Baadhi ya mambo ambayo jamii huona ni uhuni lakini yana faida kubwa kwa Afya zetu

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
Na Kenge,

Katika jamii kuna mambo ambayo kwa namna moja au nyingine yanaonekana ni uhuni au kinyume na maadili na tamaduni zetu.Lakini kimsingi mambo hayo ni muhimu na yanasaidia sana katika jamii.Ni vile kundi la watu wachache wanaofanya mambo hayo yasikubalike.

1. Massage
20230823_011039.jpg

Massage ni kinga na Tiba moja nzuri sana kwa mwanadamu.Tupo kwenye Tukirudi darasani kusoma Baiolojia tutakuta mwanadamu yupo ktk kingdom ya wanyama,Kundi Mamalia na soishi ya Vertabrates.Verterbrate ni viumbe wenye UTI wa mgongo.

Uti wa mgongo ni makutano ya mishipa ya fahamu(nyuzi) kutoka maeneo mbalimbali ya mwilini.UTI unamifula laini iitwayo verterbrae ambazo ni kama visahani,Mifupa hii ni milaini kiasi kwamba ni rahisi kuathirika na shughuli mbalimbali tuzifanyazo kama vile kazi,kutembea,kukimbia,kukaa.

Sasa baada ya shughuli nyingi za siku nzima kama ukijijengea ratiba ya kufanya massage hakika Afya yako itaimarika zaidi.Kwa bahati mbaya sehemu za kufanyia massage(Massage Pallor) zimegeuka madanguro huwezi kuingia kama Nia yako ni kupata massage tu kuna huduma nyeusi zinafanyika mule ndani ambapo uwezi kutoka salama hasa kwa wanaume.Hii inafanya massage ionekane ni uhuni.

2. Kuogelea Swimming pool
Mara nyingi nchi zilizoendelea kipaumbele cha nyumba ni pamoja na kuwepo bwawa la kuogelea. Kuoga/kuogelea ni Tiba na kinga nyingine nzuri sana kwa Afya ya mwanadamu

20230823_011400.jpg

Hakuna nyumba yenye Swimming pool watu wake wakafa kwa Presha,Shinikizo la damu,Kisukari na magonjwa mengine mengi labda kama hawaogelei.

Kuogelea ni zoezi la cardio linaupa mwili Aerobic respiration(Oxygen nyingi) ambayo huimarisha Cell za mwili na kuuweka mwili sawa.

Pia kuogelea huifanya ngozi kuwa laini na yakuvutia. Kwa bahati mbaya Jamii zetu wakiona mtu amejenga bwawa utasikia "watoto watafia humo" mara "Ile nyumba wanajifanya wazungu "

Licha ya hayo baadhi ya watu hawaheshimu maadili ya mavazi hasa wanawake hivyo kupelekea jamii kuona(kuogelea) ni uhuni .

3. Kwenda gym

20230823_011250.jpg

Kuweka mwili vizuri inahitaji mazoezi ya kutosha hasa kwa wanaume.Kama ni mgeni ukienda gym utakutana na Trainer atakupa muongozo na vitu hatari kama vile baadhi ya mikao inayoweza kusababisha maumivu wakati unanyanyua vitu vizito..

Kwa bahati mbaya jamii yetu inatazama kama kwenda GYM nao ni uhuni.Na kwa jinsia KE ukienda gym utaonekana unatafta mabwana watunisha misuli na mambo kama hayo.

Licha ya kuwepo vijana ambao nao hawana uelewa zaidi ya faida za mazoezi ya GYM kazi yao wanataka kupata mwili mzuri wa mapenzi mfano six packs,Kifua,Sholder hawa utakuta wanashinda GYM siku nzima ndio sababu jamii inaona kwenda GYM ni uhuni.

4. Kushiriki marathon

20230823_011534.jpg

Kwasasa kuna makongamano mbalimbali kutoka kwa taasisi au kampuni.Zinahamasisha kukimbia jogging. Lengo likiwa ni kuhamasisha watu kufanya maziezi.

20230823_011719.jpg

Lakini jamii imepokea ujumbe huo kitofauti kwani wengi wanaoshiriki marathon hizi wanaonekana kama wahuni.

Yapo mambo mengi ambayo Jamii zetu zinaona kama ni uhuni lakini kwa jicho la pili mambo haya yanasaidia sana kuimarisha Afya ya mwili na akili kwa ujumla

Ongeza zako

Nawasilisha
Wako mtiifu,
KENGE 01
 
Na Kenge,

Katika jamii kuna mambo ambayo kwa namna moja au nyingine yanaonekana ni uhuni au kinyume na maadili na tamaduni zetu.Lakini kimsingi mambo hayo ni muhimu na yanasaidia sana katika jamii.Ni vile kundi la watu wachache wanaofanya mambo hayo yasikubalike.

1.Massage
View attachment 2725734
Massage ni kinga na Tiba moja nzuri sana kwa mwanadamu.Tupo kwenye Tukirudi darasani kusoma Baiolojia tutakuta mwanadamu yupo ktk kingdom ya wanyama,Kundi Mamalia na soishi ya Vertabrates.Verterbrate ni viumbe wenye UTI wa mgongo.

Uti wa mgongo ni makutano ya mishipa ya fahamu(nyuzi) kutoka maeneo mbalimbali ya mwilini.UTI unamifula laini iitwayo verterbrae ambazo ni kama visahani,Mifupa hii ni milaini kiasi kwamba ni rahisi kuathirika na shughuli mbalimbali tuzifanyazo kama vile kazi,kutembea,kukimbia,kukaa.

Sasa baada ya shughuli nyingi za siku nzima kama ukijijengea ratiba ya kufanya massage hakika Afya yako itaimarika zaidi.Kwa bahati mbaya sehemu za kufanyia massage(Massage Pallor) zimegeuka madanguro huwezi kuingia kama Nia yako ni kupata massage tu kuna huduma nyeusi zinafanyika mule ndani ambapo uwezi kutoka salama hasa kwa wanaume.Hii inafanya massage ionekane ni uhuni.

2.Kuogelea Swimming pool
.Mara nyingi nchi zilizoendelea kipaumbele cha nyumba ni pamoja na kuwepo bwawa la kuogelea.Kuoga/kuogelea ni Tiba na kinga nyingine nzuri sana kwa Afya ya mwanadamu
View attachment 2725735
Hakuna nyumba yenye Swimming pool watu wake wakafa kwa Presha,Shinikizo la damu,Kisukari na magonjwa mengine mengi labda kama hawaogelei.

Kuogelea ni zoezi la cardio linaupa mwili Aerobic respiration(Oxygen nyingi) ambayo huimarisha Cell za mwili na kuuweka mwili sawa.

Pia kuogelea huifanya ngozi kuwa laini na yakuvutia. Kwa bahati mbaya Jamii zetu wakiona mtu amejenga bwawa utasikia "watoto watafia humo" mara "Ile nyumba wanajifanya wazungu "

Licha ya hayo baadhi ya watu hawaheshimu maadili ya mavazi hasa wanawake hivyo kupelekea jamii kuona(kuogelea) ni uhuni .

3.Kwenda gym.
View attachment 2725736
Kuweka mwili vizuri inahitaji mazoezi ya kutosha hasa kwa wanaume.Kama ni mgeni ukienda gym utakutana na Trainer atakupa muongozo na vitu hatari kama vile baadhi ya mikao inayoweza kusababisha maumivu wakati unanyanyua vitu vizito..

Kwa bahati mbaya jamii yetu inatazama kama kwenda GYM nao ni uhuni.Na kwa jinsia KE ukienda gym utaonekana unatafta mabwana watunisha misuli na mambo kama hayo.

Licha ya kuwepo vijana ambao nao hawana uelewa zaidi ya faida za mazoezi ya GYM kazi yao wanataka kupata mwili mzuri wa mapenzi mfano six packs,Kifua,Sholder hawa utakuta wanashinda GYM siku nzima ndio sababu jamii inaona kwenda GYM ni uhuni.

4.Kushiriki marathon
View attachment 2725737
Kwasasa kuna makongamano mbalimbali kutoka kwa taasisi au kampuni.Zinahamasisha kukimbia jogging.Lengo likiwa ni kuhamasisha watu kufanya maziezi.
View attachment 2725740
Lakini jamii imepokea ujumbe huo kitofauti kwani wengi wanaoshiriki marathon hizi wanaonekana kama wahuni.
View attachment 2725741
(Picha kutoka kwa C.ndosi)

Yapo mambo mengi ambayo Jamii zetu zinaona kama ni uhuni lakini kwa jicho la pili mambo haya yanasaidia sana kuimarisha Afya ya mwili na akili kwa ujumla

Ongeza zako.....

Nawasilisha
Wako mtiifu,
KENGE 01
Huyo dada mguu huo nimeupenda
 
Back
Top Bottom