Kama Katiba inasema Mbunge akifukuzwa uanachama Ubunge wake unakoma, ni nani anawalinda Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
539
1,000
Hakika inashangaza sana kuona baadhi ya Viongozi wetu Walioapa Kuilinda Katiba lakini ndio Wanaikanyaga kwa Makusudi tena Hadharani.Kwa Mujibu wa Katiba tuna aina mbili za Wabunge Wakuchaguliwa na Wakuteuliwa.

Na ili uwe Mbunge lazima uwe Mwanachama wa Chama cha Siasa. Moja ya Sababu za kukoma kwa Ubunge ni pamoja na Kufukuzwa Uanachama. CHADEMA imewafukuza Wabunge 19 Uanachama wao lakini Mpaka leo bado ni Wabunge. Swali la kujiuliza:

Kwanini bado ni Wabunge?

Nani anawalinda?

Kwanini awalinde licha ya kuwa wamemfukuzwa Uanachama?

Tunakuomba Mhe. Rais hebu ingilia kati suala hilo kwa Hao Wanaoichezea Katiba na pia Kuokoa Pesa wanazolipwa Wabunge hao ambazo ni Kodi za Wananchi Masikini wa nchi hii.
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
63,070
2,000
Ni yuleyule aliyemlinda bosi wa bandari na majizi mengine

Ni yuleyule aliyemlinda Musiba kuwatukana viongozi mbalimbali wakiwemo wastaafu

Ni yuleyule aliyelinda wauaji na watekaji wasiojulikana.

Ni yuleyule aliyelinda mpasuko wa umoja wa kitaifa kwa kushangilia ubaguzi na unyanyasaji kwa wasimuabudu

Ni yuleyule aliyejipanga kwenda kuongoza malaika.

Kiongozi bora, jabali la Afrika na kiboko ya mabeberu.

Mwendazake.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,813
2,000
Kwani.mkutano mkuu na baraza kuu lilishafanyika kuridhia kufukuzwa kwao? walikata rufaa na hiyo rufaa haijasikilizwa hadi leo jiulize hulo Chadema mkutano wa baraza kuu mbona umeyeyukia hewani kulikoni?

Msisukumie Ndugai
 

Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
660
1,000
Sijawahi kuona nchi ya ajabu kama hii sasa sinema hii starling kafa yataibuka mengi sana ni suala la muda tu enedelea kuomba Mungu hajawahi kushindwa kaondoa malaika gabrieli wa chattle itakuahaya ni mambo madogo mno
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom