Kama huna ngozi nene usigombee urais!

Rais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Weka kifungu cha sheria. Wewe ndo wale wanaompotosha huyo jamaa halafu serikali inashindwa kesi tunaingia hasara. Yale yale ya kujipendekeza tu.
 
Bado anatafuta
emoji23.png
emoji23.png
Mkumbushe mtani wako mkuu labda amesahau. Petro E. Mselewa mkuu bado tunasubiria jibu la swali la mtani wako Nyani..
 
Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini ambayo siyaelewi kabisa.

Inapotokea mtu maarufu anapomkosoa huyu rais wetu hadharani au inapotokea hata mtu tu wa kawaida akafanya au kusema kitu fulani ambacho kinaonekana kama kinamkosoa Rais Magufuli basi mtu huyo ataanza kuandamwa andamwa na hata kukamatwa.

Rejeeni habari za yule dogo wa UDSM alipokamatwa kwa sababu ya alichokifanya kuhusu majengo ya mabweni mapya ya wanafunzi chuoni hapo. Rejeeni suala na Nape kutishiwa na bastola mchana kweupe. Rejeeni suala la mbunge Bashe kusumbuliwa na polisi au sijui usalama wa taifa wale. Rejeeni suala la Lissu kukamatwa kamatwa na kuwekwa rumande kisa katumia lugha kali dhidi ya Magufuli.

Kwenye nchi za kidemokrasia, kama tunavodai na sisi nchi yetu iko hivyo, suala la viongozi kukosolewa, kudhihakiwa, kutukanwa, na kadhalika, ni jambo la kawaida sana.

Tazama kote duniani kwenye demokrasia na hayo mambo utayaona.

Sasa kwa nini hapa kwetu huyu rais wetu akisemwa vibaya huyo mtu aliyemsema vibaya anaanza kusumbuliwa?

Askofu Kakobe sasa hivi tumesikia habari kuwa eti atakamatwa kisa eti kadiriki kumkosoa rais.

Hivi kumkosoa rais au hata kumkebehi na kumdhihaki ni kosa kwenye nchi hii?

Kwani huyu rais wetu wakati anagombea huo urais alikuwa na matarajio gani labda? Kwamba akishatangazwa kuwa yeye ndo mshindi basi kila mtu ndo atakubaliana naye na kumuunga mkono kwenye kila kitu? Hilo kamwe haliwezekani na halitowezekana Tanzania hii.

Labda linawezekana tu huko Korea Kaskazini ingawa hata huko sidhani kama watu wote wanamuunga mkono huyo Kiduku.

Nawashauri CCM waunde kitengo cha ‘War room’ mahsusi kwa kujibu mapigo ki-hoja na kuacha kutumia vitisho vya vyombo vya dola kujibu mapigo kwa kutishia watu.
Leo angalau umeandika kitu serious. maana siku zote unabwabwaja tu. kwa hiyo na wewe umeanza kuiona hiyo eeh?? na Bado! Magufuli ataendelea kuminya mpaka kieleweke!
 
Hahahaaa

Huwa hunielewi kabisa wewe.

Pole.
 
Maziro km bashite ndo washauri wa rais ambaye naye ana phd feki hapo chacha
 
Vijana wa kitanzania bwana; tumejivika akili ya kutoelewa. Nani alikuambiwa atakamatwa. Kwanza kwenda kutoa maelezo ya kauli ulizozitoa ni kukamatwa. Mbona ni jambo la kawaida. Lowasa alienda kutoa maelezo juu ya kauli yake; Katibu wa chadema alienda kutoa maelezo juu ya kauli aliyoitoa. Je hili ni geni?. lazima ifikie wakati mtoke katika hayo matongotongo mliyojivika na mje na ajenda zenye tija.
hamchelewi kusema takwimu za kiserikali hazijaonesha kama mkuu wetu yupo na dhambi .Anaefaa kusemea mkuu wetu kakengeuka ni ile taasis ilopewa mamuraka kutoa taarifa izo
 
Rais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Nchi yenye watu milioni hamsini LAZIMA watakuwepo ''wendawazimu'' ambao hawajui lugha ya staha. Ni wengi tena sana. Na ndio lengo la mwanzisha mada i.e. Urais unataka uvumilivu. Rais ni kiongozi wa waropokaji, wenye hekima, vichaa na wanaokebehi! Umeshindwa kuelewa lengo la mwanzisha thread? Wewe unajiita mwanasheria lakini nadhani uu kilaza wa kiwango cha juu!
 
