Kama kweli Mungu anaangalia moyo tu na sio mavazi, kwanini basi watu wasitembee uchi tu?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,153
Kumekuwa ni mtizamo tofauti kuhusu mavazi hususani kwa wanawake katika jamii zinazoamini katika Mungu, mahususi kwa waamini wa kikristo. Moja ya mtizamo unaokuwa kwa kasi ni wanawake kutaka kuvaa mitindo yoyote ya mavazi pasipo kuzingatia staha na heshima kwa hoja kuwa Mungu haangalia mavazi bali anaangalia moyo tu!

Sasa katika kuipinga hoja hiyo, nimeuliza hili swali, kama Mungu anaangalia moyo tu na hana muda wala sababu ya kuangalia namna ulivyovaa kama kunakusitiri, kunamrudishia utukufu na kumjengea heshima, kwanini watetezi wa hiyo hoja wasije na uhalali wa kutetea kutembea uchi tu, maana wanadai Mungu hana muda na kuvaa kwao bali mioyo yao?

Kwanini watetezi wa kuvaa chochote hawataki kuweka msisitizo wa watu kutembea uchi?
Okay basi, wavae hata chupi tu na watembee barabarani, waingie kwenye nyumba za ibada nk.

NOTE:
Mungu alitupa akili, hekima na busara ili tuweze kuzitumia katika kuishi kwetu na mwisho tumrudishie utukufu yeye.
 
Wengi tu wanatembea uchi, labda huna macho ya kuwaona tu.

Wewe tembea tu uchi, hatukuingilii.
 
Wengi tu wanatembea uchi, labda huna macho ya kuwaona tu.

Wewe tembea tu uchi, hatukuingilii.
Mpaka sasa bado sijawaona watu wakitembea uchi hadharani, wakiingia kwenye nyumba za ibada nk. Wapo wanaokuwa robo uchi, nusu uchi, sasa hao watu wanatengeneza hoja dhaifu ya kuwa rohoni wako safi na mavazi sio kitu chochote mbele ya muumba wao. Sasa vipi wasitembee tu uchi ili hoja yao iwe na mashiko kamili? Kwanini bado wanajishtukia kimtindo katika kuvaa kwao?
 
Wewe usifate washamba hao, tembea tu uchi.
 
Kumekuwa ni mtizamo tofauti kuhusu mavazi hususani kwa wanawake katika jamii zinazoamini katika Mungu, mahususi kwa waamini wa kikristo. Moja ya mtizamo unaokuwa kwa kasi ni wanawake kutaka kuvaa mitindo yoyote ya mavazi pasipo kuzingatia staha na heshima kwa hoja kuwa Mungu haangalia mavazi bali anaangalia moyo tu!

Sasa katika kuipinga hoja hiyo, nimeuliza hili swali, kama Mungu anaangalia moyo tu na hana muda wala sababu ya kuangalia namna ulivyovaa kama kunakusitiri, kunamrudishia utukufu na kumjengea heshima, kwanini watetezi wa hiyo hoja wasije na uhalali wa kutetea kutembea uchi tu, maana wanadai Mungu hana muda na kuvaa kwao bali mioyo yao?

Kwanini watetezi wa kuvaa chochote hawataki kuweka msisitizo wa watu kutembea uchi?
Okay basi, wavae hata chupi tu na watembee barabarani, waingie kwenye nyumba za ibada nk.

NOTE:
Mungu alitupa akili, hekima na busara ili tuweze kuzitumia katika kuishi kwetu na mwisho tumrudishie utukufu yeye.
Mungu anaangalia mavazi pia. Makuhani wa Kiyahudi waliambiwa wavae nguo ya kuficha tupu zao wanapoelekea hekaluni.

Marafiki zake watatu wa Danieli walitupwa katika tanuru la moto hali wakiwa wamevaa majoho/kanzu na suruali, kwanini suruali? Je majoho na kanzu hazikutosha? Ni kwasababu walijua kanuni ya Mungu ya kuangalia mavazi na kuficha tupu zao.

Wengi wamechanganya sana ule mstari wa Biblia pale ambapo Mungu alimwambia Samueli kuwa anaangalia moyo, pale Mungu akimuambia Samueli haangalii body structure ya mtu wala uzuri wake ila moyo, hakugusia mavazi kabisa kwasababu Wayahudi walijua kanuni ya mavazi. Mavazi lazima yafiche tupu zao na uchi wao.
 
Mtume Paulo alijua kanuni ya Mungu kuhusu mavazi akawaambia wanawake kuhusu hili:
1 Timotheo 2:9-10
[9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
In like manner also, that women adorn themselves in modest apparel, with shamefacedness and sobriety; not with broided hair, or gold, or pearls, or costly array;
[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
But (which becometh women professing godliness) with good works.

Mavazi ya kusitiri ni muhimu sana kwa jinsi zote kuliko kuvaa hereni ama dhahabu ama cheni.
 
Hizo ni Hila za shetani.

Imeandikwa itoeni miili yenu iwe dhabibu takatifu ya kumpendeza Mungu.

Ikiwa Mungu aliwafunika Adam na eve Kwa ngozi ya mnyama,kwann Wana wa Mungu watembee nusu uchi.

Pia imeandikwa hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Mungu?

Iweje hekalu la Mungu liwe mlango wa kuwafanya wakuonao watamani zinaa Badala ya kuvutwa waokoke Kwa mwonekano wako wa Heshima?

Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom