Kama huna ngozi nene usigombee urais!

Kama huna ngozi nene usigombee urais!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,175
Reaction score
143,967
Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini ambayo siyaelewi kabisa.

Inapotokea mtu maarufu anapomkosoa huyu rais wetu hadharani au inapotokea hata mtu tu wa kawaida akafanya au kusema kitu fulani ambacho kinaonekana kama kinamkosoa Rais Magufuli basi mtu huyo ataanza kuandamwa andamwa na hata kukamatwa.

Rejeeni habari za yule dogo wa UDSM alipokamatwa kwa sababu ya alichokifanya kuhusu majengo ya mabweni mapya ya wanafunzi chuoni hapo. Rejeeni suala na Nape kutishiwa na bastola mchana kweupe. Rejeeni suala la mbunge Bashe kusumbuliwa na polisi au sijui usalama wa taifa wale. Rejeeni suala la Lissu kukamatwa kamatwa na kuwekwa rumande kisa katumia lugha kali dhidi ya Magufuli.

Kwenye nchi za kidemokrasia, kama tunavodai na sisi nchi yetu iko hivyo, suala la viongozi kukosolewa, kudhihakiwa, kutukanwa, na kadhalika, ni jambo la kawaida sana.

Tazama kote duniani kwenye demokrasia na hayo mambo utayaona.

Sasa kwa nini hapa kwetu huyu rais wetu akisemwa vibaya huyo mtu aliyemsema vibaya anaanza kusumbuliwa?

Askofu Kakobe sasa hivi tumesikia habari kuwa eti atakamatwa kisa eti kadiriki kumkosoa rais.

Hivi kumkosoa rais au hata kumkebehi na kumdhihaki ni kosa kwenye nchi hii?

Kwani huyu rais wetu wakati anagombea huo urais alikuwa na matarajio gani labda? Kwamba akishatangazwa kuwa yeye ndo mshindi basi kila mtu ndo atakubaliana naye na kumuunga mkono kwenye kila kitu? Hilo kamwe haliwezekani na halitowezekana Tanzania hii.

Labda linawezekana tu huko Korea Kaskazini ingawa hata huko sidhani kama watu wote wanamuunga mkono huyo Kiduku.

Nawashauri CCM waunde kitengo cha ‘War room’ mahsusi kwa kujibu mapigo ki-hoja na kuacha kutumia vitisho vya vyombo vya dola kujibu mapigo kwa kutishia watu.
 
Vijana wa kitanzania bwana; tumejivika akili ya kutoelewa. Nani alikuambiwa atakamatwa. Kwanza kwenda kutoa maelezo ya kauli ulizozitoa ni kukamatwa. Mbona ni jambo la kawaida. Lowasa alienda kutoa maelezo juu ya kauli yake; Katibu wa chadema alienda kutoa maelezo juu ya kauli aliyoitoa. Je hili ni geni?. lazima ifikie wakati mtoke katika hayo matongotongo mliyojivika na mje na ajenda zenye tija.
 
Aende kutoa maelezo ya nini sasa?

Kusema rais atubu ni kosa? Ni sababu kweli ya mtu kwenda kutolea maelezo kituo cha polisi?

What is this now? Nazi Germany??

Dumbest!
 
Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini ambayo siyaelewi kabisa.

Inapotokea mtu maarufu anapomkosoa huyu rais wetu hadharani au inapotokea hata mtu tu wa kawaida akafanya au kusema kitu fulani ambacho kinaonekana kama kinamkosoa Rais Magufuli basi mtu huyo ataanza kuandamwa andamwa na hata kukamatwa.

Rejeeni habari za yule dogo wa UDSM alipokamatwa kwa sababu ya alichokifanya kuhusu majengo ya mabweni mapya ya wanafunzi chuoni hapo. Rejeeni suala na Nape kutishiwa na bastola mchana kweupe. Rejeeni suala la mbunge Bashe kusumbuliwa na polisi au sijui usalama wa taifa wale. Rejeeni suala la Lissu kukamatwa kamatwa na kuwekwa rumande kisa katumia lugha kali dhidi ya Magufuli.

Kwenye nchi za kidemokrasia, kama tunavodai na sisi nchi yetu iko hivyo, suala la viongozi kukosolewa, kudhihakiwa, kutukanwa, na kadhalika, ni jambo la kawaida sana.

Tazama kote duniani kwenye demokrasia na hayo mambo utayaona.

Sasa kwa nini hapa kwetu huyu rais wetu akisemwa vibaya huyo mtu aliyemsema vibaya anaanza kusumbuliwa?

Askofu Kakobe sasa hivi tumesikia habari kuwa eti atakamatwa kisa eti kadiriki kumkosoa rais.

Hivi kumkosoa rais au hata kumkebehi na kumdhihaki ni kosa kwenye nchi hii?

Kwani huyu rais wetu wakati anagombea huo urais alikuwa na matarajio gani labda? Kwamba akishatangazwa kuwa yeye ndo mshindi basi kila mtu ndo atakubaliana naye na kumuunga mkono kwenye kila kitu? Hilo kamwe haliwezekani na halitowezekana Tanzania hii.

Labda linawezekana tu huko Korea Kaskazini ingawa hata huko sidhani kama watu wote wanamuunga mkono huyo Kiduku.

Nawashauri CCM waunde kitengo cha ‘War room’ mahsusi kwa kujibu mapigo ki-hoja na kuacha kutumia vitisho vya vyombo vya dola kujibu mapigo kwa kutishia watu.

Magufuli is a gutless crook! Jamaa anajifanya ubabe kumbe mchuchu tu! Kama kweli mbabe afute ‘demokrasia’ nchini. Yeye ameonyesha he don give a dang about Katiba na sheria. Sasa atoe tamko tu la kusema “Tanzania sasa haifuati demokrasia”. Ama atumie wingi wa mazombie yake yaliyo mengi Bungeni kufuta ‘demokrasia’. Hakuna atakayeendelea kumkosoa kwa kutofuata demokrasia.

Ila as long as Katiba ya sasa (pamoja na ubovu wake) inatamka Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, basi inabidi awe na ngozi ngumu tu! La sivyo ataendelea kupoteza muda kwa kukamata watu, kwani it’s just the beginning!!
 
Heshima, Comrade.

Kukata mti ni kung'oa mzizi na siyo kuchanja matawi. Kuzuia kujikwaa ni kung'oa kisiki na siyo kufukia na kusawazisha ardhi ya ulikojikwaa.

Rais ni zao la Jamii ya Kitanzania. Hajatokea Peponi wala kusikojulikana. Katokea katika Jamii hiihii isopenda kukosolewa. Hivi ni Mtanzania gani/yupi ukimkosoa kwa mantiki hang'aki na kukunja ndita?.

Kuanzia ndani ya Familia, ikiongozwa na asasi iitwayo baba. Je baba anakosolewa?. Tumekwenda mbali mpaka tumejiumbia semi za hovyo "Mkubwa hakosei". Unategemea nini?.

Shuleni, hosipitalini, katika nyumba za Ibada, katika vyombo vya usafiri hakuna anayetaka kubishana kimantiki. Ukimkosoa anakuundia tume. Na mwisho mnaishia kubaya.

Binafsi sidhani kama kumshutumu Rais ni sahihi ilhali ni zao la Jamii yetu. Huu utamaduni tumeujenga kuanzia karne na karne. Tusing'ake, tuukubali na tuurekebishe kwa kuanzia kwenye misingi.

Tukate mti kwa kungoa mzizi na siyo tuchanje matawi. Tungoe kisiki na siyo kufukia ardhi ya tulikojikwaa.
 
Hakuna binadamu anaesifiwa, Rais akubaliane na hali halisi kuwa hiyo ni nafasi ya watu hivyo wapo watakao mkubali wapo watakao mkataa kama ilivyo kwenye sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom