RC, JAJI, or anybody!.
ila nikipata fursa ya kumsalimu kwa karibu, nitampa ukweli huu wa jinsi JF mnavyokera kwa kumweleza wazi kuwa pongezi zetu kwake kwa sisi baadhi yetu, ni pongezi bonafide genuine, kumpongeza kwa dhati kabisa kwa mazuri anayolifanyia taifa letu na ku declare interest publically kuwa Mimi Pascal Mayalla, nikipongeza, ni nina pongeza kwa dhati na sihitaji uteuzi wowote licha
  1. Pascal Mayalla ni Mtanzania, anayekidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa na rais kushika wadhifa wowote kama U DC!. Siku zote nimekuwa nikisema sihitaji uteuzi, ila kuna mwana jf mmoja akauliza kama ikitokea ghafla mara pap... Pascal Mayalla umeteuliwa DC, Jee Utakataa?. Nilishindwa kujibu!, Ukiteuliwa ukikataa utaonekana ni mtovu wa nidhamu!. Ili kuzuia utovu wa nidhamu, ni vizuri uki declare interest wazi, openly na publically, Pascal Mayalla hahitaji uteuzi wa kuwa DC!.
  2. Kwenye uteuzi wa Majaji wapya, mmoja wa majaji wapya ni mwandishi wa habari binti, tulimpokea pale RTD, tukamfundisha kazi, akaenda kusoma sheria, akawa wakili wa kujitegemea juzi kateuliwa Jaji. Mimi pia nimesoma sheria, tena LL.B yangu ni LL.B (HONS) ya UDSM, hivyo ninakidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa kuwa Jaji, lakini naomba kukiri, siwezi kumhukumu mtu kifo, hivyo siwezi kuwa Jaji na naomba nisiteuliwe kuwa Jaji!.
Japo Kuna Wengi Wanapenda Uteuzi, Lakini Kuna Watu wa Ajabu!, Hawataki Kabisa Uteuzi wala Kazi za Malipo Manene!.
Kuteuliwa wadhifa wowote na rais wa JMT ni heshima kubwa, hivyo wateuliwa hufurahi kuheshimishwa, hivyo kuna wengi wanautamani sana u DC, U DAS, DED RC etc, amini usiamini, kuna watu fulani ambao hawazimikii kabisa uteuzi wowote wa ubwete!, au kazi za malipo manene!. Watu hao sio tuu ni wazuri at what they do, but they love what they do, and they are the best at what they do, ukiwateua watu hawa na kuwa u DC, japo u DC ni cheo kikubwa, lakini uki compare watakacho fanya kwenye U DC compared to what they do, it's a waste!. Just imagine unamchukua mtu kama Profesa wa Chuo Kikuu kama Prof. Shivji, ateuliwe DC!.

Mimi ni mtu wa mastory mastory, wale wa mastory, tuendelee, wale wa short and clear, nenda mwisho.
The True Story of My Life: Nilitamani Kuwa Wakili, Nikaukosa, Nikawa Mtangazaji, Baadaye Nikasoma Sheria, Sasa ni Wakili, lakini Sio Wakili Msomi, Mimi ni Wakili Mtangazaji!.
Baada ya kukosa sifa za kusomea Sheria, niliingia fani ya utangazaji, nikawa mtangazaji tena mzuri tuu, kwa wale wa zamani wanakijua kipindi changu cha "Kiti Moto", kilichopelekea ile kitu kuitwa kitimoto!.
Siku zote nikawa ni mtangazaji anayeutamani uwakili.

Nilianzia Kazi RTD nikaja TBC, Mwaka 2002 Nikaachishwa Kazi "Siwezi Kazi"!. Siku Hiyo Nilitoka Machozi!.
Malezi mengi ya Kiafrika, tunalelewa kwa kufunzwa mtoto wa kiume huruhusiwi kulia machozi, lazima ujikaze, mambo ya kulia lia ni mambo ya kike ya wanawake!. Lakini binadamu tumeumbwa tofauti tofauti, kuna wanaume wengine wana maxhozi ya karibu!, Huwezi amimi nilipofiwa na Baba Mzazi Mzee Mayalla (RIP) nilikuwa RTD, na sikulia mpaka wakati wa mazishi, lakini siku niliachishwa kazi TBC, nilitoka machozi!.

Kilichonitoa chozi sio kupoteza kazi bali sababu nilizopewa kufukuzwa kazi!. Kiukweli serikali kuna majungu, na kuna wale wenzetu wa kazi mbili, wengine wana roho mbaya za ajabu, na naamini baadhi yao wakifa, kule watanywa kuni!.

Majungu Kunihusu!.
Wazazi wangu wote wawili walikuwa watumishi wa Idara, Baba alifariki siku nyingi, mama aliendelea hadi alipostaafu kwa heshima. kumbe hawa jamaa huwa hawastaafu!. Baba ni Msukuma na mama ni mchagga wa Kurua Vunjo Moshi. Mambo yetu sisi Wasukuma yalimshinda siku nyingi mama wa Kichagga, hivyo baada ya mama kustaafu alirejea kuishi kijijini kwao Kirua Vunjo. Nikiwa TBC, kuna siku mama akaniita haraka kijijini. Ukiitwa kijijini na mzazi mstaafu lazima ushituke!, bikampigia simu mdogo wangu wa kike anayeishi na mama kama mama anaumwa au kuna nini?. Nipoambiwa mama ni mzima, ndio nilizidi kushangaa!. Nikaenda, ndipo mama akanieleza jinsi watu wa kazi kwake wamemfuata kijijini na kumueleza kumhusu mtoto wake Pascal Mayalla pale TBC!.

Naomba nisiseme mama alipelekewa umbeya gani, kiukweli kuna watu ukiwaoni kwa machoni ni kama watu ila mioyoni ni mashetani wakubwa!. Nilipoteza kazi, fomu yangu ya Opras ilichafuliwa vilivyo na kuonyesha sina uwezo!. Ukumbuke ni mtu unatimuliwa kazi kwa kuelezwa kuwa hauna uwezo, huku ni mtangazaji mwenye uzoefu wa miaka 12 kazini!. Nililia!.

Kuanzisha PPR na Kuiingizia TBC Billions!.
Japo kupoteza kazi ni majanga, kuna majanga mengine mtu unakutana nayo japo ni majanga, lakini ni Blessings in Disguise!. Ni kutimuliwa kule kazi TBC kulikopelekea mimi kuanzisha kampuni yangu ya PPR. Nikiwa TBC, mimi ndie mwanzilishi wa matangazo ya Saba Saba, hivyo baada ya kuachishwa kazi, akili ikafungunguka, nikaanzisha kampuni ya matangazo ya PPR, hivyo nikaingia Saba Saba na kufanya vipindi na kuwapelekea hao hao TBC!. Mpaka sasa, sijui kama kuna mtangazaji wao yoyote, aliyewaingizia TBC mapato kama mimi ambaye wakati nikiwa TBC, nilionekana sifai!, lakini baada ya kutimuliwa, nimewaingizia TBC, billions na bado naendelea kuwaingizia mapesa!.

Kusomea Sheria UDSM.
Enzi namaliza sekondari Ilboru ile 1988, ukikosa Dibisheni 1, sahau sheria hata ukiwa bilionea!.
Mwaka huo wa 2002 nilipo timuliwa kazi TBC, UDSM ilikuwa imeanzisha utaratibu kwa Watanzania wenye uwezo wa kujilipia, kujiunga na UDSM, na wakIkidhi sifa na vigezo, wanajiunga kosemea chochote kwa kujilipia!.
Kule kufukuzwa kazi TBC, nikajikuta sasa napata pesa nyingi kuliko ule mshahara wa TBC!, nikawa na uwezo wa kujililipia, nikajiunga UDSM, nikajilipia kusomea sheria ili niwe wakili. Nisinge fukuzwa kazi TBC, nisinge anzisha kampuni, nisinge soma sheria!,

Nimehitimu Sheria, na Kujikuta Napenda Zaidi Utangazaji
Nilihitimu sheria mwaka 2007, huwezi amini hata graduation sikuhudhuria!, kuwa mwanasheria, wakili ni kazi ya heshima kuliko utangazaji na mawakili wa kujitegemea wana make fedha ndefu kuliko uandishi wa habari na utangazaji. Mimi sikujali uwakili bali niliendelea na utangazaji kwasababu its doing what you love!. Hivyo kuna watu wana elimu nzuri, wana vyeti vikubwa, wana fursa za kuajiriwa and make milions, lakini wanaendelea kufanya wanachokipenda hata kama they don't make millions!.

Mimi ni Mwandishi Mzuri, Mtangazaji Mzuri na Naupenda Uandishi, Utangazaji!.
Sifa ya mwandishi mzuri wa habari wa magazeti, ni yule anayeandika vigongo and make headlines, na mwandishi mzuri wa TV ni yule anayeweza kufika kwenye tukio na kuripoti breaking news. Ili uweze kufika eneo la tukio kwa haraka kabisa, ni kutumia usafiri wa pikipiki. Hivyo usafiri wangu mkubwa ni pikipiki. Ile siku ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, ile 1995, ni mimi ndio nilisababisha uchaguzi ukarudiwa baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam, kutoka na kuwa the fastest kupitia vituo vingi na kutanga live.
Tulikuwa tunafanya uchaguzi siku rofauti na uchaguzi wa Zanzibar, ni mimi ndio nilikuwa Zanzibar na nikatangaza kile kitu cha kweli kilichotokea Zanzibar ile 1995!, Ni mimi ndie niliyetangaza kilichotokea kwenye vurugu za Mwembechai!.

Baada ya Mwalimu Nyerere kuacha urais, mimi ndie mwandishi pekee niliyesafiri na Mwalimu kwenye ile mikutano yake ya South South!. Mimi ndie mwandishi pekee wa binafsi Tanzania kwenda St Thomas Hospital kumuona Mwalimu, kisha kumpokea DAR na kumsindikiza hadi Butiama kwenye makao yake ya milele!. Mimi ndiye mwandishi pekee binafsi niliyesafiri na Mkapa na JK na kuripoti UNGA.

Niliweza kuyafanya hayo kwasababu naupenda uandishi nauweza uandishi na utangazaji.

Ajali Mbaya ya Pikipiki na Kazi Ubalozini Uingereza
Mwaka 2008, wakati kama huu wa Nane Nane, kwa kutumia usafiri wa Pikipiki, nilikuwa natangaza maonyesho ya 88 kutoka vituo viwili kwa mpigo, Nane Nane Morogoro, Nane Nane ya Dodoma. Kwa kutumia piki piki yangu, Moro Dodoma ni saa 2 tuu!. Ni katika hii shanting ya 88 kati ya Moro na Dodoma, nikapata ajali mbaya ya pikipiki nikawa confined to a wheelchair for sometime.

Kufuatia hali hiyo, ndipo nikiwa hospitalini nchini India, nikaona Tangazo la Kazi. kupitia Jamiiforums. Wizara ya mambo ya Nje ya Uingereza, FCO, inatafuta Mshauri wa Siasa wa Balozi wa Uingereza. Nikaomba hiyo kazi, njkapata, Mshahara mnene, mnono, kuliko mshahara wa waziri!, mazingira mazuri ya kazi. Hivyo mkiona wengine tunaiheshimu sana jf na kuithamini sana jf, tunaomba mtuelewe!.

Sababu za kuomba kazi ni baada ya kuwa confined to a wheelchair, ikawa utangazaji wa pilika pilika siuwezi tena.
Nikiwa Ubalozi wa Uingereza nikapelekwa kutibiwa Afrika Kusini, nikapona nikasimama tena!, nikauujaribu utangazaji, nikajikuta naweza kuendelea kutangaza, amini usiamini, niliopt kuacha kazi ya milions na heshima kubwa na kurejea kwenye kazi yangu ya utangazaji of which I make nothing compared!. Hivyo watu humu mnaponidhania nautafuta U DC, kiukweli mnaniumiza ni kama mnanitukana!, Pascal Mayalla ateuliwe DC for what?. Kuna watu wanaitamani U DC kwa sababu ya lile Shangingi la VX, GX au V8!, kumbe kuna sisi wengine, japo kwa sasa tunatembelea uba, bolt na daladala, lakini magari yetu ni Range Sport!.

Tofauti Kati ya Pongezi za Ukweli, Bonafide Genuine na Pongezi za Uchawa na Kujikombakomba ni very thin!.
The dividing line kati ya pongezi za kweli kwa Rais wa nchi anapofanya vizuri na pongezi za kujikomba komba ama uchawa, is very thin, namna pekee ya kutofautisha ni pongezi genuine atapongezwa kwa mazuri tuu, lakini akikosea, atakosolewa, lakini pongezi za uchawa, kazi yao ni kupongeza tuu, hata akosee vipi, hawatamkosoa!.

Pascal Mayalla ni Msifiaji na Mpongezaji Mzuri, Ila Pia ni Mkosoaji Mzuri
Kila ninaposifu viongozi, kuna watu wanadhani ninasifu kuwinda uteuzi, na waamini Pasco Mayalla hajalamba uteuzi wowote, kwasababu ya ukosoaji wake. Msifiaji mtafuta uteuzi, kamwe hawezi kukosoa!, Pasco Mayalla alimsifu sana JK, ila pia alimkosoa, alimsifu sana JPM, ila pia alimkosoa hadi JPM akamtania "'Mayalla ni Njaa", na Sasa tunamsifu Samia, na ikitokea akakosea pia tunamkosoa!, kwasababu tunajua Rais Samia ni Binadamu, hivyo hawezi kuwa perfect, hivyo japo hapa namsifu rais Samia, siku akikosea, tunamkosoa kwa heshima na unyenyekevu la lengo la kujenga na sio kumbomoa!, constructive criticism.

Kwa Nini Pasco Mayalla, Hataki Uteuzi Wowote wa Hisani?.
Tanzania ni nchi yetu sote, wazalendo wa kweli, wana wajibu wa kuisaidia nchi yao na viongozi wake, sababu pekee inayosababisha Pascal Mayalla hataki uteuzi wowote ni kwa sababu Pascal Mayalla ni member wa Mhimili wa Nne, huku nilipo, nina isaidia sana nchi yangu na kuwasaidia sana viongozi wangu na nchi yangu kuliko hata nikiteuliwa. Na kuna ma DC waliokuwa wanafanya mambo makubwa mazuri ya kulisaidia taifa kabla hawajateuliwa na baada ya kuteuliwa, now they do nothing!.