kukoselewa Kwenye Siasa Ni Jambo La Kawaida Sio Tanzania Tu Mpaka Nchi Za Nje

Wengi wanapenda kukosoa kwa kwa njia ya matusi na hii inaletwa na jazba wakati watu wanaona PERSONAL INTERESTS zao hatitekelezwi

Viongozi wenye busara uchukua ushauri na kuyapuuzia matusi, UKUBWA NI JA; Mtu unapochagua kuwa kiongozi inabidi utarajie kukoselewa

Viongozi wetu wajifunze sana kukubali kukoselewa
 
we nyani kaa ujue Urais ni Taasisi.

Unaelewa vizuri dhana ya Urais ni Taasisi.

Ushawahi msikia Magufuli akiwajibu au kuwa attack directly kama wewe unavyodhani.

Acha Taasisi ya Urais ilindwe kwa namna inavyofaa.
 
Juhaa kabisa wewe!
 
Wengine wanataka uraisi wa urahisi.

Something's gotta give. No free lunch.
 
Urais ni taasisi nyeti mnoo, ina heshma zake na lazma heshma hizo zilindwe kwa gharama yeyote, nijuavyo hata pale kwenye ile taasisi akikaa Mbowe au Lissu lazma paheshimiwe
 
Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini ambayo siyaelewi kabisa.

Inapotokea mtu maarufu anapomkosoa huyu rais wetu hadharani au inapotokea hata mtu tu wa kawaida akafanya au kusema kitu fulani ambacho kinaonekana kama kinamkosoa Rais Magufuli basi mtu huyo ataanza kuandamwa andamwa na hata kukamatwa.

Rejeeni habari za yule dogo wa UDSM alipokamatwa kwa sababu ya alichokifanya kuhusu majengo ya mabweni mapya ya wanafunzi chuoni hapo. Rejeeni suala na Nape kutishiwa na bastola mchana kweupe. Rejeeni suala la mbunge Bashe kusumbuliwa na polisi au sijui usalama wa taifa wale. Rejeeni suala la Lissu kukamatwa kamatwa na kuwekwa rumande kisa katumia lugha kali dhidi ya Magufuli.

Kwenye nchi za kidemokrasia, kama tunavodai na sisi nchi yetu iko hivyo, suala la viongozi kukosolewa, kudhihakiwa, kutukanwa, na kadhalika, ni jambo la kawaida sana.

Tazama kote duniani kwenye demokrasia na hayo mambo utayaona.

Sasa kwa nini hapa kwetu huyu rais wetu akisemwa vibaya huyo mtu aliyemsema vibaya anaanza kusumbuliwa?

Askofu Kakobe sasa hivi tumesikia habari kuwa eti atakamatwa kisa eti kadiriki kumkosoa rais.

Hivi kumkosoa rais au hata kumkebehi na kumdhihaki ni kosa kwenye nchi hii?

Kwani huyu rais wetu wakati anagombea huo urais alikuwa na matarajio gani labda? Kwamba akishatangazwa kuwa yeye ndo mshindi basi kila mtu ndo atakubaliana naye na kumuunga mkono kwenye kila kitu? Hilo kamwe haliwezekani na halitowezekana Tanzania hii.

Labda linawezekana tu huko Korea Kaskazini ingawa hata huko sidhani kama watu wote wanamuunga mkono huyo Kiduku.

Nawashauri CCM waunde kitengo cha ‘War room’ mahsusi kwa kujibu mapigo ki-hoja na kuacha kutumia vitisho vya vyombo vya dola kujibu mapigo kwa kutishia watu.
now you are back to your sense thank God
 
Sheria gani inakataza kumdhihaki rais? Sheria gani inakataza kumkejeli rais?

Kwa utawala huu hizo sheria za kukataza watu "wasimdhihaki" na "kumkejeli" rais zitatungwa ili kumridhisha huyu rais asiyependa na kuogopa kukosolewa. Wakishatunga "sheria" hizo, nchi ndio itakuwa rasmi ya chama kimoja. Inasikitisha na kukera sana!
 
Back
Top Bottom