Kama kukasirika kasirika tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama kukasirika kasirika tu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tata, May 30, 2012.

 1. T

  Tata JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  SMS01:

  "Sipigi simu na wala sijishughulishi na huyo mamako. Hata ukisafiri simpeleki hospital nisingekuwa mimi ungejua kama mama yako ana tatizo hilo. Hilo la mzigo umeona nalo neno la kukasirika, kama mme wake anasema mnao mzigo why me nisiseme. Kama kukasirika kasirika tu".


  SMS02:
  Mimi nataka kuondoka kwenye nyumba yako. Naomba unipe go ahead.


  Kwa ufupi huu ni ujumbe wa SMS ulioandikwa na mke kwenda kwa mume wake wa ndoa baada ya kutokea kutoelewana juu ya uwepo wa mama ya mume (yaani mamamkwe) nyumbani kwao. Ulifuatana kwa tofauti ya takribani wiki moja.

  Mama mkwe huyo ni mtu mzima mwenye umri wa zaidi ya miaka sabini na ni mgonjwa ambaye hawezi tena kujitegemea. Hivyo mama huyu anahitaji msaada wa karibu wa watoto wake ili aweze kuishi.

  Mke ana mtazamo kuwa mama mkwe wake amekuwa ni mzigo usiobebeka unaohitajika kuondolewa hapo nyumbani wakati ambapo mme anasisitiza kuwa mama yake kamwe hawezi kuwa hawezi kamwe kuwa mzigo kwake. Kimsingi mume anaamini kuwa anawajibika kumtunza mama yake katika hali hiyo mpaka hapo ama atakapopona au vinginevyo. Pia mume hapendi kusikia mama yake akifananishwa na mzigo kwani mama huyu ndiye hasa aliyemlea mme mtu akiwa mdogo baada ya baba yake kuwatelekeza na mama huyu na kuamua kuoa mke mwingine.

  Baada ya sintofahamu kutokea mke ameamua kugoma kuongea (na kutoa ile huduma nyingine) na mume wake na kama haitoshi amemtumia ujumbe huu wa SMS akirejea mazungumzo yao ya awali ambayo walishindwa kuelewana. Kuhusu simu mume alimwomba mke wake ampigie daktar anaye ndiye anamtibu mama huyu ili kuweka appointment ya kwenda kumuona.

  Ndugu zangu wake kwa waume hebu tushauriane hatua muafaka za kuchukua kutatua changamoto kama hii.

   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  poleni........
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  amwache aondoke ...
  huyo mwanamke hafai kabisa..
  akafie mbali huko....
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hapo hakika maji yamezidi unga kwa habari ya mahusiano. Lakini kwa ujumla huyo si mke, na anatakiwa awe discarded haraka iwezekanavyo!
   
 5. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Hafai kabisaaaa
   
 6. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ndio maana uislam ukaruhusu mwanamume kuoa zaidi ya mke mmoja
  kiburi hicho angepata wapi ndio kwanza angejifunza kupitia wenzake
  kwa staili hii kama ni kaka yangu tamsaidia kumuandikia talaka
   
 7. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hivi utamfananishaje mama wa mwenzio na mzigo? huyo dada kakosea sana, na kama anasoma JF anatakiwa kuomba msamaha kwa mumewe na pia kwa MUNGU.
  Mimi huwa sifagilii kukaa na mama mkwe ndani ya nyumba, lakini inapotokea kuwa ni mgonjwa huwa nakuwa wa kwanza kudai aje nyumbani, hata kama ana matatizo yake huwa hayanihusu, ninachokifanya ni kuhakikisha anatibiwa vizuri na kupata chakula kizuri ili apone haraka arudi kwake, maana mgonjwa akiwa mbali na mkijua kabisa hakuna mtu wa kumwangalia ipaswavyo huwa tension inahamia kwa mgonjwa.
   
 8. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyo dada kakosea lakini na hili tuliangalie na upande mwingine maana kuna wanaume wengine wanahisi mke ndo punda, hata kanga za mama yake hafui au hata ajitolee kusafisha chumba anacholala mama yake ili tuone anakumbuka alinyonya hilo ziwa basi. nafikiri tungepata habari ya upande wa pili tujue
   
 9. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ndio maana watu tunashauriwa kufunga ndoa na watu tunaowapenda hasa! Ni kweli kumlea huyo mama ni mzigo, especially kama mke hasaidiwi ipasavyo na wanafamilia wengine. Ila Some words are better not spoken!Kama unayo baki nayo moyoni tu.
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  DAh pole ila ninaomba kuwakumbusha kina kaka kuwa mnapooa/oana na wenzi wenu jueni kuwa mnacease kuwa wenye mamlaka ya mwisho na maamuzi binafsi ndani ya nyumba. Ni wazi kuwa mama umemleta kwa kulazimisha pasipo kukubaliana (kushawishiwa) na mwenzi wako. Kama kuna makubaliano ya kumuhudumia Mama hapo kwenu si rahisi kwa mwanamke kukujibu haya.

  Wanawake tumeumbbwa tofauti, wapo wale ambao immediately baada ya kuolewa anauvaa u-toto wa wazazi wa ande ya mumewe na kulichukulia kuwa ni wazazi wake ambapo huwa mwepesi yeye kabla hata mume hajasema, kusuggest kumleta mama nyumbani na kumhudumia kwa karibu. Ana kheri ampataye mke wa aina hii ila hata kama mkeo ni mzito katika hili, usichukulie mabavu kuwa eti kwa vile umeoa, nyumba mnayoishi ni yako wewe n.k ndo ujiamlie tu umlete mama hapo bila kushauriana na mkeo.

  Wanawake wengi hupenda kushirikishwa hata kama anajua kabisa kuwa hana uwezo wa kukushawishi otherwiae but ukimshirikisha hata kwa kauli taarifa..kuwa Wifey nafikiri tumlete mama hapa ili aweze kupata matibabu kwa urahisi mke wangu, nategemea utanisaidia katika hili....... inatosha. Lakini imefika alfajiri, jioni unekuja nakupokea na mama Mkwe nyuma kha.....kwanza ntaanzajenga chuki kwa kuwa ameninyima haki yangu ya kukukiss mlangoni siku hiyo!
   
 11. bahatika

  bahatika Senior Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwakweli huyo dada ana roho ngumu jamani, je kama angekuwa mama yako mzazi ungemwitwa mzigo, mi nadhani alikuwa anataka kuondoka mda mrefu hapo ndo kapata sababu, amuache aende
   
 12. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Pole yake mume! Nafikiri kama ana dada ampeleke mama kwa dada. Tukisema amwache aondoke mama atakosa wa kumhudumia. Tusimlaumu huyu mke, kumuhudumis ma mkwe si wajibu wake wa ndoa though kibinadamu alitakiwa kufanya. Apewe ushauri na mtu wa imani angalau basi afanye kwaajili ya Mungu.
   
 13. Y

  Yetuwote Senior Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamekuwa kwenye ndoa muda gani sasa? Hili litasaidia kujua ushauri gani nitoe.
   
 14. m

  mmanga mswahili Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uislamu ndio ndio inayokwenda sambamba na mazingira ya mwanaadamu
   
 15. s

  sangija Senior Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kakosea kumuita mzigo ila huyo mume yeye anachangia kwa kiasi gani kumsaidia mama yake? Usikute kamleta hapo tu na mke ndo mwenye jukumu kwa kwanzia kufua, kumwogesha, kumpeleka chooni kama hilo linawezekana, kumlisha n.k. Alafu ukute bado kuna watoto ambao nao wanamhitaji.

  Atafute utaratibu mzuri wa kumwangalia mama yake hapo hapo kwao bila kuruhusu mke wake alemewe na kazi. Nna uhakika akifanya hivyo na kama mkewe hamchukii huyo mama hawatokuwa na matatizo tena.
   
 17. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tupa kele huyo
   
 18. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ninamuacha tu aende zake, mimi nitamtibu mamangu hadi hapo Mungu atakapotekeleza alichokiamua. Yaani baada ya ujumbe huo wa pili, ningempa go ahead, na ningeomba likizo kazini nimuuguze mamangu. Na kutoka hapo nisingemuuliza kitu huyo mke wala nisingejishughulisha naye tena. Hawa wake zetu ndiyo huwa wanatutafutia laana kutoka kwa wazazi wetu, halafu zikishatupata wao wanatukimbia. I better miss her, nibaki na baraka za wazazi there are milions of women outthere looking for men.
   
 19. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  anatingisha kiberiti tu! ataondoka jua litampiga atarudi, au anadhani hao wa nje watamthamini kama mumewe?? wanamtamani na kumtaka coz yupo kwa mume wake, once akitoka hapo, atauona mziki wake, ila mmhhhh nimeumia sana, amefanya vibaya sana!
   
 20. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,023
  Likes Received: 2,645
  Trophy Points: 280
  Huyo mke wa huyo jamaa anachemsha sana,ukiolewa/kuowa mnaingia mkataba wa kuishi pamoja kwenye shida na raha,sasa kwa muono wangu hapo ni penye shida kwahiyo huyo mke awe mvumilivu mpaka shida hiyo ipite kwani you never know kesho inaweza kuwa ni mama au baba wa mwanamke,naye kafikia mahali hajiwezi itabidi mwanaume naye akubali kuubeba huo mnaouita mzigo(ametumia neno baya sana kwa mama wa mwenzake) na hiyo ndiyo ndoa kinyume cha hapo ndoa inakuwa ni batili.
   
Loading...