Kama Katiba inasema Mbunge akifukuzwa uanachama Ubunge wake unakoma, ni nani anawalinda Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA?

Mnakumbuka wale wabunge 19 walioingizwa bungeni kwa kuaminisha umma kuwa ni wa CDM wakati hawakupitishwa na CDM.

Kibaya zaidi kuna mmoja alikwenda kuchukuliwa mahabusu na kuja bungeni kuapishwa.

Magu alichukia sana hili jambo la wafanyakazi hewa kiasi kwamba ilifanywa ukaguzi nchi nzima kuwabaini.

Cha kushangaza ni Magu huyohuyo aliyewaingiza wabunge hewa 19 bungeni na wamekuwa wakilipwa fedha na walipa kodi.
 
Mnakumbuka wale wabunge 19 walioingizwa bungeni kwa kuaminisha umma kuwa ni wa CHADEMA wakati hawakupitishwa na CDM.
Kibaya zaidi kuna mmoja alikwenda kuchukuliwa mahabusu na kuja bungeni kuapishwa...
Hehehehe, mmoja nilimuona akimlipua Dr Kimei
 
Hakika inashangaza sana kuona baadhi ya Viongozi wetu Walioapa Kuilinda Katiba lakini ndio Wanaikanyaga kwa Makusudi tena Hadharani.Kwa Mujibu wa Katiba tuna aina mbili za Wabunge Wakuchaguliwa na Wakuteuliwa...
Hao ni wahujumu uchumi maana wanachukua malipo wasiyo stahili.

Ndugaye anastahili awe jela muda huu maana huo ni ufisadi.
 
Ni yuleyule aliyemlinda bosi wa bandari na majizi mengine

Ni yuleyule aliyemlinda Musiba kuwatukana viongozi mbalimbali wakiwemo wastaafu...
Aliyebariki ufisadi wa kutisha kuendelea kutamalaki hapa nchini.
 
Kwani.mkutano mkuu na baraza kuu lilishafanyika kuridhia kufukuzwa kwao? walikata rufaa na hiyo rufaa haijasikilizwa hadi leo jiulize hulo Chadema mkutano wa baraza kuu mbona umeyeyukia hewani kulikoni?

Msisukumie Ndugai
Rufaa maamuzi yake yanajulikana tu kuwa tumewafuta na kuwavua uanachama.
 
Acheni ubabaishaji walikata rufaa baraza kuu la Chadema hafi leo hii hamjakutana
Rufaa ni kurudishiwa uanachama sio kulinda ubunge otherwise wangeweka zuio mahakamani kama zitto.

Mbona Lipumba alipowavua wale wabunge 8 wa CUF hukumu ilitekelezwa mara moja na Ndugai hta haikusubiri majibu ya rufaa!!

Vipi sofia simba walisubiri majibu ya rufaa?

Mbona Lissu alivuliwa ubunge licha ya kesi kuwepo mahakamani!!

Tuache double standards kama utaratibu ni huu siku zote basi uendelee hadi kwa Kina Mdee
 
Kwani.mkutano mkuu na baraza kuu lilishafanyika kuridhia kufukuzwa kwao? walikata rufaa na hiyo rufaa haijasikilizwa hadi leo jiulize hulo Chadema mkutano wa baraza kuu mbona umeyeyukia hewani kulikoni?

Msisukumie Ndugai
Baraza kuu lilikua postponed sababu ya mlipuko wa Covid hata kamati kuu huwa wanakutana kwa Zoom conference call!!

Sasa mkutano wa level ya baraza kuu ni ngumu kuufanya kwa Video call ukizingatia wingi wa wajumbe na miundombinu ya mawasiliano hasa vijijini.

But muhimu ni kwamba hukumu ilipaswa itekelezwe na Bunge then hao kina Bulaya wangekimbilia mahakamani kuweka zuio la muda mpaka rufaa isikilizwe.

Sio eti rufaa ya baraza kuu ndio bunge lisubirie!! Hyo mbona haikuwezekana kipindi cha wabunge wa CUF na Sofia simba kuenguliwa?

Ile rufaa ni ya kuokoa uanachama haina uhusiano na ubunge wao kabisa sasa toka lini kuvuana uanachama ni concern ya spika? Yeye kazi yake ni kufikishiwa tu taarifa yenye minutes za kikao husika basi
 
Lete fact, hivi Kuna mwaka gani hapa chadema hawajapiga makelele ya uchaguzi mbovu mbona bungeni walikuwa wanaenda?
Ignorantia juris non excusat: meaninga; a legal principle holding that a person who is unaware of a law may not escape liability for violating that law merely by being unaware of its content.
 
Hakika inashangaza sana kuona baadhi ya Viongozi wetu Walioapa Kuilinda Katiba lakini ndio Wanaikanyaga kwa Makusudi tena Hadharani.Kwa Mujibu wa Katiba tuna aina mbili za Wabunge Wakuchaguliwa na Wakuteuliwa...
CAG alikague Bunge aone pesa ya walipakodi inavyopotezwa na Bunge bila sababu za msingi. Atathmini Bunge limeitia serikali hasara kiasi gani kwa kulipa mishahara na posho kwa wabunge ambao wamefukuzwa uanachama na hatua zichukuliwe.

TAKUKURU wachunguze huu ni wizi kama wizi mwingine kesi yake ni ya uhujumu uchumi.
 
Kwani.mkutano mkuu na baraza kuu lilishafanyika kuridhia kufukuzwa kwao? walikata rufaa na hiyo rufaa haijasikilizwa hadi leo jiulize hulo Chadema mkutano wa baraza kuu mbona umeyeyukia hewani kulikoni?

Msisukumie Ndugai
Tumekusikia braza tulia naibu spika wetu
 
Hakika inashangaza sana kuona baadhi ya Viongozi wetu Walioapa Kuilinda Katiba lakini ndio Wanaikanyaga kwa Makusudi tena Hadharani.Kwa Mujibu wa Katiba tuna aina mbili za Wabunge Wakuchaguliwa na Wakuteuliwa...
Wanawezaje kutunga sheria wakati ndiyo wavunja sheria namba moja, kwa nini wanawakilisha majimbo ya matumbo yao huku wanaiba kodi zetu. ni aibu mwizi wa kuku anafungwa wao wanaachwa? huu ni uonevu
 
Kwani.mkutano mkuu na baraza kuu lilishafanyika kuridhia kufukuzwa kwao? walikata rufaa na hiyo rufaa haijasikilizwa hadi leo jiulize hulo Chadema mkutano wa baraza kuu mbona umeyeyukia hewani kulikoni?

Msisukumie Ndugai
Huwezi kuhukumiwa kifungo bado upo uraiani unakuwa jela ukisubiri maamuzi ya mahakama ya juu, hivyo siyo wanachama mpaka kikao kitoe maamuzi hawatakiwi kuwapo bungeni hadi baraza kuu litoe maamuzi
 
Back
Top Bottom