Media ni Mhimili Sisi Watu Mhimili wa Media, Kama Unatimiza Majukumu Ya Kimhimili, Unataka Uteuliwe ili Ufanye Nini?.
Serikali zote duniani, zinaundwa na mihimili mitatu ambayo ni rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, ila kuna mhimili wa Nne!. Mhimili huu wa nne ambao sio rasmi, unaitwa “The Fourth Protocol” or “The Fourth Estate”.

Ile mihimili mitatu rasmi, ni rasmi kwasababu ndio iliyomo kwenye katiba, inatambulika na wakuu wa mihimili hiyo wanatambulika rasmi na kuheshimika sana, hawa ni Rais, Spika na Jaji Mkuu, ule mhimili wa Nne kwa vile sio rasmi, sio tuu hautambuliki, bali hauna hata mkuu wa mhimili, lakini mhimili huu upo!.

Mihimili hii mitatu ambayo ni rasmi, inaheshimika na majukumu yake, nguvu yake, , mamlaka yake,na madaraka yake yako wazi yameainishwa kwenye katiba, lakini huu mhimili wan ne usio rasmi. Kwa vile hautambuliki, hivyo nguvu yake, madaraka yake na mamlaka yake hayatambuliki lakini kiukweli yapo na una nguvu fulani kubwa kuliko hata hii mihimili mingine yote ila ngubu hii haijulikani rasmi kwasababu mhimili huu sio rasmi!.

Mhilimili huu wa nne usio rasmi ni “The Media”. Mhimili huu japo haujatajwa rasmi ndani ya katiba yetu, ila kazi za mhimili huu, imetajwa ndani ya Ibara ya 18 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977 chini ya ibara za haki za binaadamu kuwa kila Mtu ana haki ya kupata habari.

Mhimili huu wanne, ndio kiunganishi kikuu cha mihimili ile mitatu na wananchi.

Kuna kitu fulani kikubwa muhimu kuhusu taifa lolote ambacho siku zote kinasahaulika, wengi wakidhani kitu muhimu zaidi kwenye taifa lolote ni taifa lenyewe tuu yaa ni eneo!. Mfano wa Makala hizi za “Kwa Maslahi ya Taifa”, tunapozungumzia maslahi ya taifa hapa tunamaanisha maslahi ya Taifa la Tanzania, hivyo Tanzania ndio inahesabika kuwa ndio kila kitu, kumbe kiukweli kabisa kitu ambacho ndio kila kitu hata kabla ya taifa lenyewe ni watu!, Watanzania!.

Hawa watu, Watanzania, ndio wamiliki wa nchi ya Tanzania, hawa watu, Watanzania ndio wenye ardhi yote ya Tanzania, yaani hii nchi ni mali yao!.

Hawa wananchi wa Tanzania, ndio wenye Katiba ya JMT!. Ukiisoma Katiba ya JMT, ya mwaka 1977, neno la kwanza kwenye katiba ni “We The People” (Katiba iliandikwa kwanza kwa Kiingereza ndipo ikatafasiriwa kwa Lugha ya Kiwahili).

Hivyo kitu muhimu cha kwanza ni watu, ndio wenye nchi, ndio wenye katiba, hivyo ndio wenye hii mihimili yote mitatu rasmi na huu mhimili wan ne usio rasmi.

Mhimili huu wanne usio rasmi, ndio mhimili kiunganishi kati ya mihimili hiyo mitatu ya rasmi ya dola na wananchi, ni sisi waandishi wa habari ndio tunawapelekea taarifa za kutoka mihimili yote mitatu na kuwafikia wananchi, na kukitokea jambo lolote kutoka kwa wananchi kwenda kwa serikali yao, ni sisi tena waandishi wa habari, tunawafikishia serikali mrejesho kutoka kwa wananchi, hivyo mhimili huu wan ne ndio mhimili muhimu kuliko hata hiyo mihimili mitatu rasmi!.

Kazi rasmi za media, za kitradisheno ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, lakini kazi za media za kisasa, haziishii kuhabarisha kuelimisha na kuburudishwa, media ya kisasa ndio the watchdog of the society, yaani mbwa wa ulinzi wa jamii, hii mihimili mitatu ikikosea ni sisi mhimili wanne ndio wenye uwezo wa kukosoa na kuisaidia jamii.

Kule kwa wenzetu nchini Marekani, mhimili huu unaheshimiwa sana na umejijengea heshima kubwa kufikia kiwango cha kumshikia bango rais mmoja wa Marekanim Rais Gerald Ford wa Marekani aliyefanya makosa fulani kwenye uchaguzi wa Marekani kwa gazeti la The Washington Post kuripoti kashfa iliyoitwa kashfa ya Watergate, kuliko mlazimisha rais huyo afungashe virago vyake na kuikimbia Ikulu ya Marekani, hivyo ni media ndio ilimpopoa na kumtupa pembeni.

Hata hapa nchini kwetu, sisi media tunafanya kazi kubwa nzuri ya kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha, kukosoa, na kushauri, kupitia tahariri, maoni ya wahariri na makala mbalimbali elimishi zinazoandikwa na waandishi manguli, mimi mwana safu wenu Paskali Mayalla, nikiwa ni mmoja wao. Hivi hizi kazi zetu za uhabarishaji, uelimishaji, uburudishaji, ukosoaji, ni huduma nzuri kwa taifa kuliko uteuzi wowote.
Rais wetu Mama Samia, ameonyesha kwa kauli, maneno na matendo kuwa yeye ni mtu msikivu, na kuna mazuri mengi ameyafanya na anaendelea kuyafanya, yanayostahili pongezi. Sisi watu wa media, tukiandika jambo lolote zuri kumpongeza rais Samia kwa mazuri yake, tunanyooshewa vidole kuwa tunanyemelea uteuzi wa UDC, U RC au Ukurugenzi yaani U RAS au U DAS!. Kwa vile mimi ni Mtanzania na nina sifa za kustahili kuteuliwa nafasi yoyote ya uteuzi, kwa sababu ni haki yangu, kama Mtanzania, naomba ku declare publically kuwa mimi Pascal Mayalla, sipongezi kwa kutafuta uteuzi wowote wa u DC au u RC au Ukurugenzi, au uteuzi wowote wa Mama!.

Na kwa vile mimi niko Mbeya kwenye Nane Nane, na Mama Samia pia yuko Mbeya kuja kufunga Nane Nane, hapo kesho, ikitokea nikakutana na Mama Samia kesho kwenye Nane Nane,
Simulation ya encounter ya Pasco na Mama Samia
PM:“Sjikamoo Mama!...
RS : Marhaba Mwanangu.
PM: Nina Salaam zako kutoka JF!, akisimama, then nitampa salaam zake,
Asiposimama, then salaam zangu zitakuwa zimeishia hapo!.

Ikitokea amesimama, then nitampongeza kwa kazi nzuri!, na Tatu nitampa salamu zenu wana jf, na mimi Pascal Mayalla kumtamkia mama kuwa sitaki uteuzi wowote!.
Namna ya kukutana na kuzungumza na rais Samia hapo kesho ni kwa kutumia kitu kinachoiitwa na power of mind suggestibility, kama niliotumia hapa

Kesho ni zamu ya Rais Samia

Wasalaam.

Paskali.
 
Mama ni moja ya viongozi wachache duniani ambao ni waadilifu wasiopenda kabisa dhulma. Hilo pekee linamfanya awe kiongozi bora. Ijapokuwa kuisimamisha haki huhitaji ushirikiano wa watu wengi, kwa kuanzia kuwa na rais muadilifu ni hatua muhimu.

Tukiachana na hiyo, hivi waliochukua fomu wamefikia wangapi brother P. Nilikuwa busy sijapata updates.
 
Dah unaharibu. Rais Samia hana uthubutu, amezungukwa na genge la wahuni wezi
 
Wanabodi
Kwa Maslahi ya Taifa ya Leo
View attachment 2316635View attachment 2316636
Wana JF Wenzangu, tuacheni ushamba!, Media kumpongeza Rais kwa kazi nzuri na kufanya vema, kufanya vema, sio kujipendekeza kunyemelea uteuzi!, rais wetu pia ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote, akifanya vema, anastahili pongezi as encouragement, aendelee kufanya mazuri zaidi na zaidi, lakini baadhi ya watu humu kiukweli mnakera, sisi watu wa media, kila tukimpongeza rais kwa kufanya vema au mazuri yoyote, mnatuzodoa na kutunyooshea vidole kuwa pongezi hizo ni pongezi za kinafki kujipendekeza tuu ili kusaka uteuzi!.

Tangu rais Samia ameingia madarakani amefanya mengi mazuri ya kustahili pongezi za dhati, nami nimempongeza kwa mengi, lakini nakereka kila nikipongeza nabezwa kuwa nafukuzia uteuzi!.

Haya sasa Mungu bariki, mimi niko Mbeya, kwenye maonyesho ya Nane Nane nikifanya Vipindi vyangu vya Nane Nane na PPR, na rais yuko Mbeya, ndiye mgeni kwenye kilele cha Nane Nane, hivyo kesho ndio itakuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Rais Samia face to face, tangu Mungu alipomteua kuwa rais wetu, hivyo ikitokea katika pita pita za mabandani. ikitokea akapita karibu yangu, nitamsalimia kwa sauti kubwa tuu na atasikia, sijui kama atajibu, shikamoo yangu...

Declaration of Interest: Pascal Mayalla. hahitaji uteuzi wowote wa hisani wa rais kuwa DC, DED, RAS, RC, JAJI, or anybody!.
ila nikipata fursa ya kumsalimu kwa karibu, nitampa ukweli huu wa jinsi JF mnavyokera kwa kumweleza wazi kuwa pongezi zetu kwake kwa sisi baadhi yetu, ni pongezi bonafide genuine, kumpongeza kwa dhati kabisa kwa mazuri anayolifanyia taifa letu na ku declare interest publically kuwa Mimi Pascal Mayalla, nikipongeza, ni nina pongeza kwa dhati na sihitaji uteuzi wowote licha
  1. Pascal Mayalla ni Mtanzania, anayekidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa na rais kushika wadhifa wowote kama U DC!. Siku zote nimekuwa nikisema sihitaji uteuzi, ila kuna mwana jf mmoja akauliza kama ikitokea ghafla mara pap... Pascal Mayalla umeteuliwa DC, Jee Utakataa?. Nilishindwa kujibu!, Ukiteuliwa ukikataa utaonekana ni mtovu wa nidhamu!. Ili kuzuia utovu wa nidhamu, ni vizuri uki declare interest wazi, openly na publically, Pascal Mayalla hahitaji uteuzi wa kuwa DC!.
  2. Kwenye uteuzi wa Majaji wapya, mmoja wa majaji wapya ni mwandishi wa habari binti, tulimpokea pale RTD, tukamfundisha kazi, akaenda kusoma sheria, akawa wakili wa kujitegemea juzi kateuliwa Jaji. Mimi pia nimesoma sheria, tena LL.B yangu ni LL.B (HONS) ya UDSM, hivyo ninakidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa kuwa Jaji, lakini naomba kukiri, siwezi kumhukumu mtu kifo, hivyo siwezi kuwa Jaji na naomba nisiteuliwe kuwa Jaji!.
Japo Kuna Wengi Wanapenda Uteuzi, Lakini Kuna Watu wa Ajabu!, Hawataki Kabisa Uteuzi wala Kazi za Malipo Manene!.
Kuteuliwa wadhifa wowote na rais wa JMT ni heshima kubwa, hivyo wateuliwa hufurahi kuheshimishwa, hivyo kuna wengi wanautamani sana u DC, U DAS, DED RC etc, amini usiamini, kuna watu fulani ambao hawasimikii kabisa uteuzi!, au kazi za malipo manene!. Watu hao sio tuu ni wazuri at what they do, but they love what they do, and they are the best at what they do, ukiwateua watu hawa na kuwa u DC, japo u DC ni cheo kikubwa, lakini uki compare watakacho fanya kwenye U DC compared to what they do, its a waste!. Just imagine unamchukua Profesa wa Chuo Kikuu kama Prof. Shivji, ateuliwe DC!.
Mimi ni mtu wa mastory mastory, wale wa mastory, tuendelee, wale wa short and clear, nenda mwisho.

Rais wetu Mama Samia, ameonyesha kwa kauli na vitendo kuwa yeye ni mtu msikivu, na kuna mazuri mengi ameyafanya na anaendelea kuyafanya, yanayostahili pongezi. Sisi watu wa media, tukiandika jambo lolote zuri kumpongeza rais Safia kwa mazuri yake, tunanyoosjewa vidole ku3wa tunanyemelea uteuzi wa UDC, U RC au Ukurugenzi yaani U RAS au U DAS!. Kwa vile mimi ni Mtanzania na nina sifa za kustahili kuteuliwa nafasi yoyote ya uteuzi, kwa sababu ni haki yangu, kama Mtanzania, naomba ku declare publically kuwa mimi Pascal Mayalla, sipongezi kwa kutafuta uteuzi wowote wa u DC au u RC au Ukurugenzi, au uteuzi wowote wa Mama!.

Na kwa vile mimi niko Mbeya kwenye Nane Nane, na Mama Samia pia yuko Mbeya kuja kufunga Nane Nane, ikitokea nikakutana na Mama Samia kesho kwenye Nane Nane, Kwanza nitamsalimia, “Sjikamoo Mama!...

Pili nitampongeza kwa kazi nzuri!, na Tatu nitampa salamu zenu wana jf, na mimi Pascal Mayalla kumtakia mama kuwa sitaki uteuzi wowote!.
Namna ya kukutana na kuzungumza na rais Samia hapo kesho ni kwa kutumia kitu kinachoiitwa na power of mind suggestibility, kama niliotumia hapa

na hapa

Wasalaam.

Paskali.
Hongera sana Pascal Mayalla
 
Wewe ukizungukwa na kundi la wahalifu usiku, maana yake wewe ni muhalifu, au inatakiwa watu wewe wajitokeze kukusaidia?
Umenena vyema kabisa tena una hekima. Ukizungukwa na wezi au wahari wewe siyo mharifu na ndiyo maana tunasema Rais Samia ni mtu safi mwenye maono na nchi na ni rais mwenye exposures na ameishi maisha ya watanzania. Wezi na majambazi yanamfanya ashindwe kutoka kufanya yale watanzania wanahitaji
 
Tuacheni ushamba??!!
Labda wewe msaka teuzi ndio mshamba.!
 
Hahaaa huyu mzee amezeeka vibaya sana.
CCM haina hata huruma na inawafanya watu kuwa mazezeta wazee kwa vijana kusujudia teuzi uchwara. Tulio bakia na Akili timamu ni wachache sana tunawaona akina Paschal ni njaa kali wanateseka.
Nchi hii ina ardhi kubwa na fursa kede kede lakini ccm imewafumba macho na kuwafanya watu kuwa mazezeta kutwa kucha hayataki kufanya kazi kwa bidii kujiletea maendeleo yanasubiri kujikomba komba kulamba makalio ya watu wapatate kuteuliwa. Huu ni utumwambaya sana.
Maendeleo hayana Vyamaa.
 
Kuwasifu na kujipendekeza kwa walamba asali ilihali wewe unaambulia kumeza mate na kujaza gesi tumboni hakuna faida!

Rais anafanya majukum yake, hakuna sababu ya kumsifia sifia kwenye kila kitu.
Sina uhakika sana kama na nchi nyingine wana tabia kama hizi za watz (anaupiga mwingi) Kama ni sehemu ya majukumu yake na anapata posho kwanini kusifia sifia? Au anajitolea??

Kuna watumishi wa umma wanakesha na kutokwa jasho kwa mshahara kiduchu kwa maslahi ya taifa; ni nani anawajali na kuwasifia? Zaidi tunasema ni majukumu yao!

Mwacheni afanye majukumu yake. Sifa haziondoi ukweli!
 
Mpaka mkeka wa Madas ma ded na DC upite tutashuhudia mengi mno.

Kumsifia Rais sio jambo baya.

Kumkosoa Rais sio jambo baya.

Wala hakuhitaji uandike uzi ili ueleweke.

Ni mambo yanayoeleweka kabisa.

Ila sasa kila kitu ni kwa kiasi.

Ukisifia sana lazima tujiulize na vile vile ukikosoa sana.
 
Wanabodi
Kwa Maslahi ya Taifa ya Leo
View attachment 2316635View attachment 2316636
Wana JF Wenzangu, tuacheni ushamba!, Media kumpongeza Rais kwa kazi nzuri na kufanya vema, kufanya vema, sio kujipendekeza kunyemelea uteuzi!, rais wetu pia ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote, akifanya vema, anastahili pongezi as encouragement, aendelee kufanya mazuri zaidi na zaidi, lakini baadhi ya watu humu kiukweli mnakera, sisi watu wa media, kila tukimpongeza rais kwa kufanya vema au mazuri yoyote, mnatuzodoa na kutunyooshea vidole kuwa pongezi hizo ni pongezi za kinafki kujipendekeza tuu ili kusaka uteuzi!.

Tangu rais Samia ameingia madarakani amefanya mengi mazuri ya kustahili pongezi za dhati, nami nimempongeza kwa mengi, lakini nakereka kila nikipongeza nabezwa kuwa nafukuzia uteuzi!.

Haya sasa Mungu bariki, mimi niko Mbeya, kwenye maonyesho ya Nane Nane nikifanya Vipindi vyangu vya Nane Nane na PPR, na rais yuko Mbeya, ndiye mgeni kwenye kilele cha Nane Nane, hivyo kesho ndio itakuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Rais Samia face to face, tangu Mungu alipomteua kuwa rais wetu, hivyo ikitokea katika pita pita za mabandani. ikitokea akapita karibu yangu, nitamsalimia kwa sauti kubwa tuu na atasikia, sijui kama atajibu, shikamoo yangu...

Declaration of Interest: Pascal Mayalla. hahitaji uteuzi wowote wa hisani wa rais kuwa DC, DED, RAS, RC, JAJI, or anybody!.
ila nikipata fursa ya kumsalimu kwa karibu, nitampa ukweli huu wa jinsi JF mnavyokera kwa kumweleza wazi kuwa pongezi zetu kwake kwa sisi baadhi yetu, ni pongezi bonafide genuine, kumpongeza kwa dhati kabisa kwa mazuri anayolifanyia taifa letu na ku declare interest publically kuwa Mimi Pascal Mayalla, nikipongeza, ni nina pongeza kwa dhati na sihitaji uteuzi wowote licha
  1. Pascal Mayalla ni Mtanzania, anayekidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa na rais kushika wadhifa wowote kama U DC!. Siku zote nimekuwa nikisema sihitaji uteuzi, ila kuna mwana jf mmoja akauliza kama ikitokea ghafla mara pap... Pascal Mayalla umeteuliwa DC, Jee Utakataa?. Nilishindwa kujibu!, Ukiteuliwa ukikataa utaonekana ni mtovu wa nidhamu!. Ili kuzuia utovu wa nidhamu, ni vizuri uki declare interest wazi, openly na publically, Pascal Mayalla hahitaji uteuzi wa kuwa DC!.
  2. Kwenye uteuzi wa Majaji wapya, mmoja wa majaji wapya ni mwandishi wa habari binti, tulimpokea pale RTD, tukamfundisha kazi, akaenda kusoma sheria, akawa wakili wa kujitegemea juzi kateuliwa Jaji. Mimi pia nimesoma sheria, tena LL.B yangu ni LL.B (HONS) ya UDSM, hivyo ninakidhi sifa na vigezo vya kuteuliwa kuwa Jaji, lakini naomba kukiri, siwezi kumhukumu mtu kifo, hivyo siwezi kuwa Jaji na naomba nisiteuliwe kuwa Jaji!.
Japo Kuna Wengi Wanapenda Uteuzi, Lakini Kuna Watu wa Ajabu!, Hawataki Kabisa Uteuzi wala Kazi za Malipo Manene!.
Kuteuliwa wadhifa wowote na rais wa JMT ni heshima kubwa, hivyo wateuliwa hufurahi kuheshimishwa, hivyo kuna wengi wanautamani sana u DC, U DAS, DED RC etc, amini usiamini, kuna watu fulani ambao hawasimikii kabisa uteuzi!, au kazi za malipo manene!. Watu hao sio tuu ni wazuri at what they do, but they love what they do, and they are the best at what they do, ukiwateua watu hawa na kuwa u DC, japo u DC ni cheo kikubwa, lakini uki compare watakacho fanya kwenye U DC compared to what they do, its a waste!. Just imagine unamchukua Profesa wa Chuo Kikuu kama Prof. Shivji, ateuliwe DC!.
Mimi ni mtu wa mastory mastory, wale wa mastory, tuendelee, wale wa short and clear, nenda mwisho.

Rais wetu Mama Samia, ameonyesha kwa kauli na vitendo kuwa yeye ni mtu msikivu, na kuna mazuri mengi ameyafanya na anaendelea kuyafanya, yanayostahili pongezi. Sisi watu wa media, tukiandika jambo lolote zuri kumpongeza rais Safia kwa mazuri yake, tunanyoosjewa vidole ku3wa tunanyemelea uteuzi wa UDC, U RC au Ukurugenzi yaani U RAS au U DAS!. Kwa vile mimi ni Mtanzania na nina sifa za kustahili kuteuliwa nafasi yoyote ya uteuzi, kwa sababu ni haki yangu, kama Mtanzania, naomba ku declare publically kuwa mimi Pascal Mayalla, sipongezi kwa kutafuta uteuzi wowote wa u DC au u RC au Ukurugenzi, au uteuzi wowote wa Mama!.

Na kwa vile mimi niko Mbeya kwenye Nane Nane, na Mama Samia pia yuko Mbeya kuja kufunga Nane Nane, ikitokea nikakutana na Mama Samia kesho kwenye Nane Nane, Kwanza nitamsalimia, “Sjikamoo Mama!...

Pili nitampongeza kwa kazi nzuri!, na Tatu nitampa salamu zenu wana jf, na mimi Pascal Mayalla kumtakia mama kuwa sitaki uteuzi wowote!.
Namna ya kukutana na kuzungumza na rais Samia hapo kesho ni kwa kutumia kitu kinachoiitwa na power of mind suggestibility, kama niliotumia hapa

na hapa

Wasalaam.

Paskali.
Kwahiyo wewe unaona mema tu? Mbona hujawahi kuona mabaya ukayasema? Au hakuna mabaya? Sisi sio wajinga kama unavyofikiri
 
Mkuu Paskal heshima kwako......ukirudi Dar ukitulia tujadili na kuchambua yanayoendelea bandarini .....ubinafsishaji operation za bandari na kwisha mkataba ticts....miaka waliyopewa wamefanya kwa weledi ? Watapewa mkataba mpya ? Naona kama tumelisahau hilo muhimu sana kwa Taifa....asante
 
Kuwasifu na kujipendekeza kwa walamba asali ilihali wewe unaambulia kumeza mate na kujaza gesi tumboni hakuna faida!

Rais anafanya majukum yake, hakuna sababu ya kumsifia sifia kwenye kila kitu.
Sina uhakika sana kama na nchi nyingine wana tabia kama hizi za watz (anaupiga mwingi) Kama ni sehemu ya majukumu yake na anapata posho kwanini kusifia sifia? Au anajitolea??

Kuna watumishi wa umma wanakesha na kutokwa jasho kwa mshahara kiduchu kwa maslahi ya taifa; ni nani anawajali na kuwasifia? Zaidi tunasema ni majukumu yao!

Mwacheni afanye majukumu yake. Sifa haziondoi ukweli!
Nataman kuona jina lako kwenye list ya ma DC wapya.

#Maendeleo hayana Chama.
 
Back
Top Bottom