Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,889
Zingatia maneno haya hekima ya watawala
Tunapoenda shule kufunzwa tunaenda kufuta ujinga na kujifunza maarifa mapya ili tuweze kuishi vema kwenye dunia yenye muingiliano wa imani tamaduni na mila tofauti tofauti
Kila jamii ili iweze kuishi kwa amani, uhuru na muingiliano na jamii zingine hujitungia na kujiwekea sheria kanuni na taratibu mbalimbali kulingana na mahitaji ya nyakati.. Ukamilifu na ustawi wa hizi sheria ndani ya Jamii husika huwezeshwa na hekima ya viongozi waliokasimiwa kuongoza wengine
Kwahiyo hekima ya hali ya huu huhitajika popote penye sheria kanuni na taratibu toka kwa kiongozi husika
Tanganyika kwa sehemu kubwa kiutamaduni inabebwa na utambulisho wa jamii ya wamasai kwa sehemu kubwa huku wakifuatiwa na Wakwavi Wasandawe nk! Hawa pamoja na wimbi kubwa la elimu za wageni lakini wameweza kulinda utamaduni wao hadi leo hii.. Wanastahili pongezi kubwa!
Kwahiyo popote alipo Mmasai ni kielelezo cha utamaduni asilia usiochakachuliwa na kivutio kikubwa cha utalii kupitia
Kusokota nywele kwa mtindo wa sangita
Ndonya usoni
Kutoboa masikio
Mapambo ya shanga
Mavazi ya mashuka
Viatu vya kubazi za asili
Mshipi wa ngozi halisi ya mnyama
Sime
Rungu
Fimbo
Pamoja na kwamba kubeba sime rungu na fimbo kiasili ilikuwa ni kwa ajili ya kujilinda na kuonesha ukakamavu lakini hivyo vifaa vimekuwa sehemu muhimu ya utamaduni wao na kichocheo kikubwa cha utalii.. Na ni mara chache mno huzitumia vibaya hizo zana
Kuna kitu kinaitwa urithi wa dunia hiki kimeletwa maalum kwa ajili ya kulinda maeneo, jamii, mimea na vitu vyote vilivyo katika kitisho cha kutoweshwa na dunia ya usasa .. Wamasai wanaingia huko!
Hivyo basi pamoja na sheria ya kutotembea na silaha visiwani Zanzibar lakini kuna hii hekima ya kujali na kuheshimu utamaduni wa wengine..
Wamasai Zenji si kitisho cha usalama kwa kutembea na sime zao zilizo kwenye ala wala fimbo wala rungu.. Hawa ni kivutio cha utalii na wanasaidia kuingiza mapato
Je sheria ya kuvaa almost nusu uchi inasemaje Zenji? Mbona hii inavumuliwa kwa watalii? Lakini inabomoa maadili ya Mzanzibari kwa sehemu kubwa sana ila mamlaka ziko kimya kabisa! Kwanini?
Kitisho kikubwa kabisa Zenji kwa sasa sio Wamasai na sime zao bali ni ushoga kwa vijana wa kiume, ulawiti, usagaji, ubakaji, biashara ya ngono na madawa ya kulevya!
Lakini cha kushangaza mamlaka badala ya kushughulika na haya ya msingi zimebaki kuwashughulikia wamasai wachache na rungu zao zisizoathiri Jamii..
Je mamlaka za Zenji zina masilahi gani kwenye
Ushoga?
Ulawiti?
Usagaji?
Ubakaji?
Biashara ya ngono?
Madawa ya kulevya?
Sent using Jamii Forums mobile app