Jensen salamone
JF-Expert Member
- Sep 28, 2019
- 320
- 639
Awali kabla ya ujio wa wazungu Waafrika hatukuwahi kujua kitu kinachoitwa nguo. Na haya mavazi tunayovaa kufunika mwili mzima ni utamaduni tumeiga toka kwa wazungu.
Sisi Waafrika mavazi yetu makuu yalikuwa ni magome ya miti, majani na ngozi za wanyama tena katika uvaaji tulikuwa tunastiri sehemu nyeti tu huku sehemu kubwa ya mwili ikibaki wazi(uchi).
Hivyo mamlaka zinapowachukulia hatua wanaovaa nusu uchi kwa madai kwamba wanakiuka maadili ya Kitanzania ni ukatili na uonevu.
Ukweli ni kwamba wote wanaovaa nusu uchi wana enzi utamaduni wa Kiafrika kwa vitendo ndio maana Wamasai na Wahadzabe wameendelea kuenzi utamaduni huo.
Kwahiyo ikiwa mamlaka zinazohusika na maadili zinaona kuvaa nusu uchi ni kinyume na maadili ya kitanzania, tunaziomba zianze kwa kuwakamata Wamasai wanaozunguka mitaani wakiwa wamevaa lubega huku wakiacha vimapaja nje na sio kuonea akina Amber Lulu, Gigy na mastaa wengine ambao kimsingi wana enzi utamaduni wa Mwafrika kwa vitendo.